Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera awaonya wasimamizi wa uchaguzi kuwa wataumbuka

Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera awaonya wasimamizi wa uchaguzi kuwa wataumbuka

Mimemskiliza Jana Mahera nikaona naye ameshapoteana na wahujumu wa Uchaguzi wameanza kutajana. Wagombea walikuwa wanashinda Ofisi za Tume kudai hizo Barua ila Tume ikawa inawazungusha Tu. Leo Kati ya siku 60 za kampeni zimebaki siku 12 ndio anawataka wakurugenzi watoe Barua Ili iweje?? Kimsingi ameshaona kuna kuumbuka mchana kweupe.

Watakaopewa Barua leo wanapaswa waende mahakamani kuzuia Uchaguzi katika maeneo Yao Ili wapate muda Sawa wa Kupiga Kampeni. Vinginevyo wakiingia uwanjani na wakashindwa, watapoteza sifa ya kukata rufaa huko mbeleni.

Aidha, wahakikishe hizo Barua zina tarehe halisi (ya Siku wanayopewa Barua) mana wanakuwaga na tabia ya ku-back-date Ili kufunika uovu wao.
 
Huyo hawezi kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi labda Mkurugenzi wa Maigiizo! Walichokifanya hadi sasa ni kumlinda pacha wao CCM.
 
Ndio mujue mnapoambiwa Tume sio Huru. Hii ni moja ya mfano.
 
Anaanza kurudi kwenye 'mstari' dakika za majeruhi baada ya kupima kina na kuona akimsikiliza Jiwe ataishia kwenye Sheria za kimataifa.

Bado Anapaswa kuwajibika. Asiwauzie kesi wasimamizi. Chaguzi katika maeneo barua zilipofichwa ziahirishwr waliofichiwa wapate muda wa kufanya kampeni zao.
 
Anaanza kurudi kwenye 'mstari' dakika za majeruhi baada ya kupima kina na kuona akimsikiliza Jiwe ataishia kwenye Sheria za kimataifa.

Bado Anapaswa kuwajibika. Asiwauzie kesi wasimamizi. Chaguzi katika maeneo barua zilipofichwa ziahirishwr waliofichiwa wapate muda wa kufanya kampeni zao. Kajifunza kwa yule polisi wa kinondoni. Sio zombe sio IGP, ni yeye na familia yake
 
Kwamba kuna Mgombea atakuwa hapigi kampeni muda huu akisubiri majibu ya rufaa na hana taarifa kwa kuwa wasimamizi labda wameficha barua?

Kwanini NEC isizipublish hizo barua kama anaamini zimefichwa? Kwanini NEC isiwaataarifu wagombea wenyewe moja kwa moja kwani wana contact numbers zao?

Hizi ni abradacadabra!
 
Alafu huyu jamaa sijui ni dhehebu gani?
Maana anayoyafanya na bado jumamosi au jumapili anabeba msaafu na kitabu cha nyimbo aah😬!!
Uzuri kila mtu atajibu mbele ya haki kwa kila alichokitenda hata kingekuwa kidogo kama sisimizi.
 
Nadhani ziara ya balozi wa dunia jana... pale Lumumba
 
Kila kiongozi ana mamlaka yake katika utekelezaji wa majukumu Kama mkurugenzi wa Tume alishatoa rufaa akatuma kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo Sasa analaumiwaje kwa wagombea kutopata hizo barua tusisahau kuwa Mkurugenzi wa Tume anasimamia uchaguzi nchi nzima ana mambo mengi ya kufanya kufuatilia kwa kila mtu Kama amepata barua ni jambo gumu Sana manake muda hausimami kumsubiri yeye ayafanye hayo.

Yeye kashafanya kwa nafasi yake Sasa hii statement pengine ametoa baada ya kusikia minong'ono Sasa anawatahadharisha walioko chini yake kwamba yeye ameshafanya yake wataumbuka wao waliofanya hujuma kwa mantiki hiyo yupo sahihi kabisa
 
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Mahera amewaonya wasimamizi wa uchaguzi ambao wameficha barua za uteuzi za wagombea wa ubunge na udiwani ambao walishinda rufaa zao kwa sababu majina na picha zao zitakuwepo kwenye karatasi za wangombea halali wa uchaguzi.

Hivyo amewaangiza wasimamizi wa uchaguzi wakabidhi barua hizo kwa wagombea ili waendelee na kampeni kuomba ridhaa kwa wananchi kwa nafasi walizoomba.

Chanzo: Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku.

Swali: Je, Tume ya Uchaguzi haina mamlaka kamili ya kuwadhibiti na kuwasimamia wasimamizi wa uchaguzi?
NECCCM
 
Kila kiongozi ana mamlaka yake katika utekelezaji wa majukumu Kama mkurugenzi wa Tume alishatoa rufaa akatuma kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo Sasa analaumiwaje kwa wagombea kutopata hizo barua tusisahau kuwa Mkurugenzi wa Tume anasimamia uchaguzi nchi nzima ana mambo mengi ya kufanya kufuatilia kwa kila mtu Kama amepata barua ni jambo gumu Sana manake muda hausimami kumsubiri yeye ayafanye hayo. Yeye kashafanya kwa nafasi yake Sasa hii statement pengine ametoa baada ya kusikia minong'ono Sasa anawatahadharisha walioko chini yake kwamba yeye ameshafanya yake wataumbuka wao waliofanya hujuma kwa mantiki hiyo yupo sahihi kabisa
Unasemaje kuwa yupo sahihi wakati wagombea walifuatilia rufaa zao hadi huko Dodoma akawa anawapiga chenga? Aidha kwa nini hakufuatilia kuwa wakata rufaa wanapewa barua zao hata baada ya warufaa kuendelea kulalamika Tume na mbele ya vyombo vya habari?

Je, hana mamlaka juu ya wasimamizi wa uchaguzi? Na kama ni hivyo kwa nini asieleze mapema ili warufaa wachukue hatua nyingine?
 
Unasemaje kuwa yupo sahihi wakati wagombea walifuatilia rufaa zao hadi huko Dodoma akawa anawapiga chenga? Aidha kwa nini hakufuatilia kuwa wakata rufaa wanapewa barua zao hata baada ya warufaa kuendelea kulalamika Tume na mbele ya vyombo vya habari?
Je hana mamlaka juu ya wasimamizi wa uchaguzi? Na kama ni hivyo kwa nini asieleze mapema ili warufaa wachukue hatua nyingine?
Kuna protocol za kufuata katika kila Jambo mkurugenzi wa uchaguzi asingeweza kutoka ofisini kwake hadi majimboni moja kwa moja kupeleka barua ya rufaa kwa mgombea anatumia channels zilizopo kisheria ambazo ndio hizo za kupitia kwa wasimamizi wa uchaguzi Sasa Kama msimamizi wa uchaguzi hajatoa barua atajibu yeye ndio maana nasema binafsi nimeelewa kauli mkurugenzi wa Tume kwamba shida haipo tena ofisini kwake ndio maana hao wagombea wamewekwa kwenye karatasi ya kupigia kura hiyo ni hatua ya wazi kuwa ofisi yake imetenda haki. Sasa Kama Kuna tatizo mahali atahusika kujibu ambae tatizo lipo eneo lake ndio maana amewatahadharisha
 
Hapa kunavinza linatupwa likampate mtu limnukie kondoo wakafara anaandaliwa.
 
hivi Anasali wapi tuongee na viongozi wake wa kiroho juu ya unafiki wake juu ya wanadamu. Mambo yake ni aibu tupu kisa madaraka
 
Back
Top Bottom