Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Scotland: Rais Samia ametuangusha

Sasa dar ukipanda miti kwenye eneo la 20*20 utapata hata sehemu ya kupaki baiskeli?
Ndio iwe marufuku kila nyumba iwe na miti hafu 20 kwa 20 ujenzi ni uchafuzi wa mji mtaa unakosa hata kichochoro wala sehemu ya kupita hewa msongamano mkubwa
 
Mbona kaongelea hyo ya Zanzibar na kisiwa kuzama, barafu ya Kilimanjaro kuyeyuka, au ulitaka aongelee uwanja wa ndege wa Chato?
 
Uharibifu wa mazingira nchini Tanzania sio tatizo kubwa. Athari za mabadiliko ya tabia nchi hazitufikii kwa kiasi ambacho kinaweza kufikiriwa. Tanzania sio mlengwa mkuu wa mfuko wa carbon emitters
 
Absolutely, Hangaya aone aibu! Lakini ndio hivyo tena wenzetu hawana aibu wamekaa kimipashopasho tu. Thank you Zygot for sharing.
 
Ndio iwe marufuku kila nyumba iwe na miti hafu 20 kwa 20 ujenzi ni uchafuzi wa mji mtaa unakosa hata kichochoro wala sehemu ya kupita hewa msongamano mkubwa
Hivi kijisehemu Cha 20x20 mtu anajengaje nyumba? Alafu anachimba kisima kirefu cha maji na kuweka underground sewer.
Hatari sana!
 
Labda niku ulize. Njia zipi huwa zinatumiwa na mataifa kupunguza au kuzuia mabadiliko ya tabia nchi?. Viongozi kutoka nchi ambazo zinasababisha mabadiliko haya kwa kiasi kikubwa wamejadili sana kuhusu uwezekano wa kuwa na "Net zero emissions" itakapo fika mwaka 2050. Je huwa wanatumia mikakati ipi kukabiliana na tatizo hili?. Katika kufanya haya, gharama kubwa huwa inahusishwa na kitu kipi labda?
 
Kubali hatima yako. Resign to your fate. Bila ya kuombaomba utawatesa watu tena utaua. Hakuna lolote utakalotoboa bila ya misaada zaidi ya nguo na viatu vyako kwa uchovu.
Hapo ndo tulipofikia?!! "Nchi ya viwanda...!!" Eti bila kuombaomba utawatesa watu, utaua...nk
Ingependeza ikiwa hiyo ombaomba yako ingefanywa kwa staha zaidi - walosaini mikataba mbalimbali yenye utata wakasulubiwa, matumizi mabaya yasokuwa ya lazima yakadhibitiwa, utajiri mkubwa wa madini na raslimali tulizo nazo ukaonekana kutumika vizuri kwa manufaa yetu na ufujaji unaoendelea kupatiwa dawa.
Ni uungwana pia, unapokwenda kuomba, ionekane kuwa wa nyumbani kwako wananufaika. Isiwe unatumia jina la uwakilishi kumbe ni kwa manufaa binafsi. Wanaokufa kwa kukosa matibabu wapungue, wajinga kwa kukosa elimu bora wapungue na tatizo la umaskini pia lipungue, na watu waone kuwa kuna umakini fulani unaoendelea. Na hizo hotuba zinazosifiwa mchana kutwa, usiku kucha zishuhudie hayo.
Kuwa ombaomba isifanywe kuwa tabia au utamaduni wetu... viongozi waone aibu, ingawa kidogo. Otherwise it's more of the same thing. Waimba mapambio nao wajue kuwa kuna wengi wanao kereka na wanayoyaona yakifanyika yasiyo na uhalisia wowote
 
Yani ndio vipigwe marufuku kabisa kwenye miji mikubwa imagine hicho kiwanja kilivo kidogo
 
Sasa amekosea wapi? Mbona unaji contradict mwenyewe. Kwanza unakubali kuwa kwenye mkutano kuna watu wanajuwa kuliko yeye namna Tanzania inavyo athirika na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa hiyo ulitaka arudie wanachoelewa?

Yeye amekidhi matakwa ya presidency kwa kukubali kuchukua hatua dhidi ya ukataji miti na kupunguza uzalishaji wa hewa jivu. Na amwsababisha nchi I qualify kwenye GCF grant ya COP 26!!

Hebu fanyeni ya kwenu na familia zenu, Samia ndiyo Rais na anafanya vizuri
 
Hao US wana miradi mingi wanataka tu data kufanya research zao kwa manufaa yao, watu wana pika data wana pata hela wanasepa, no body is your friend
 
Una kubali kwamba fedha hizo zinapatikana bila kuonyesha mikakati inayo tekelezeka na kubaini uzito wa tatizo hilo nchini?
Hiyo siyo level ya Rais. Kwenye mikutano kama hii, hutanguliwa na technical teams meetings hata mwezi mmoja kabla. Vile vile wakati plenary meetings za Marais zikifanyika kunakuwa na breakaway sessions by agenda and by country. Naamini hiyo mikakati unayoitaja iko kwenye documents za Waziri mwenye dhamana ya mazingira au NEMC
 
Maswali mazuri!
Hatua zipo nyingi sana. Lakini moja wapo kubwa ni kubadilisha technolojia kutoka zile zinazotumia fossil fuels kupata nishati. Hapa zinatafutwa njia mbadala na rafiki kwa mazingira kama jua, upepo, mawimbi ya bahari, geothermal, hydro n.k.
Serikali hizo aidha zinafanya hivyo zenyewe au zinashirikisha sekta binafsi na watafiti!
FEdha nyingi zinahitajika kuwekeza kwenye technolojia hizo mpya ikiwa ni pamoja na kujenga ushawishi kwa wateja na watumiaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…