Kama utaamua kutumia akili na kuacha hisia za uoga, kusujudu na kuabudu binadamu basi utagundua DINI ya kweli huwezi kuipata kwenye NYUMBA ZA IBADA katika karne hii ya 21.
Ni kwasabau DINI zetu zimeingiliwa na Tamaa, chuki, unafiki, ulafi na uongo wa hali ya juu na tunatumia nyumba za ibada kuficha dhambi Hizi. Viongozi wa dini leo hii wanatukana hadharani wapate nafasi za kisiasa, wanachochea chuki na badala ya kuunganisha watu wao ndio chanzo cha matabaka na mgawanyo.
Hakuna Dini nzuri kama kuhubiri na kuishi UPENDO, kusaidia WAHITAJI na kuwasamahe wale wote waliotukusea. Hizi ni bidhaa adimu kwenye dini za leo ambazo viongozi Wamekuwa MABALOZI wanasiasa.
Inasikitisha kuambiwa Watu hawa wanaliombea taifa amani, taifa ambalo linapandikizwa chuki na visasi vinavyopewa baraka na viongozi hao hao wa dini.
Hawa viongozi wa dini ni wa kupingwa vikali na wanasiasa wa vyama vyote sio CCM, CHADEMA,ACT n.k