Uchaguzi 2020 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM: Dkt. Hussein Ally Mwinyi achaguliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM. Membe afukuzwa rasmi

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM: Dkt. Hussein Ally Mwinyi achaguliwa Kugombea Urais Zanzibar kupitia CCM. Membe afukuzwa rasmi

Mbarawa kanyofolewa ili Mwinyi apite. Ya Membe vs Lowassa then Magufuli yanaweza kutokea
 
Naaaaah, Nahodha lazima achukue, nilimpa Makame ila kakosa basi tena.. Sasa Nahodha is better kuliko Mwinyi by far.
Mimi toka mwanzo nampa Dr Khalid Salum Mohammed na ndiye YEYE

Mwinyi Makamu wake

Tusubiri tuone ,nime bett hivi
 


Leo Halmashauri Kuu ya CCM inapokea mapendekezo ya Kamati Kuu kuhusiana na waliopendekezwa kugombea Urais wa JMT na ule wa Zanzibar.

Kadhalika itapokelewa ripoti ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 5 iliyopita na kupitishwa ilani ya miaka 5 ijayo.
Mkutano uko mubashara TBC na Channel ten, ITV, Star tv na Upendo tv

Up dates:
Wajumbe wameshaketi ukumbini wakimsubiri mwenyekiti ambaye ataingia wakati wowote kuanzia sasa. Rais Magufuli ameingia ukumbini na wajumbe wote wanamshangilia kwa shangwe na vigelegele.

Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amefungua kikao hiki na kutoa rai kuwa ianzwe ajeda kubwa ya Uchaguzi wa Mgombea Urais Zanzibar

Rais Magufuli pamoja na Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuanza na ajenda ya Wagombea Urais Zanzibar. Mpaka sasa kuna jumla ya majina matano ya Ugombea Urais Zanzibar.

Dr Bashiru amewataka Wagombea watano waliopitishwa na kamati maalumu ya halmashauri kuu kuja mbele ili kusalimia alafu baada ya mchakato huo Mwenyekiti atataja majina matatu yaliyopita.

Rais Magufuli (Mwenyekiti wa CCM) ametoa idhini ya majina matatu yaliyopendekezwa kusomwa na katibu Mkuu wa chama Dkt. Bashiru ambaye amesema kuwa Wagombea watatu waliopita ni:
1. Dkt. Khalid Salum Mohamed.
2. Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi.
3. Shamsi Vuai Nahodha.




Maendeleo hayana vyama


1.KUYALINDA MAPINDUZI

2.KUUENZI MUUNGANO WETU.

Maneno ya DHAHABU kabisa.....
 
Hongera Mwinyi kwa kuwa Rais wa Zanzibar 2020.
Mwinyi akishapita hapo tyr ni Rais hakuna kizuizi kingine.
 
Kuna kijana amezuiwa kupewa maiti ya mkewe hapo Muhimbili National Hospital mpaka atakapolipa shilingi 1,470,800.
Wasamaria walimsaidia kuchimba kaburi ili amhifadhi marehemu mkewe lakini kutokana na kuwekewa ngumu na serikali ya wanyonge, wamelazimika kufukia kaburi kisha kumchangia fedha za nauli kijana huyo ili arejee kwao Mtwara.
Hivi sasa huyo bwana yuko njiani akielekea makwao akiwa amebeba kichanga cha wiki tatu na maiti ya mkewe ikiendelea kushikiliwa hapo Muhimbili.

Huyu ni mmoja kati ya wapiga kura mnaowategemea. Kwa hakika hakuna chama cha kidhalimu duniani kinachoweza kuishinda CCM.

Kama umeguswa wasiliana na huyu mnyonge anayeteseka kwa kunyimwa mwili wa mpendwa wake kwa namba ya simu 0778 140 361
Hii serikali ya magufuli ni ya kitapeli sana, imesheheni WAHALIFU LUKUKI. Kuna haja gani ya kuilipisha maiti?
 
Back
Top Bottom