Mkutano wa Chadema na Rais Samia: Mtu hakatai WITO hukataa anachoitiwa

Mkutano wa Chadema na Rais Samia: Mtu hakatai WITO hukataa anachoitiwa

Kazi ya mdomo ni kula na kuongea. Usipokuwa na kitu cha kula basi utaongea

1653114469213.png
 
Hivi unaenda kuongea nao nini juu ya ule uvunjifu wa sheria wanaoufanya makusudi?

Mikutano ya siasa ni haki ya kisheria, wameizuia makisudi kwa mabavu, ni kitu gani kinawazuia hao jamaa kuruhusu tu mikutano ya siasa?

Halafu kama issue ni mazungumzo, yabaki kwenye mambo ya msingi kama kutibu majeraha yaliyosababishwa na ule uchafuzi mkuu wa 2020 ambao uhuni ulifanyika.

Mimi ningewaelewa endapo Samia angeruhusu mikutano ya siasa, coz hilo zuio liliwekwa na mwendazake, lakini ajabu na Samia analiendeleza, huyu nae ni msumbufu tu anajua vizuri anachofanya ni uhuni.

Kwangu kama maridhiano yangebaki kwenye ule uchafuzi wa 2020 uliosababishwa na mwendazake ambaye leo hayupo, hapa nisingekuwa na lalamiko.

Lakini sio kukaa na mtu unambembeleza aruhusu kuondoa zuio lililokiuka sheria, huku ni kujidharau, tuondoe hii mentality ya kinyonge, susia uchaguzi, waende wenyewe na vibaraka wao.

Mbona Chadema hawakupeleka wabunge bungeni CCM wamehangaika kutengeneza wasaliti 19 wakawapeleka kule, naamini kama wangekuwa hawatishiki wasingetengeneza wale wahujumu uchumi 19.
 
Wanaochochea cdm wakatae ni wale waliokuwa watesi wao jana. Kinachowauma ni kuona Samia anawaprove wrong kwamba siasa ni ya wote na hakuna mwenye hati miliki ya uongozi. Wakafie mbali huko aliko mwenzao.
Prove wrong for what? kuendelea kususia mikutano ya siasa?
 
Watu wakae wakijua Mbowe hajawahi muomba mh Samia kukutana naye ila kutokana na utu wa mh Rais wa kutopenda kuongoza taifa lenye manung' uniko na mgawanyiko ameamua kuzungumza na kaka yake ambaye ni mtanzania mwenzake je kuna ubaya gani hapo?Watu wajue tz ni kubwa na muhimu kuliko mh Rais na mh Mbowe
 
Mbowe na Heche wameitwa wewe unapata Nini?

Miaka inaenda, kina Joyce Mukya wanacho Cha kurithi wewe Ndugu zako watarithi UNYUMBU.

Wewe Ni msukule wa wanasiasa kina Mbowe na watoto wako watakuwa misukule wa watoto wa kina Mbowe.

Hakuna Mambo ya bahati mbaya dunia hii.
Sasa matusi ya Nini? Kwanini umenitukana? Si ungelitoa jibubyakaisha na si matusi! Sabato njema
 
Wale mnaopinga Mbowe na Chadema kukutana na Rais ingien misituni mpambane na Serikali tuone mtapata matokeo gani.
Imesema kweli, kama wana gutts, waingie msituni. Mtu anasema njoontuzunhumze, mnasema hatuji, Basi nenda infantry tuone matokeo!
Ni wazo jema kujadiliana
 
Huyo Mbowe muuni tu yeye na Ccm na sukuma Gang wote wasanii

Badala muwatete Wananchi nyie mnaangalia interest zenu tu

So mavyama yote hapa Tz. Ni kwa Ajili ya wizi tu.
Upumbavu huo hata mie siwezi na mrema pia alishindwa, yaani atetee mijitu isiyojitambua akiwekwa sello hata kusogea gerezani kwenda kumsalimia hamthubutu, mbowe chukua pipa kamiminiwe na wewe asali ulambe, umekaa gerezani miez9 keyboards woriaz tuliashia kuandika twira hashtag #mbowesiogaidi# #freembowe# hatukuthubutu kuandamana hata maji ya kunywa hatukuleta.
 
Mmmhh. Ngoja ninywe mtori, nyama nitazikuta chini. Sina imani na hayo mazungumzo, na mifano ninayo.
Hebu tiririka kidogo ndugu Tindo. Tindo ni kifaa kinachotwanga sehehmu ngumu.

Naomba umwage mifano miwili mitatu kwa faida ya wengi.
 
Huyo Mbowe muuni tu yeye na Ccm na sukuma Gang wote wasanii

Badala muwatete Wananchi nyie mnaangalia interest zenu tu

So mavyama yote hapa Tz. Ni kwa Ajili ya wizi tu.
Alipovunjiwa biashara zake wewe si ulikiwa unamsimanga na kuchekelea?? sasa unataka skusaidie nini kwani yeye ni Rais?
 
Wanaochochea cdm wakatae ni wale waliokuwa watesi wao jana. Kinachowauma ni kuona Samia anawaprove wrong kwamba siasa ni ya wote na hakuna mwenye hati miliki ya uongozi. Wakafie mbali huko aliko mwenzao.
Ndio hao hao wengi ni yale maccm fisi.
 
Kuna watu wanasema hakuna sababu ya Chadema kukutana na Samia kwa mwenedo wa tunayoyaona including issue ya Halima et al. To me, kwa mazingira ya leo baada ya Mwendazake, ambaye alikuwa Jiwe "katili" kama ametokea mtu akasema njoo tutungumze, si busara kukataa wito. UTAKATAA UNACHOITIWA. Busara za kawaida zinaniongoza hivyo!
Hongera Mbowe, Hongera Chadema kwa kuitikia wito maana pressure ilikuwa kubwa eti msiende huko.
Hopefully you did not compromise your position on all political issues you have been demanding for decades!

FINALLY: Tunaomba mrejesho, TO BUILD TRUST AMONG TANZANIANS AS THIS WAS AND IS STILL A CONTENTIOUS ISSUE!
Mbowe na.Prof Lipumba ni kitu kimoja
 
Ndio hao hao wengi ni yale maccm fisi.
Mimi naunga mkono kila jitihada inayopelekea kuleta maelewano katika uwanja wa siasa. Itakuwa kosa kubwa Sana kwa CDM kutokutumia fursa ya kuleta maridhiana ya kitaifa kuhusu jinsi ya kuendesha siasa nchini. CCM ni chama sawa kabisa na CDM. Hakipaswi kunyimwa haki za kuendesha siasa kwa mujibu wa Katiba iliyopo na Sheria zilizopo.

Hongera Sana Mbowe na Uongozi wa juu wa Chadema kwa kuitikia mwito na kukutana na CCM.

Kama kuna nia njema, muda utatuonesha. Kama ni figisu figusi pia muda utatoa jibu.
 
Kesho tu watasusia kikao cha Msajili au NEC na mtaibuka tena kuwapongeza.

CDM iko consistent kwenye kitu kimoja tu, Kufukuza wanaotishia uenyekiti wa Mbowe.
 
Back
Top Bottom