Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tumeandika sana tangu Jambo Forum (2006) mpaka hii leo Jamii Forum (2024), kuwa kuna raia wa nnje wamepatiwa pasi za Tanzania na wana vyeo huko serikalini,mashirika ya umma na taasisi za umma,lakini vyombo vya dola vimeweka pamba masikioni.

Kuna miaka ya 2010 hivi RSO wa mkoa fulani alipelekewa "dossier" ya mtu fulani mkubwa,akasema atafanyia kqzi,lakini mpaka leo huyo mtu yupo na nafasi kubwa tuu.

Hii inchi ni kama nyeti za kuku upepo uvumapo.
Ipo siku tutalia.
Mkuu tusichoke kuandika, huenda wakatusikiliza sisi Raia hao wenye mamlaka yao
 
Vyombo vya ulinzi hupambana na tishio. Raia wa nchi yetu anaweza akawa tishio kuliko raia wa nchi jirani au mkimbizi. Sio vizuri kumuonea mtu ambaye siyo agent.
 
Tumeandika sana tangu Jambo Forum (2006) mpaka hii leo Jamii Forum (2024), kuwa kuna raia wa nnje wamepatiwa pasi za Tanzania na wana vyeo huko serikalini,mashirika ya umma na taasisi za umma,lakini vyombo vya dola vimeweka pamba masikioni.

Kuna miaka ya 2010 hivi RSO wa mkoa fulani alipelekewa "dossier" ya mtu fulani mkubwa,akasema atafanyia kqzi,lakini mpaka leo huyo mtu yupo na nafasi kubwa tuu.

Hii inchi ni kama nyeti za kuku upepo uvumapo.
Ipo siku tutalia.
Inawezekana ndio maana Hatupati Katiba Mpya ni sababu ya Hawa watu aliotaja CDF?
 
Samia ameanza kuliagiza jeshi tena kuhusu hizi chaguzi 2 za 2024/2025!!!....

Kwamba Jeshi liwe tayari kwa lolote Lile!

Hii kwa jeshi sio ombi tena!... Ni amri-tekelezi ....Ni tayari!.

Hii ni taa nyekundu tayari kwa vyama vyote kuelekea 2024/25 vijiandae kisaikolojia!

Hii ina Maana chaguzi za 2024/2025 zitakuwa na backup ya jeshi!

Hizi chaguzi hazitakuwa tofauti na ule uchaguzi wa 2019/2020 wa mwendazake.

Hii nchi Bado tuna safari ndefu sana ya kuwa na demokrasia huru.
Kwakweli wamemharibia sana...Hii kauli haikutakiwa ije public...Daah watu wabaya sana!
 
Sheria zetu ziko wazi Utaifa wa Kuzaliwa, wa kujiandikisha na wa kuhamia.
Hapa tz as long as wewe ni supporter wa chama kubwa Hakuna anayekuda Cheti cha Kuzaliwa cha Bibi yako wala Babu yako.
Wapi huwa wanadai vyeti?
 
Kama wapo kwenye nafasi kubwa za maamuzi nini kifanyike juu yao?
Na hao ni waliofahamika, je kuna uhakika gani hao waliofahamika tayari wameshaweka mapandikizi yao huko kwenye ngazi za chini za maamuzi?

Siku zote haya yanasemwa ila leo CDF kusema mwenyewe ni hatari!
Wapo na wengine wanamiliki mpaka Mali,ardhi,mabiashara bongo
Nyie zuba3nizubaeni hko mbeleni hamna chenu [emoji1]

Ova
 
Kama wapo kwenye nafasi kubwa za maamuzi nini kifanyike juu yao?
Na hao ni waliofahamika, je kuna uhakika gani hao waliofahamika tayari wameshaweka mapandikizi yao huko kwenye ngazi za chini za maamuzi?

Siku zote haya yanasemwa ila leo CDF kusema mwenyewe ni hatari!
Na Bora kasema CDF angesema mwingine kingenuka😆😆
 
Ningekuwa Mimi nashauri basi, tuanze upya kama nchi tuandike Katiba mpya, tufanye uchaguzi na power iwe shifted Kwa watu wote Ili kuwe na power control...Hapa Tulipofika sioni mwanga, kama jeshi Lina lalamika, Rais analalamika, sisi public tufanye nini kama mifumo imegoma kufanya kazi?
 
Tulia Mzee,

CDF kasema bado wanatafakari kwanza ili kupata namna bora ya kuwaondosha ama kuwahamisha hapa nchini.
Kwa hiyo wewe, ndugu na jamaa zako mjiandae soon kuwa deported mpaka nyumbani kwenu.
Kwetu ni hapa hapa. Haondoki mtu. Tanzania Hana mwnyewe ukimuondoa MGOGO. Wengine wote ni wahamiaji.
 
Hakuna cha kupambana walienda kwa mafungu kama wakimbizi
Na leo ni Wamarekani na wana haki zote
Wewe unapigania nini sasa hapa wala sikuelewi
Tujikite kwenye hoja ya mkuu wa majeshi
Mnawabagua wasomali kwa muonekano lakini kuna wenye asili ya kibantu kibao hata kabla ya mkoloni
Hata wewe babu yako anaweza kuwa alitokea Malawi ila hamtaki kusema kwa woga tu
Ila you have to be proud aisee kwa asili yako
Hata kama ni nani haijalishi mbona Mkapa walikuwa wanasema wqlitokea jirani na alikuwa mzalendo haswa na kuiongoza nchi?

Kama kuna wahaini au magaidi kamateni lakini Dunia hii hakuna anaeweza kukataza movements za watu
Nikitaka kupita border napita bila hata passport mradi uwe na hela tu kwa nchi masikini
 
Chakufanya ni kuendesha nchi kwa utawala wa sheria. Mamraka yote ya rudi kwa wananchi. Hapo hata mgeni akipewa uraisi haita kuwa na shida kwani atafuwata sheria za nchi na kama akikosea wananchi watamuondowa kwa kura. Siku zote maamuzi ya wengi ni maamuzi ya ki Mungu pia ni ya haki.
Siku izi hakuna hata Askari kidole sasa wageni wana pita watakavyo hadi tunawapa uongozi na wengine tunaoa na kuolewa
 
Back
Top Bottom