Mkutano wa Kitaifa wa Haki, Amani na Maridhiano, 2022: Rais Samia asema Maendeleo hayafanywi na CCM na Rais pekee, aahidi ushirikiano na vyama vingine

Kumbe tulishakimbizwa uchumi wa kati, sasa mbona hatukuambiwa wajameni? Zile mbwembwe zilivyokuwa wakati tunaambiwa tumeingia uchumi wa kati mbona hazikuwa vile kutuambia tumetolewa
 
CHADEMA wamegoma kuhudhuria ila wanafuatilia mkutano husika kupitia JF, usipoongoza utaongozwa
 
Huu uzi unasinzia labda ni kwa sababu Mwamba Mbowe hajahudhuria au?
Mbowe sio Mtanzania pekee ktk nchi hii, kila raia ana umuhimu wake kama ulivyo uona kwa mbowe na kuto jiona wewe binafsi.
 
Hangaya amesema madai ya Katiba Mpya yako nje ya uwezo wake na hayatekelezeki.
 
Wanaovunja Katiba na sheria ni hao hao wanaohubiri Amani!
Maridhiano hakuna bila kwajibishwa waliotesa na kuua watu.
 
Wanaovunja Katiba na sheria ni hao hao wanaohubiri Amani!
Maridhiano hakuna bila kwajibishwa waliotesa na kuua watu.
Na mwenyekiti wa TCD ndiye makamo wa mwenyekiti CCM. Wonders shall never end.
 
Kwa madini haya sasa unataka longo longo za nini mtu anakufahamisha kabisa linajadilika, ukipewa fursa ya kujadili usiingize hisia zako tuu, nchi hii tulipowengi na tujenge kwa kauli za kuvumiliana
 
UVCCM_ TAIFA
APRILI 05, 2022.

Picha na Matukio ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. KASSIM MAJALIWA akizungumza na baadhi ya mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, BUNGENI JIJINI DODOMA.

#AlipoMamaVijanaTupo
#Kaziiendelee
 
Hapa tumepata Rais sio yule Punguwani alituyefanya tuishi kama Digidigi.
 
Hotuba ileeee!

'Theme' ni ile ile, ya kuwaomba CCM, kumwomba Mwenyekiti wa CCM, Kumwomba Rais, aridhie kuwepo na mabadiliko. Bila wao kuridhia haiwezekani kamwe kuwepo na mabadiliko.

Na ili waridhie, ni lazima mabadiliko yanayopendekezwa yawe rafiki kwa wao. Yaani yasihatarishe uwepo wao madarakani.

'Mentality' ya aina hii ndicho kitakachokuwa kikwazo kuleta mabadiliko yoyote ya maana ndani ya nchi hii.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vyama vya siasa na wadau wengine wa siasa kufanya majadiliano na kutoa mapendekezo ambayo yataleta maridhiano, haki na amani hapa nchini.

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akifungua Mkutano wa kitaifa wa haki, amani na maridhiano uliofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Aidha, Rais Samia amevitaka vyama vya siasa kufanya majadiliano kwa kuzingatia hali ya siasa, uchumi na mazingira halisi ya nchi kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao.

Rais Samia pia amesema Tanzania ilichagua mfumo wa vyama vingi ili kuiwezesha kupata maendeleo kwa haraka hivyo, amewahakikishia kuwa Serikali itashirikiana na vyama vya siasa hususan katika masuala ya kisera na kisheria ili kuijenga nchi.

Vile vile, Rais Samia amekiagiza Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Kuangalia mfumo wa wajumbe wanaounda Taasisi hiyo ili kujumuisha wawakilishi kutoka ngazi zote za kisiasa na kuhakikisha wanafikia malengo yanayokusudiwa.

TCD ni Taasisi isiyo ya Kiserikali iliyoundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mabaraza la Madiwani iliyosajiliwa mwaka 2005.

ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu












View attachment 7.jpeg
 
KATIBA MPYA ni kilio kwa watanzania. Tunahitaji KATIBA mpya
 
Bei zinapanda sababu kukwepa aibu ya kuacha kupeleka hela kwenye miradi mikubwa isotoja ya mwenda ,sasa kuliko aibu bora watu wale nyasi
 
CHADEMA wamegoma kuhudhuria ila wanafuatilia mkutano husika kupitia JF, usipoongoza utaongozwa

Hapa jf sio ofisi ya cdm bali eneo huru la kutoa maoni. Cdm hawajashiriki kama chama, wakati sisi huku kwenye mitandao ya kijamii tunajadili habari yoyote tuitakayo. Pata uelewa wa hili bwana kilaza.
 
Rais Samia amesema vyama vyote vya siasa vimekubaliana kwenda pamoja katika kuwaletea wananchi hivyo atakayewageuka wenzake njiani huyo ni mkosi.

Rais amesema kazi ya vyama vya siasa ni kuangalia utendaji wa serikali hivyo mshikamano ni muhimu.

Source: Eatv habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…