Heri kukopa kuliko ombaomba. Unapokopa unaonesha unauwezo wa kurejesha. Ombaomba utafanywa chochote. Kukopa hata nchi tajiri ukopa. Marekani, Ufaransa, Italy na nyinginezo zinamadeni kibao, kwa kukopa.
Ombaomba, ni kutokuwa na akili za ya kufikiri njia nyingine ya kumaliza au kukabiliana na tatizo.
Tanzania hatuna uharibifu mkubwa wa mazingira. Hivyo unapoomba hizo fedha hata wao wanaangalia na kucheka tu.
Katika uharibifu wa mazingira kuna sheria ya "Polutor pay system" hivyo Tanzania hatumo. Hela za nini, tusiwe tunajidhalilisha. Uwezo wa kutunza mazingira yetu bado tunao sisi wenyewe. Shida serikali haijui kupanga miji yetu. Wao wanadhani kujenga kila sehemu ndo maendeleo. Där es Salaam haina sehemu ya kupumlia, hakuna Park au bustani kubwa za miti katikati ya mji hata pembezoni.
Tanzania tunachojua ni kukatamiti na kujenga. Dar nzima utatembea na miji mingine hakuna hata benchi la kukaa mtu apumzike.
Wakati wa Nyerere alijaribu kuimarisha Park ktk miji kadhaaa lkn baadae ziligeuzwa viwanja kujenga.
Sasa tunachoomba ni nini wakati hatujui hata kutunza mazingira. Serikali ni waongo tu ndo maana fedha ya Uviko wao wanajengea madarasa. Wakati walisema tozo itajenga. Hizo fedha zingetumika kuboresha afya.
Watanzania tunapenda ushabiki, badala ya kumshauri kiongozi nini kifanyike chenye maslahi ya Taifa. Na kubwa wataalam wetu wanacopy na kupaste taarifa na hotuba. Ni wavivu kufikiria jumbo jipya. Hivyo kama Rais si mfuatiliaji atajikuta anajikita yaleyale. Kuomba fedha ni falsafa ya nchi za Afrika zikidhani hela ndo suluhisho kwa kila kitu. Hata wakipewa hazitumiki ktk kusudio lililoombewa.
Ndo maana wazungu wanatudharau na kutucheka kuwa tunafikiria hela na misaada kila wakati.