TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Ikulu ya Zanzibar, Charles Hillary afariki dunia

Nilikua nasikiliza mechi za Epl kwenye radio ilikua timu ikisawazisha goli unaskia anasema "moja moja"
Mkuu Kama una clip yake akitangaza kabumbu tuwekee maana nimeimisi sauti yake ya dhahabu.
 
TANZIA Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary afariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kuandika => ALIYEKUWA ni kosa kubwa, sbb bado ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi mauti yamemfika

Ukisema ALIYEKUWA - maana yake aliondoka au alistaafu nafasi hiyo kabla ya mauti kumfika, hivyo ujue kuandika vema kiswahili.
Kwahy jamaa bado n mkurugenzi huku akiwa mfu? 😂
Ww ndo ujue kuandika Kiswahili vyema.
 
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, Hilary amefariki baada ya kuugua ghafla na mauti yamemkuta akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila.

Marehemu Charles Hilary alizaliwa Zanzibar miaka 66 iliyopita eneo la Jang’ombe. Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini

Alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1981 na kuitumikia hadi mwaka 1994 alipojiunga na kituo binafsi cha Radio One Stereo kinachomilikiwa na IPP

Mwaka 2003 aliondoka nchini na kujiunga na Radio Deusch Welle (DW) nchini Ujerumani, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akiwa Idhaa ya Kiswahili

Mwaka 2015 aliamua kurejea nchini na kujiunga Azam Media ambako alifanya kazi hadi mwaka 2023. Alihitimisha muda wake akiwa Mkuu wa Idara ya redio ya UFM, baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar.

Mungu amweke mahala pema peponi mzee wetu.
Ameumaliza mwendo mapema zaidi akiwa na Nguvu zote,R.I.P bwana Hilary
 
Pia awasalimie Karem Besta,Eda Sanga,Uncle J Nyaisanga,Rehema Mwakangale,Zuberi Msabaha,Deo Kiduduye,Freddy Felix au Fredwa,Job aiza Kamwamto wa Kenya,Leondard Mambo Mbotela wa Kenya na na wengine
Ooh, kumbe mama 'Eda Sanga' alishatangulia mbele za haki? Alifariki mwaka gani, mkuu?
 
Marehemu mara ya kwanza namsikia mwaka 2005 BBC swahili kila weekend anatangaza mechi za EPL kwa kiswahili so tukiwa hatuna jero la kwenda kibanda umiza, tunaenda dukani kwa mangi (RIP MANGI) Anafungulia radio hadi mwisho..RIP legend..
Anasema siku aliyoumia ni siku timu yake ya Arsenal inakula 8 toka kwa MSN u huku yeye akiwa mtangazaji. Siku hiyo hata mimi niliumia sana.
 
Maisha ya Dunia yanapumbaza sana,tukiwa hai tunajisahau ..lakini katika kitu ambacho kinakuja bila hata taarifa basi ni kifo..vyote tutaviacha..
 
Kaugua ghafla 😭😭😭

Back
Top Bottom