Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Ebu tueleze hapa, ni kivipi Lissu anataka kuiweka rehani ardhi yetu? Ni vihashiria gani ambavyo vinapelekea kusema hivyo?.Tusaidie hapa tuelewe tukawe mabalozi kwa familiya na marafiki zetu.

Vinginevyo basi na tuendelee kuwa mabalozi wa Lissu,tuzidi kumtafutia kura kwa familiya zetu na wafanyakazi wenzstu na kwa ndugu jamaa na marafiki.
zero kabisa, yani mnatetea mtu anaetaka kuweka rehani ardhi yetu? Unajidai upo deep kumbe umejaza manyoya tu kichwani. Mkiona hamuwezi kuisapoti CCM bora mkae kimya kuliko kutetea uovu.
 
Aliposema akishinda watamtangaza alimaanisha. Huyu bwana hatanii, nadhani ameona dalili za kumtangaza.

Na hayo ni mafanikio ya Rais Magufuli kuchukua likizo ya kampeni hapo Dodoma badala ya kwenda kwenye kampeni.

Wameona dalili za kumtangaza na wanapoona popularity yake wanaanza kuogopa

Jamani hofu lazima iwepo unapoona jambo linakuzidi uwezo lakini huna budi kutii sheria badala ya kulivuruga jambo
 
Sasa Lissu akienda ndo atajua Lissu nyoko. Ataenda na hii clip na atawapiga maswali kutoka kwenye hii hii clip hadi watapoteana 😂😂😂😂
Tena akahoji why wanaoenguliwa ni upinzani pekee, pili je Kama mgombea kuzulumiwa haki yake ya kutotangazwa mshindi haki yake atapaje.
 
Aliposema akishinda watamtangaza alimaanisha. Huyu bwana hatanii, nadhani ameona dalili za kumtangaza..
CCM awakutegemea kuuona nyomi ,nyomi ufanya kazi ya wizi kuwa ngumu. Yahya Jameih alimiliki Hadi tume anajipangia tu asilimia za ushindi lkn wananchi walipoamua alipigwa na tume yake Barrow akatangazwa mshindi.

Tuliwaambia CCM jijengeni kwenye umma nguvu ya ushawishi na sio dola ona Sana pumzi imekata. Tumieni dola iwalazimishe kupendwa mjaze nyomi bila wasanii na mabango Hadi chooni.

Jiwe anashindana na wakati.
 
Huo Moto wa Kanda ya ziwa si wa kitoto aise ngoja tuone kipindi cha pili Sasa,ccm wamepoteana na tume yao. Hoja za kitoto kabisa eti wataiba madini yao zero kabisa huyu kibraka ana elimu gani reasoning yake ipo down Sana.
Ilitakiwa hayo mahojiano na Lissu yasimamiwe na neutral figure siyo yeye huyo kada.
 
Kauli hizo ni mwendelezo wa maneno na matendo ya dhahiri NEC haipo huru ni kama tawi la ccm. Wanasheria kusanyeni ushahidi mnaweza kuanzisha kesi yenyo mashiko mbali ya mazingira tata mifumo yetu.
ushauri mzuri sana.
 
Tunaposema Lissu ni hatari ndio muelewe. Mkurugenzi wa uchaguzi kachanganyikiwa na kuanza kunadi sera kama kichaa.
Sasa kama kibaraka hofu yake ni dhahiri namna hii ‘bosi’ wake ana hali gani?

Hii sio aibu, ni fedheha!
Yeye atakua dhoofu bin hal!
 
Katika ujinga tume imefanya ni huu. Hawa jamaa wanajiingiza kwenye 18 za Lissu wenyewe. Badala wafikirie jinsi gani wanaiba kura siku ya uchaguzi wao wanamwita Lissu. Lissu hafanyi kampeni kwenye TV watu wengi hawamuoni, wanavyomwita na anavyopangua hoja ndio anaongeza wafuasi na waumini mtaani.

Kila siku Lissu akiongea anapunguza waumini wa ccm na kuwashawishi wampe kura tofauti na wagombea wengine. Ningekua mm nipo kitengo hicho.

Ningewambia mitandao ya SIM yote kila Lissu akiongea wekeni network E sehemu zote watu washindwe kusikiliza hotuba zake. Ila huu mchezo wa kumuita huyu jamaa tume inajiingiza matatizoni sababu hata vyama vingine vinakosea.
 
Kuna tetesi nimezisikia toka Alhamisi iliyopita kuwa mzee Meko hofu kuu imemuingia baada ya ripoti ya ndani ya CCM kuonesha hali ya CCM kisiasa inakwenda mrama kupita maelezo toka kampeni kuanza.

Inasemekana mzee Meko amekuwa mkali kupita maelezo, na ameagiza wateule wake wote waingie field kusaidia kuokoa jahazi la sivyo ndani ya wiki moja atawatumbua kama kichaa.

Hivyo tusishangae sana haya ya huyu kada wa CCM ambaye ndiye mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuja kumfanyia kampeni kwa lazima.

Mchezo wao wa kupanic tuliuelewa wazi baada ya kumuona Pole Pole anarudia kufanya Press comference ndani ya masaa 48 toka kufanya press yake, halafu Press yake ikaishia kuvurumisha matusi matupu.
 
Ilitakiwa hayo mahojiano na Lissu yasimamiwe na neutral figure siyo yeye huyo kada.
Anahofia kukosa ajira


Screenshot_20200928_000007.jpg
 
Back
Top Bottom