Elections 2010 Mkutano Wa Hadhara Wa Wana-JF [Online]

Health Insurance ndio priority kwangu.
Maisha ya watanzania ni magumu. Hela za kulipia hospitali kila tunapougua hatuna. Serikali iboreshe sector ya afya na kuanzisha bima ya afya. Hata kama itaendelea kutoa huduma duni, lakini tuwe na uhakika wa kutibiwa. Hichi ni kitu cha msingi sana kama serikali inania ya dhati kuwakomboa wananchi wake.

Kuongeza wigo wa mapato na kudhibiti matumizi.
Nimefurahi kuanzishwa kwa zile cash register ambazo wauzaji hawawezi kukwepa kodi. Ubunifu wa aina hiyo ndo unahitajika continuously pale TRA. sio kila siku kuongeza kodi kwenye soda, bia na sigara.

Tatizo la serikali ni kwenye matumizi. Vitu vinavyofanyika serikalini havina value for money.
Kama mimi ndo ningekuwa Rais; ningeongeza mishahara ya wafanyakazi wote serikali
kima cha chini 1mil, watakaoa kuwa kwenye managerial levels, kima cha chini 2mil depending na sector.


Kwanini niongeze mishahara kiasi hicho?
  • Kupanua wigo wa kodi
  • Kuyaongezea uwezo mashirika kama NSSF, PSPF, PPF yaweze kufanya kazi za maendeleo zaidi kwasababu yana usimamizi mzuri. Hii itatokana na michango ya wanachama. Tunajua ni jinsi haya mashirika yanavyotumika kuleta maendeleo kila sehemu ya dunia.
  • Kuboresha maisha watanzania
  • Kupunguza uombaji wa rushwa kwa wafanyakazi wa serikalini
  • Ku-attract talented individuals wajitokeze kuifanyia kazi nchi yao
Huu mshahara utakuja na machungu yake
  • Kufuta allowances zote za vikao, ili watu wakae ofisini kufanya kazi
  • Kununua magari yasiyozidi CC 2500 kwa watumishi wote wa serikali wanapohitaji kuwa na magari ya serikali
  • Kufuta marupurupu ya safari za nje - ambapo mfanyakazi yeyote wa serikalini mpaka kufikia level flani, akisafiri nje ya nchi, tulipa gharama zake based on actual cost. Akiwa anafanya retirement aambatinishe na vithibitsho ya fedha aliyotumia inayobaki anarudisha hazina. Hiyo itapunguza sana demand ya USD. Safari za ndani zitaendelea kuwa na allowances kwasababu zinatija
Elimu ya bure mpaka kidato cha nne

Tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika sector ya elimu. Walimu ndo wanatakiwa wawe watu wanaolipwa vizuri kuliko wafanyakazi wa maofisini. Ila hayo malipo mazuri yaanze baada ya mabadiliko yafuatayo
  • Walimu wachaguliwe kutoka wanafunzi waliofauru vizuri na sio failures: Huwezi kumchukua mwanafunzi aliye fail F4 akapata course ya miezi 3 aje kufundisha ukitegemea utapata taifa lenye watu wasomi na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Tunaiua nchi yetu bila wenyewe kujua
  • Upimaji wa ubora waalimu uwe unafanyika, na ndio kiwe kigezo cha malipo. Sio shule kila siku inakuwa imejaza Div 4 halafu mwalimua wa hiyo shule awe analipwa sawa na anafaulisha vizuri.
Ubora wa elimu ni kitu tunachokiangalia juu juu sana, ila miaka kumi mbele hili litakuwa tatizo kubwa sana kwa taifa letu.

Kwa ufupi mambo makuu matatu ambayo ntapenda Kiongozi atakae ingia madarakani ayasimamie ni
Healthy Insurance
Ukusanyaji na usimamizi madhubuti wa matumizi ya serikali
ELimu ya bure ambayo ni bora kwa watanzania wote kuanzia shule za awali mpaka kidato cha 4
 
Aisee . . . Nimerudi sasa . . . Wakati tunapitia hoja zilizotolewa naomba wafuatao waje jukwaani kutoa maoni yao:
Msanii
Jile79
Njaa
Dark City
Eeka Mangi
Butterfly
jethro
Mburahati
safina
Xuma
Ambassador
Mr. Zero
Chesty
ThinkPad
Mujuni2
mlachake
Ahsante Mwenyekiti kwa rukhsa yako.
Ninapendekeza kwa serikali mpya kwamba, viongozi wa serikali hasa mawaziri watakapotoa taarifa zisizo za kweli iwe BUNGENI au popote pale wawajibishwe kwa manufaa ya UMMA.
Pili, ieleweke kwamba waziri au mwanasiasa yeyote anayeingia kutumikia umma kwa cheo chochote avuliwe madaraka yake kwenye Chama (chochote kile) ili kuwepo na uwajibikaji na kujituma kwa uadilifu.
Tatu, serikali mpya ifilisi mali za wooote waliokwiba mali za umma.
Nne, serikali iboreshe elimu kwa kuwaongezea mshahara walimu na wanaohitimu na kupata daraja la juu ndio wapelekwe ama waruhusiwe kujiunga na vyuo vya ualimu.
Tano. Maabara za kisayansi ziimarishwe kuchechemiza wabunifu na madediketa wa sayansi kuzitumia kwa manufaa ya taifa
 
Mwenyekiti.
ninatoka nje kidogo kunusa ugoro maana zogo la humu ndani, hatusikilizani.
ntarudi punde
 


Nyunyu karibu sana. Toka jana nilituma watu wakutafute nikaambiwa umekwenda kule nanihii . . . kunanihiii . . . shughuli muhimu.

Siku nyingine ukisikia kikao muhimu kama hiki jitahidi kuwahi. Na siku hizi kuna Boda Boda so, kuwahi siyo issue ya foleni tena.

Turudi kwenye hoja sasa:

Hili na katiba liko sawa na limekaa vema. Tusaidiane kumtafuta dr. Mvungi atuletee draft tuanze kuipitia hapa.

Hili na Elimu nadhani ni Muhimu ila mpaka sasa hatujaliweka sawa. Kuna moja alisemaa elimu ya msingi iwe hadi kidato cha nne. Je baadaa yaa hapo itakuwa imemwandaa kijana wa Kitanzania kukabiliana na maisha?

wale waliobahatika kuhudhuria Silivan Summit mlimsikia Rais wa Mozambique akiongea kuwa yeye Mpango Mzima wa Elimu ni kujenga Vocational training Centres mapka level ya kata. ameshafanya hivyo kila wilaya sasa. Na akasema vijana wakimaliza wanaingia moja kwa moja katika soko la ajira ya kazi za mikono na uzalishaji.

Tuna shida kwani haapa vijiweni down town nawaona hadi university Graduates na wengine na Masters wakitafuta ajira. Wa diploma na advanced ndo usimseme, tayari nina CV 10 wakiomba niwatafutie ajira nami wala sijawapatia bado kwani hazipo.

Hebu tuelewane katika hili, tunataka nini hasa katika Elimu? Let us be brief and to the point.
 
Nyunyu, kuna suala la Kilimo nadhani umelielezea vema sana. lakini bado linataka ufafanuzi.

Hawa 80% wako vijijini. Na 50% wana mapato chini ya $ 1.00 kwa siku. wana watoto wanawasomesha, wanahitaji matibabu, malazi, nguo, chakula nk? Sasa serikali iaanzie wapi?

Iwape pesa au ruzuku? Iwape mashamba walime?

Iwaanzishie vijiji vya Ujasiliamali (siyo Ujamaa) vilivyojikita katika kilimo?

Au wafanye nini hasa?
 

Aisee Mangi, umenichekesha sana. Unakuja town na Bajaji? Daladala haifiki kwenu au Bodaboda hakuna? Ndo maana umechelewa.

Sasa ukikumbuka unachotaka kusema uje hapa jukwaani.

Halafu lugha ya kejeli haturuhusu. Hivyo vibabaji kubeba mama wajawazito ndiyo nini sasa?
 

Asante Kijana, ukishapeleka uji urudi.

Hoja yako imekuwa na nguvu ya kuleta tetemeko. Yaani kwa maana nyingine hoja yako ni timilifu katika suala la Elimu. Nadhani katibu liweke vema hasa kuzingatia ni vipi Elimu itasaidia kutoa ajira kwa vijana wanapomaliza masomo.
 


Swadata! Umenena vema, nadhani haya yote tutayaingiza katika maazimio yetu.
 
1. Elimu
2. Afya
3. Miundo mbinu
Nawasilisha


Aisee baba yangu, unaweza ukayatolea ufafanuzi wa kina ili tutakapoipa serikali inayoingia madarakani iweze kuyafanyia kazi kwa ufanisi?

Tunasubiri hoja zako za ziada!
 

Kipepeo tuko pamoja na hili la katiba limekaa vema.

Bila ya shaka tutafanya majumuisho katika kutoa maazimio ya huu mkutano.

Ukiwa na hoja ya zaida haasa katika suala la kuondoa umasikini karibu sana.
 
Kipepeo tuko pamoja na hili la katiba limekaa vema.

Bila ya shaka tutafanya majumuisho katika kutoa maazimio ya huu mkutano.

Ukiwa na hoja ya zaida haasa katika suala la kuondoa umasikini karibu sana.
Mwenyekiti hebu tuwekee pannel yako ya wanamajumuisho maana unaposema kutakuwa na mjumuisho hapo unaniacha njia panda kwani sijajua nani ni nani ktk mjadala huu
 

Msanii karibu sana. Toka jana nilituma watu wakutafute hawakukuona. Vipi ulikuwa wapi na huu mkutano unajua umuhimu wake? Au uko kwenye kampeni?

Hoja yako ina nguvu sana. Kuna walioshauri juu ya "Uadilifu, Weledi na Utawala bora" Pia kuna wazo kuwa iundwe mahakama ya "wahujumu Uchumi na mafisadi" na atakayepatikana na makosa, anyongwe hadhaarani hadi afe. Hili tumeliundia kamati inayoongozwa na WoS.

Pia tumekubaliana kuwa Mawaziri ziwe ni kazi za ajira. Na kuna waliosema nafasi za Ubunge ziwe hazina mshahara bali posho tu.
 

Bajaji ni ambulance za kisasa zaidi, Comfortable na zinafika kwa urahisi zaidi kijijini kuliko mjini. Zimetengenezwa kwa uimara zaidi. Na kubwa zaidi RAISI Wa Tanzania wa awamu ya 10 atakuwa mama yake alipelekwa dispensary pale kijijini na BAJAJI maana lazima awe na akili za ziada!
 
Tuvunje muungano..........wazanzibar warudi kwao tuendelee na mambo yetu kwani tunapoteza muda mwingi kujadili kitu hiki

Jile tumekupata . . . Hii itaingia katika Mjadala wa Muundo wa Muungano wetu na hatimaye kura za maoni.

Vipi kuhusu, masuala ya uchumi na kodi?
 

Msanii safi sana . . . huwezi kupata soft copy uzibandike hapa? hatufanyi mchezo na agenda hizi. Tukimaliza tunachapisha na kukabidhi kwa serikali ijayo.

Naomba kuwakilisha.
 


Chaiman, ni kwlei nin can ya beer (LOL) maana siye kwetu ni kinywaji kama maji ,,,,,

Hili la muungani linanikera manake kila siku linaibuka kwa sura tofauti

nina uhakika tukiitisha referendum sasa hivi na watu wakipewa civic education, mwenyekiti watu watasema bora kila mtu ajue mji wake!

baada ya hayo, naomba kuwaaamkua umati uliofurika hapa jangwani!
 

Haaa haaa, umenifurahisha sana na dhana ya Elimu ya Kuchangamana. Nadhani hii ndiyo Mwalimu Nyerere aliitumia kuua Ukabila na Udini. Sasa sina uhakika huu mfumo wa sasa hivi kama unaangalia hili. Ukiongeza na hao waalimu unaowaita voda fasta basi ndo hivyo tena.

Labda nikuulize swali, tunahitaji Elimu ya namna gani hasa?
 

Kama walivyosema wadau wengine, elimu ni kipaumbele cha vipaumbele vyote. Hata hivyo ni ngumu sana kuja na recipe ambayo ni muafaka sasa hivi. Niliwahi kusema huko nyuma kwamba ili hii nchi iende, inabidi kila kitu kipigwe chini na kuanza upya (to overhaul the main system and subsystems). Kwa upande wa main system, ndo hapo wadau wanaweka mkazo kwenye kuandika katiba mpya (nasisitiza tena na tena, kuandika katiba mpya). Kwenye sub-systems (sectors) kama elimu, ni muhimu kukaa chini bila kukurupuka na kuandaa education master plan (au road map) ambayo itakubaliwa na wadau mbali mbali. Kwa sasa ni vigumu kueleza ni mfumo gani wa elimu unafaa zaidi ingawa baadhi ya maoni ni mazuri sana.

Nawasilisha,.....DC
 

Du! Kabengwe umenikuna baba'ke! Kula da deki. Mpango Mzima umekaa vizuri.

Nilikuwa nasoma hadi nacheka.

Hawa Waserikalini sijui kama wanasoma hapa . . . Inshallah ngoja tuweke kwenye majumuisho yetu.

Bravo sana! nakufagilia mkuu!
 

Msanii, kwanza karibu tena. Mkuu umetukuna sana kwa pointi zako. Zinatuweka vizuri kuongezea zilizopita hasa suala zima la katiba.

Hili la tano Msanii, unaweza kulitolea ufafanuzi wa kina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…