Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?...
Mkurugennzi kaamua kuonyesha rangi yake halisi..
 
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?...
Huyu ni kada kama wengine sema tu hatujuwi namba ya kadi yake. Amekosa hata busara za kujuwa kiti alichokikalia kinamtaka a behave namna gani??.

Lisu kuwaambia wafanyakazi kuwa ataongeza mishahara ndo kiwatisha?, Eti hataki Mgombea atakaye uza madini yetu nje, kwani sasa hivi madini yanayochimbwa Tz yanatumika humu nchini?

Kama yanauzwa nje, ni nani anaye yauza kama si Magufuli ambaye tume anayo iongoza imeshamruhusu kugombea?. Huyu jamaa ni wa kukemewa aache ujinga kwa nafasi alonayo hatakiwi kuegemea upande.

Ni dhahiri kwamba kashinikizwa kusema anachokisema na yule alompa nafasi hiyo.
 
Tume ya taifa ya uchaguzi haipaswi kwa namna yoyote ile kuwa tawi la kampeni la ccm. Huyu bwana tunamjua ni ccm damdam ila kwa nafasi aliyonayo alipaswa asiegemee upande wowote.

Anajitengenezea mazingira ya kuisapoti ccm hadharani ili hata ikishindwa aitangaze imeshinda. Tafadhali bwana Mahela, jiuzulu nafasi hii maana umejiandaa kulitumbukiza taifa kwenye machafuko.
 


Hebu tazameni hizi video, atawaambia nini watanzania?
Mkiambiwa tume ya Uchaguzi siyo huru mnabisha kitu gani watu wa Mungu?
 
Kada wa magufuli anataka Sera za magufuli ndo ziwe za upinzani!!!
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!...
Hapo ndipo tume na wanapokesea, tunachokitaka tunakijua wenyewe tuacheni tuchague wenyewe, hata tukichagua jiwe lituwakilishe kwani toka tunaichagua CCM lini ilishawahi kuniletea ugali mezani ? Tunakula kwa nguvu na jasho letu msitutishe.
 
Tume ni tawi la ccm na wanatekeleza ilani ya ccm. Na tume ni mojawapo ya mitambo ya ushindi. Ila msimu huu CCM watatoka madarakani na kufutwa.
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!

Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao
Huyu jamaa ni mpumbavu kama wapumbavu wengine! Ina maana anaipigia kampeni CCM? Sitamheshimu hata siku moja nyoko kabisa! Nani amemwambia raia wanataka ndege? Mamamake!!
 
Kwani sasa hivi madini yanachimbwa na wasukuma na kuuzwa soko la Kariakoo? Huyu jamaa amekula maharage ya wapi? Ninachojua mimi ni kwamba madini yanachimbwa na wageni na yanauzwa huko huko nje kwa wageni. Mitutusa mingine bhana!
kila mkoa una soko la madini ambapo wachimbaji hupeleka kwa ajili ya kuuza, haya masoko aliyaanzisha JPM baada ya sakata la makinikia
 
Ahaaaa ahaaaa, halafu eti tume ya uchaguzi inajiita iko huru huku kiongozi wa tume anaghani mashairi ya ccm. Magufuli ameishurutisha hiyo tume wamtangaze yeye na chama chake kwa 90%+, hivyo tume wanatuandaa kisaikolojia. Kitendo cha Lisu kusema haramiachia Mungu kinaichanganya tume maana wana matokeo tayari kabla ya kura halisi. Nimecheka sana eti hawataki mtu atakayepeleka madini yao nje kwa wazungu, kwani mpaka wanaochimba ni kina nani, na baada ya kuyachimba wanayapeleka wapi kama sio kwa wazungu? Kweli tume hii imeshapoteza uhalali
Kwakweli sikujuwa kama huyu jamaa ni wa namna hii, ni dhahiri kuwa tume haiko huru lkn kashindwa hata kufunika funika??. Hebu niambie kwa speech hiyo anawezaje kusimama na kusema tume anayo iongoza ni huru??.......btw, wapekenyuaji mtujulishe namba ya kadi ya uanachama wake, maana ni hakika kwamba kadi ya CCM anayo.
 
kusema kwamba mgombea inabidi atetee rasilimali za nchi na awe mzalendo sio kua neutral? Kwamba kwa kusema hivyo basi wanampigia kampeni mgombea wa CCM? Ukiona mtu ana react kwenye hili ujue mgombea wake sio mzalendo wala mtetea rasilimali za nchi.
Mimi nasema mtu neutral anatakiwa azungumzie kanuni na taratibu za uchaguzi
Kuhusu sera na madini. Barabara n.k sio jambo la busaara kulizungumzia
Yeye abakie kua ni refa au muamuzi
Sio mtu wa kuzungumzia formation ya timu
Itakae cheza 4 4 2 Sawa itakayo cheza 10 1
Sawa jukumu la refa ni kutoa muamuzi ya goli pernat, coener, offside etc
Lakini watanzania tunataka timu yenye kucheza 4 4 2 nadhani sio maadili
Yeye abaki kwenye kitab cha muongozo wake
Anyways yupo huru kumfanyia kampeni amtakae na sidhani Watanzania watabadili mawazo Yao kwa sera hizo zaidi ya watu kumshangaa tu
 
Wakuu, huyu Mkurugenzi wa tume Ya Uchaguzi nilimsikiliza Lakini nikasikitika alipowashawishi wananchi wamchague rais ambae anatetea maslahi Ya nchi nikashangaa Sana kuwa huyu anatumia nini kufikiri?

Haya majitu yamepora hii nchi, ulisikia wapi Mkurugenzi wa Uchaguzi anapiga kampeni? Sasa mbona kaongea hilo tu akashindwa kuongea issue ya ukatiri?

Hivi haya majitu yamesoma Lakini yameshindwa kujikumbusha kuwa makatiri wote duniani yalijificha kwenye kichaka cha neno "KUTETEA NCHI " na Yote yalikuja kuuuwawa makatiri Ya neno hilo, wote walijikita Kwa neno la kutetea nchi, majitu yanauwa watu, yanatesa watu, yanapora watu Mali zao, yanaendesha vikosi vya kigaid ndani Ya nchi na kuviita wasiojulikana, yanapambikizia watu makes, hili lenye Meno na mdomo Kama ngiri linakuja kupiga kampeni Wakati ndilo lisimamizi, Kama haya mahutu yameingiaje Tanzania? Haya Siku moja inabid tujitoe muhanga nayo ili kuokoa kizazi kijacho
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!...

Huyu DR. anatumika vibaya bila yeye kujijua. Yeye akae ofisini, mambo ya kampeni hayawezi. Sasa anapotumia ofisi yake kuwaponda baadhi ya wagombea na kusema watchuka madini na kupeleka nje, kayatoa wapi hayo kama si propanganda alizojazwa na boss wake?
 
Dhuu huyo kaonyesha dhahiri rangi ya ngozi yake. Nilikuwa sina mpango wa kupiga kura sasa nitampigia kura mtu wangu rasmi
 
Huyu jamaa ni kunguni kweli, yeye ni msimamizi, aache watu wapambane, yaani anajipambanua kabisa kwamba yeye ni nani na ni kitu gani, ingekuwa habri nyingine
 
Huyo alitakiwa agombee Jimbo la Serengeti huko . Amekengeuka hajui mipaka ya kazi yake.
 
Back
Top Bottom