TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

Charles alikua ni mtu wa watu, Mtu wa haki na very fair

Sifa zake kuu ni wakati ule akiwa kwenye radio za Tunza bara hasa ITV na radio one

Yeye na marehemu Julius nyaisanga walinyanyua sana rpivate media

Tumkumbuke Kwa impact ya muda mrefu

Zanzibar alienda juzi tu baada ya Mwinyi kuwa rais
 

Attachments

  • 5369019-d83af5714991bb9e1c8b3011c18a2151 (1).mp4
    2.3 MB
Alikuwa mtenda haki katika kutoa mawasiliano au ni wale wale
Ni wale wale Ile issue ya Zanzibar kumiliki eneo upande wa bagamoyo aliishupalia Sana kuandika matangazo na kuyapost na kwenda kwenye media ngoja afe
 
Hili no tamko very fair Kwa kazi yakr

Hatq sisi tuna ardhi nchi nyingi sana tu

Zambia pekee tuna zaidi ya viwanja 10 Lusaka Tena prime areas

Hapo yeye amesoma taarifa ya umiliki wa ardhi ya smz huko bagamoyo

Ulitaka asemeje? Mbona tunakua wajinga aana siku hizi?
 
#TANZIA: Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary afariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa taarifa zaidi, kurasa za itvtz zitaendelea kuwajuza.

#ZBCUpdates
 
Tuishi kwa kupendana, tuache kufanyiana ubaya, hii dunia ni mapito tu.
Poleni sana.
R.I.P Charles daima tutakumbuka weledi wake katika Utangazaji wa Habari
 
RIP

Ulikuwa na roho ya upatanishi

Nakumbuka vile vikao vyetu ukiwa ITV jinsi ulivyowasaidia Wasanii mbalimbali Kimawazo akina Bishanga, JB, Kanumba, Ray, Richie tukiwa pale La Charls

Wengi hawajui umeshiriki kukuza vipaji vingi vya Sanaa nchini

Iringa mjini 1980s ulituachia kumbukumbu ya MC bora kabisa kwenye harusi ya Bilionea Mpangala wa Dar Young Africans
 
Daaah! Kumbukumbu ya sauti yake kichwani mwangu, ni ile ya ule mkwara wa WAZENJI kutupiga sisi WA BARA, eti TUMEVAMIA ARDHI YA WAZENJI ILIYOPO HUKU BARA!
 
#TANZIA: Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary afariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa taarifa zaidi, kurasa za itvtz zitaendelea kuwajuza.

#ZBCUpdates
Duh! R.I.P mwamba.

Huyu alikuwa mtangazaji Bora wa soka kuwahi kutokea hapa nchini Tanzania.

Cc Monetary doctor Al-mukheef
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini

Alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1981 na kuitumikia hadi mwaka 1994 alipojiunga na kituo binafsi cha Radio One Stereo kinachomilikiwa na IPP

Mwaka 2003 aliondoka nchini na kujiunga na Radio Deusch Welle (DW) nchini Ujerumani, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa Idhaa ya Kiswahili

Mwaka 2015 aliamua kurejea nchini na kujiunga Azam Media ambako alifanya kazi hadi mwaka 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Mungu amweke mahala pema peponi mzee wetu.
Very shocking.

May his soul rest well. We'll really miss him.
 
Daaah! Kumbukumbu ya sauti yake kichwani mwangu, ni ile ya ule mkwara wa WAZENJI kutupiga sisi WA BARA, eti TUMEVAMIA ARDHI YA WAZENJI ILIYOPO HUKU BARA!
Haya maneno utayakataa siku ukifiwa na mtu wa karibu sana
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini

Alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1981 na kuitumikia hadi mwaka 1994 alipojiunga na kituo binafsi cha Radio One Stereo kinachomilikiwa na IPP

Mwaka 2003 aliondoka nchini na kujiunga na Radio Deusch Welle (DW) nchini Ujerumani, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa Idhaa ya Kiswahili

Mwaka 2015 aliamua kurejea nchini na kujiunga Azam Media ambako alifanya kazi hadi mwaka 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Mungu amweke mahala pema peponi mzee wetu.

TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary afariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.


Kuandika => ALIYEKUWA ni kosa kubwa, sbb bado ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mauti yamemfika

Ukisema ALIYEKUWA - maana yake aliondoka au alistaafu nafasi hiyo kabla ya mauti kumfika, hivyo ujue kuandika vema kiswahili.
 
Back
Top Bottom