TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

#TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary afariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa taarifa zaidi, kurasa za ZBC @zbc_zanzibar zitaendelea kuwajuza.

#ZBCUpdates
 

Attachments

  • 5369019-d83af5714991bb9e1c8b3011c18a2151 (1).mp4
    2.3 MB
Mungu akujaaalie na kukupa Shida Kadri ya Dua za watesi wako wewe uliye mwelevu.
Usiamini ujinga ,kufa kupo labda kama sio binadamu.. Ukitaka kukimbia kifo na maumivu ya kufiwa basi usizae mtoto...
 
#TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary afariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa taarifa zaidi, kurasa za ZBC @zbc_zanzibar zitaendelea kuwajuza.

#ZBCUpdates
Mods please change the title

Tunaweza kuwa na grievance zetu lakini Tuache kuruhusu watu wanaonormalize vitu vya hivyo kama huyu mleta mada
 
Usiamini ujinga ,kufa kupo labda kama sio binadamu.. Ukitaka kukimbia kifo na maumivu ya kufiwa basi usizae mtoto...
Huko Tanga mmeshatuletea Msemo wenu;
"WAZURI HAWAFI"
Majirani zenu hapo Ng'ambo wakapigilia Msumari
"KIFO NI KIFO TUUU".
 
Innallillah wainnah ilayh rajiuun, nguli wa utangazaji, nilimjua kwa mara ya kwanza miaka ya 2007's wakati akitangaza Epl
Kumbe tuko na wanetu hapa.Mimi nimesoma naye ila alikuwa big brother kwangu nikiwa darasa la kwanza yuko darasa la saba.
Hata hivyo kutangulia sio kufika uzee ni tunu ujana ni mapito ya muda tuko pamoja mdogo wetu lazima uwe na historia yako.
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini

Alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1981 na kuitumikia hadi mwaka 1994 alipojiunga na kituo binafsi cha Radio One Stereo kinachomilikiwa na IPP

Mwaka 2003 aliondoka nchini na kujiunga na Radio Deusch Welle (DW) nchini Ujerumani, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa Idhaa ya Kiswahili

Mwaka 2015 aliamua kurejea nchini na kujiunga Azam Media ambako alifanya kazi hadi mwaka 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Mungu amweke mahala pema peponi mzee wetu.
Mbona una rukaruka, hujasema aliwahi kufanya kazi TBC kama Mkurugenzi Mkuu, inamaana aliruka akaingia Azam?

Anyway, RIP mwamba mpenda haki, bado unaishi kwenye mioyo ya watu wengi
 
Nilichojifunza na Wanangu Ntawafundisha na hata sasa mimi Binafsi mtaani naishi hivyo;

Kuna jamii ukiwa juu yao kwa Cheo au fursa au kipato akijua ukitoka wewe atapata yeye ni sheedar muda wowote unaenda kwa Sanda.
Unàmaanisha nini?
 
Back
Top Bottom