Wanabodi,
Niko ndani ya ukumbi wa JNICC kwenye Mkutano huu muhimu
Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa tarehe 3 na 4 Januari, 2024 View attachment 2855370
Mkuu
Venus Star , asante sana kwa taarifa, hii sio ya kukosa!,
Ila to be honest, nilikuwa nina wasiwasi na baadhi promo za Mkutano huu, kama baadhi ya washiriki hawa
View attachment 2855372View attachment 2855373View attachment 2855374
View attachment 2855375 japo sijabaatika kumuona yeyote kati ya hao, ila Chadema wamewakilishwa na Makamo Mwenyekiti wa Chadema na na NKM wa Chadema, Kamanda Salum Mwalimu, ambaye yuko in full regalia ya combat.
Mkutano umeanza, fuatilia live Mubashara kupitia Wasafi
View: https://www.youtube.com/live/WMNZqOQv-jo?si=gbOqXz5I22MQuyka
Kwa Tanzania Bara, ukisema upinzani unamaanisha Chadema!, huu ni mkutano wa 3 wa Baraza la Vyama vya Siasa, mikutano miwili iliyotangulia, Chadema walisusa. Mkutano wa kwanza pale Dodoma, mimi niliwaomba wasisuse
Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.
Chadema waligomea wito wangu ila hapa walikuwa na justified reason ya kususa, Mwenyekiti wao alikuwa korokoroni akikabiliwa na kesi ya ugaidi.
Kesi ya Mbowe ikafutwa, Mbowe akaachiwa, CCM wakafanya mazungumzo ya maridhiano na Chadema, wakafikia makubaliano ya kugawana nusu mkate. Lakini mkutano wa pili wa Baraza la Vyama vya Siasa, bado Chadema walisusa!.
Hivyo mkutano huu wa 3 ulipoitishwa, nikaandika tena kuwasihi Chadema wasisuse
Baada ya maridhiano kuna haja kuendele kususa na kuzira? Njooni mezani, tukae pamoja, tuwe wamoja, twende pamoja!
This time ombi hili limezaa matunda, Chadema wameshiriki kikamilifu, hivyo ni faraja kubwa kwa wapenda demokrasia.
Karibuni.
Paskali