===
Nimefuatilia mkutano Mkuu wa nishati maarufu kama M300 Africa nimejifunza yafuatayo:-
1. Nigeria na Africa Kusini ndio nchi zilizofanikiwa zaidi kuzalisha na kusambaza Umeme kwa kutumia sekta binafsi ( PPP )
2. Moroco ndio nchi pekee Africa yenye umeme wa bei chini zaidi na unazalishwa na sekta binafsi.
3. Tanzania haiwezi kuendelea na mpango wa TANESCO kuzalisha umeme pekee tukitegemea umeme kuwa wa bei nafuu, Lazima pawepo na ushindani wa bei na huduma,
Ushauri, Nashauri kituo cha Ubia nchi PPPC kutafuta Wawekezaji serious wa nishati nchi ili kuibua ushindani wa kibiashara ili kutoa nafuu kwa walaji ambao ni Wananchi.