Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Doh! Nimecheka sana aisee.
Bavicha bhana..Nakuambia tena hawaibi kura za uraisi. 2015 ,wapinzani kwa ujumla wao walipata asilimia nyingi kuliko Magufuli. Wapinzani wakiweka pembeni tofauti zao wakaweka mgombea mmoja vs Magufuli. I tell you Magu anashindwa saa nne asubuhi.
Si inasemekana hataki tena?Breaking News.
Mgombea Urais wa Tz kupitia Chama cha Mapinduzi 2020 Dk. John Joseph Magufuli amemchagua Mama Samia Suluhu Hasani kuwa mgombea mwenza wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. View attachment 1503737View attachment 1503738
mamvi kazuga yuko hoi kwa usingiziHata mm NISINGEKUWA RAIS bila mh.Kikwete......
Aliwatwanga MPAKA marafiki zake😂😂😂😂😂
Mashallah rais wetu JPM mungu akupe uhai mrefu aaaamin
Hii karatasi ilikuwa na mtego wa maksudi kabisa, hata ukitia [emoji3514] kwenye kivuli maana yake umesema HAPANA kwa kivuli.... umekikataa kivuli hivyo kura inahesabika ya Nyerere.
Kutawala wajinga ni raha sana.
Kawadanganya nini tena wafuasi wake.Kigogo sijui huwa anafeli wapi
Hakuna mgombea mbadala na wanaohesabu kura ni waowao kwahiyo angeweza kupata hata 123% sio ajabu.Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Jumamosi, Julai 11, 2020 jijini Dodoma, Wajumbe 1,846 wanatarajiwa kushiriki. Mkutano huo unongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
AJENDA:
1. Kufungua Mkutano
2. Marekebisho ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977, Toleo la 2017
3. Taarifa za Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 za SMZ, SMT na CCM
4. Uteuzi wa Mgombea wa CCM wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
5. Kufunga Mkutano.
UPDATES;
Mkutano Mkuu wa CCM unafanyika leo tarehe 11 Julai 2020 ukiwa na lengo kuu la kumpitisha mgombea wa Urais wa JMT.
Mkutano umehudhuriwa na wanachama 1,822 huku wanachama waliokosekana wakiwa 23 sawa na 1% hivyo uko sahihi kikatiba na ajenda zinaweza kujadiliwa.
Katika hotuba yake, Rais Magufuli kama mwenyekiti wa mkutano huo, amewashukuru viongozi wa upinzani waliohudhuria katika mkutano huo
Amemshukuru Lyatonga Mrema, mwenyekiti wa TLP kwa kauli yake ya kusema TLP haina mgombea bali itamuunga mkono mgombea wa CCM
Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF amesema chama chao katika uchaguzi wa 2020 kinakuja na agenda ya “Furaha kwa Watanzania inawezekana”
Ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika leo Juni 11, 2020 Jijini Dodoma alipopewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya vyama vya upinzani vilivyoalikwa
Pia Professa Lipumba amewaomba CCM kuwa na siasa za ustaarabu kitapoanza kipindi cha kampeni akisisitiza kupambana kwa hoja
Mzee Kinana -
Amewaomba Wajumbe mkutano mkuu wampe mgombea kura zote bila kuharibika bila hapana ili apate nguvu kuliongoza taifa letu.
Amewasihi Wanaccm kufanya kazi kwa bidii kwa kujitolea kutafuta kura za Rais, Wabunge na madiwani. Hakuna uchaguzi rahisi.
Kuna Watia nia na ubunge wengi sana, kuna jimbo la Rorya watia nia wako 60, nawaomba hatimaye watamteua mgombea mmoja wa CCM hivyo wasigawane kura.
Mzee Mwinyi
Nawaomba wenzangu tumekutana hapa na wanatanzania nzima pamoja na wapinzani. Sote tumeshuhudia kuwa mgombea Rais wetu tuliye naye ameshika madaraka kasoro miaka mitatu kama mambo mengi, ya ajabu kama kununua ndege 11. Sijawahi kuona nchi inayosemwa haina pesa inanunua ndege 11 kwa pesa za ndani. Hakika Rais Magufuli amefanya mambo ya ajabu katika sekta zote ikiwemo Umeme na SGR.
Tumekaa miaka mingi na uwezekano wa kupata umeme lakini Rais wetu kalishugulikia suala la umeme kwa kujenga Stiegler's Gorge na karibu tunakuwa mabepari wa umeme.
Nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba lazima tuienzi, , tusiingilie lakini tunaweza kuiahirisha kwa muda mfupi ili kumpa Rais wetu kipindi kingine kimoja cha asante. Hichi ni asante na kisha tuendelee vile vile mpaka dunia iishe. Hiki ni maalum kwasababu ana mengi nchi itayakosa.
Rais Magufuli akimjibu Mwinyi kuhusu kuongezewa kipindi kingine
Mbona wewe (Mzee Mwinyi) hukuongeza muda baada ya kumaliza? Au mzee Mkapa hakuongeza? au Mzee Kikwete hakuongeza? Ila nimekuelewa Mzee Mwinyi wewe ni mtani wangu.
Agenda: Uteuzi wa Mgombea Urais kupitia CCM
Rais Magufuli amejivua Uenyekiti ili aweze kupigiwa kura, Uenyekiti umekaimishwa kwa Mzee Sheini.
Matokeo
Msimamizi wa Uchaguzi, Spika Ndugai anasoma...
Wajumbe walohudhuria ni 1822
Kura zilizopigwa ni 1822
Hakuna kura iliyoharibika kura halali ni 1822. Kura za ndiyo ni kura 1822 sawa na asilimia 100.
Hussein Mwinyi
Nimefanya kazi na Marais watatu ambao ni Mkapa, Kikwete na Magufuli. Ninawashukuru wote kwa kunielekeza lakini kuna Rais ambaye Mstaafu ambaye sijafanya kazi nae ila ndio Mzazi wangu Mzee Mwinyi, amenilea, kama nina tabia njema basi ni malezi yake, namshukuru Mama yangu Mama Sitti tuko nae hapa, mchakato wa Urais umefanya nipungue uzito ila Mama yangu amepungua zaidi.
Namshukuru Mzee Mkapa nikiwa Kijana wa miaka 33 (Mbunge wa Mkuranga) aliniteua kuwa Naibu Waziri Afya,Mzee Mkapa ulinifungulia njia, namshukuru Mstaafu Kikwete katika utawala wake wa miaka 10 yote nilikuwa Waziri, namshukuru JPM pia kwa kuniamini na kunipa Uwaziri.
Katika miaka mitano ya kufanya kazi na wewe, nimejifunza mengi kwako Rais Magufuli . Wapo waliosema mimi ni mpole lakini nimejifunza kuna mambo yanataka uwe mkali, mfano rushwa, uzembe na ubadhirifu, nikichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar nitakuja na style ya Rais Magufuli katika maeneo hayo.
=> Rais Magufuli: “Mambo yaliyofanyika ni mengi, kila mmoja ni shahidi, hata Viongozi wa Vyama vya upinzani wanafahamu mazuri yaliyofanyika hata Nchi jirani wanafahamu, Ndege 11 kununuliwa kwa mpigo tena kwa cash, Elimu bure,Barabara,vituo vya Afya nyinyi wote ni mashahidi”
=> Rais Magufuli: “Tumeipeleka Nchi kwenye uchumi wa kati, tumepambana vizuri na corona na mengine mengi, tumeitengeneza Tanzania, ni mafanikio yetu wote hata ambao hawako CCM na ndio maana Mzeee Mrema mapema kabisa akasema yeye hana mgombea Urais, mgombea wake CCM maendeleo hayana chama”
=> Rais Magufuli: “Nimefurahi kuwaona Marais Wastaafu, nimefurahi kumuona Mama Anna Abdallah huyu Mama alinifundisha Kazi lakini pia alimfundisha kazi Mwinyi akiwa Naibu Waziri wa Afya, nimefurahi kumuona Mzee Kinana, Lowassa, Mzee Sumaye, Maspika Wastaafu na wote”
=> Rais Magufuli: “Nimefurahi kumuona Mzee Mwinyi Mzee wa ruhusa, nimefurahi kumuona Mzee Mkapa Mzee wa uwazi ingawa sijajua ni uwazi upi?, nimefurahi kumuona Mzee Kikwete naona mvi zimeanza uzee unamuwinda, hii ndio Tanzania, nimefurahi kumuona Dr.Bashiru, Mzee Mangula n.k”
=> Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Mhe. Augustino Mrema: “May 04, 2019 sisi TLP tulikaa tukajadili nani atuongoze, H/Kuu TLP ikasema hatuna mbadala wa Magufuli tukasema Magufuli anatosha, tukakutana tena May 08,2020 kura zote zikamuangukia Magufuli”
=> Mrema: “TLP tumesema wewe Magufuli unatosha, tutafanya kampeni Nchi nzima kuhahakisha unachaguliwa tena, ombi langu kwenu CCM tujipange kuhakikisha kwenye Kata na Majimbo yote kuna mgombea wa TLP na CCM, tusing’ang’anie jimbo moja Watu wa CCM 30 ni matumizi mabaya ya rasilimali Watu”
=> Mrema: “Baada ya May 08,2020 Halmashauri Kuu TLP kusema Magufuli anatosha kuwa mgombea wetu, May 09,2020 tukamuita Polepole aje, tukamualika na Msajili aje ashuhudie kuwa kikao cha TLP hakikuwa cha Magumashi na hapo tukapiga kura kisha wote wakasema tena wanamtaka rais Magufuli”
RAIS MAGUFULI APITISHWA KUWA MGOMBEA WA CCM KWA 100% YA KURA ZA WAJUMBE
Rais John Pombe Magufuli ameteuliwa na CCM kuwa mgombea wa Urais kwa mwaka wa uchaguzi 2020
Kwa kura 1822 zilizopigwa na wajumbe wa kamati kuu, Rais Magufuli amepata kura 1822 ya kura za ndio
Awali katibu mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally alisema, ilibidi wawe na wagombea watatu lakini hakukuwa na mgombea aliyejitokeza kuchukua fomu ya kugombea urais
Hali hiyo ilimfanya Rais Magufuli awe mtu pekee aliyechukua fomu ya kugombea Urais kupitia CCM
Magufuli amefanikiwa kukiweka CCM kwapani kama sio makalioni.Mwaka huu Chadema wanachungulia na kuondoka bila comment kama 2015
Itakuwa ngumu sana.Akimaliza arudishe na majaliwa kwenye nafasi yake wembe uendeleze makali
Ni kama corona tu hakuna kilichafanyika cha kidemokrasia ni uhuni wa kisiasa kwani watu hawana uchaguzi ni lazima.Habari wakuu,
Ninekuja mtembelea jamaa yangu hapa nimemkuta anafuatilia mkutano wa CCM na zoezi la upigaji kura liko linafanyika huko. Kilichonichekesha katika zoezi hili ni:
1. Hakuna usiri
2. Wajumbe wanapigiana kura (nimeona mmoja anapiga kwa niaba ya mwenzake)
3. Maandalizi hayakuwa vizuri (kuna uchache wa peni ) naona wana azimana tu, hawajui hata walienda fanya nini.
4. Naona watu wanatumia kujitangaza, baada ya kupiga kura wanajionesha ili teuzi zipite kwao.
5. Ukusanyaji wa kura ni vichekesho
kifupi, sijaona cha maana katika hili zoezi; liko kiswahili swahili sana.
Mafiga matatuBreaking News.
Mgombea Urais wa Tz kupitia Chama cha Mapinduzi 2020 Dk. John Joseph Magufuli amemchagua Mama Samia Suluhu Hasani kuwa mgombea mwenza wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. View attachment 1503737View attachment 1503738
Amenyweshwa sumu halafu akazibwa mdomo!. Kweli nchi hii mbaya sana. Ni kama akina Mwakyembe walivyonyweshwa sumu halafu wakapewa uwaziri na kuzibwa midomo. Ahaaahaa!Huyo mzee Mpumbavu tu
Jumbe brown towashi wa Kardinali Pengo , HAHAHAHHHAHHHHHHHaaa umenaswa pabaya