Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

Uchaguzi 2020 Mkutano wa Viongozi wa Dini wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuelekea Uchaguzi Mkuu!

viongozi wa dini wapo Kenya kule huwezi kuta wanashirikiana na watu dhalimu ili wapate bahasha,usimama pamoja na walionewa,Viongozi wa dini congo walisimama kidete na wananchi hadi dikteta kabila akaachia madaraka baada ya kuvimbiwa na kulewa kodi za wakongomani na kupelekea kupitisha mkataba wa kutakiwa kukaa madarakani
Kenya kampeni hufanyika hadi makanisani!
 
Kila siku nawaambia dini ni upuuzi lakini hamsikii
sio upuuzi achana na hawa wahuni waliovaa amjoho ambao shetani amewatumia kumkufuru Mungu mbona nchi nyingi tu viongoziw adini awafungamani na madhalimu,nenda hat hapo Kenya tu huwezi kuta wanakaribisha wahuni kwenye madhabahu zao kw akutegemea kuhongwa bahasha
 
Kama utaamua kutumia akili na kuacha hisia za uoga, kusujudu na kuabudu binadamu basi utagundua DINI ya kweli huwezi kuipata kwenye NYUMBA ZA IBADA katika karne hii ya 21.

Ni kwasabau DINI zetu zimeingiliwa na Tamaa, chuki, unafiki, ulafi na uongo wa hali ya juu na tunatumia nyumba za ibada kuficha dhambi Hizi. Viongozi wa dini leo hii wanatukana hadharani wapate nafasi za kisiasa, wanachochea chuki na badala ya kuunganisha watu wao ndio chanzo cha matabaka na mgawanyo.

Hakuna Dini nzuri kama kuhubiri na kuishi UPENDO, kusaidia WAHITAJI na kuwasamahe wale wote waliotukusea. Hizi ni bidhaa adimu kwenye dini za leo ambazo viongozi Wamekuwa MABALOZI wanasiasa.

Inasikitisha kuambiwa Watu hawa wanaliombea taifa amani, taifa ambalo linapandikizwa chuki na visasi vinavyopewa baraka na viongozi hao hao wa dini.

Hawa viongozi wa dini ni wa kupingwa vikali na wanasiasa wa vyama vyote sio CCM, CHADEMA,ACT n.k

Kwenye kila mvutano wa kijamii, lazima wananchi na viongozi na jumiya zao lazima watachagua upande. Kama sio upande wako jitahidi kujiuliza sana , kuna nini?
 
viongozi wa dini wa ukweli hawa hapa.... wanaongea vitu vinavyoeleweka.

viongozi wa dini hawasifu mtu - humsifu MUNGU pekee.

Dunia hii kweli imejaa hadaa eti huyu Katibu wa maaskofu katoliki Kitime nae anatoa ushauri kwa waumini na viongozi-kweli usilolijua sawa na usiku wa giza.
 
Viongozi wa dini sisi waumini tupo nyuma yenu.nyinyi mnaongozwa na roho wa Mungu,mema mnayofanya hakika ni miongozo iliyobarikiwa na Muumba mbingu na nchi.
Mungu awaongoze mzidishie upendo wenu kwa Rais wetu kipenzi JPM.
Hao Viongozi wa dini wahuni
 
Kiukweli hao viongozi watakuwa ni wapumbavu sana!
Mpumbavu ni wewe unayeyauonea haya ukweli wa mambo, Mazuri yakifanywa na yeyote hata ni Chama kipya kitakachoingia madarakani, ifike mahali Kwanza tuyapende yanayofanywa na kusimamiwa vizuri na viongozi wetu na kutoka kila pahala, yakifanywa na mpinzani tuyakubali na kujivunia pia

Tujivunge Kwa lipi kuyaongelea haya mapinduzi makubwa kabisa yaliyofanyika Chini ya usimamizi wa Raisi wetu? Tujivunge kuipenda nchi yetu na vitu vinavyofanyika Kwa sababu Tu kafanya mtu asiyependwa na wapinzani siyo,

Huo ndio upumbavu sasa, tutayapenda na kujivunia yote atakayokuja kuyafanya mh Lisu Pindi Mungu atakapoona vema awe Raisi wetu

Acha Ujinga kuandika Ujinga
 
Kuna haja ya kuacha kwenda MAKANISANI.

MAKANISA yote Ni CCM
Kweli asee tunatakiwa tuache tabia ya kuamini katika dini au makanisa bali tuamini katika Mungu mmoja, kusali sio lazima uwe katika dini fulani au uende kanisani, unaweza hata ukatulia nyumbani kwako na familia yako na mkasali, hizi dini zimeanzishwa na binadamu kama sisi tu, na haya makanisa ni nyumba kama nyumba zingine tu
 
Kama utaamua kutumia akili na kuacha hisia za uoga, kusujudu na kuabudu binadamu basi utagundua DINI ya kweli huwezi kuipata kwenye NYUMBA ZA IBADA katika karne hii ya 21.

Ni kwasabau DINI zetu zimeingiliwa na Tamaa, chuki, unafiki, ulafi na uongo wa hali ya juu na tunatumia nyumba za ibada kuficha dhambi Hizi. Viongozi wa dini leo hii wanatukana hadharani wapate nafasi za kisiasa, wanachochea chuki na badala ya kuunganisha watu wao ndio chanzo cha matabaka na mgawanyo.

Hakuna Dini nzuri kama kuhubiri na kuishi UPENDO, kusaidia WAHITAJI na kuwasamahe wale wote waliotukusea. Hizi ni bidhaa adimu kwenye dini za leo ambazo viongozi Wamekuwa MABALOZI wanasiasa.

Inasikitisha kuambiwa Watu hawa wanaliombea taifa amani, taifa ambalo linapandikizwa chuki na visasi vinavyopewa baraka na viongozi hao hao wa dini.

Hawa viongozi wa dini ni wa kupingwa vikali na wanasiasa wa vyama vyote sio CCM, CHADEMA,ACT n.k
Wa Kwanza bila Shaka ni Mch na Mbunge mh Msigwa, yeye ndiye wa Kwanza

Yeye alimsingizia wizi katibu mkuu wa CCM mstafu Kinana...
 
Kitu kimoja ambacho hawa watu wa utawala huu hawajui ni kuwa karibu 80% ya wapiga kura tayari wanajua watakavyo piga kura.

Hao wanaitwa viongozi wa dini hawawezi kuwabadili watu nia zao kwani wanaogopa sana kuhitilafiana na waumini wao katika maswala yasiyo ya kiroho.

Nimeona niwasaidie hawa watu wa ccm kwa sababu naona wameshikwa mno na kihoro kuelekea kwenye uchaguzi huu kwani naona wana wasiwasi kura za upinzani zinaweza zikapindukia mpaka hadi tume yao izidiwe kufanya uporaji na shinikizo ikawa kali ndani na nje kuwashinikiza watangaze matokeo haraka.

Ccm are vividly rattled, nervous and tense towards this election.
 
Kweli asee tunatakiwa tuache tabia ya kuamini katika dini au makanisa bali tuamini katika Mungu mmoja, kusali sio lazima uwe katika dini fulani au uende kanisani, unaweza hata ukatulia nyumbani kwako na familia yako na mkasali, hizi dini zimeanzishwa na binadamu kama sisi tu, na haya makanisa ni nyumba kama nyumba zingine tu
Uko wapi bwana....✌👍🙏
 
Jamani mbona juzi tu tena hao viongozi wa dini walikuwa CDM na tuliwasifu kwa nyimbo na mapambio inamaana mmesahau kwa muda mfupi hivi, mimi siamini hapa kuna jambo linahitaji kujadiliwa. Au kwa sababu leo wako na JPM tunaanza kuwasema, hapana mtakuwa Mafalisayo wanafiki, tulizeni vichwa mtaujua ukweli ndugu zangu dunia inazunguka.
Mbowe aliwasema taifa bila viongozi wa dini hakuna taifa na hili tulilishika kutoka kwa kiongozi wetu, nandiyo maana TULIANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA .......
 
Back
Top Bottom