Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mtaje please, onyesha uzalendo.Mkimbizi aliyelengwa wa kizazi kimoja anajulikana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtaje please, onyesha uzalendo.Mkimbizi aliyelengwa wa kizazi kimoja anajulikana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024
CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.
Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.
CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.
Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.
RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”
Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.
Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."
Soyo siri kuwa Kagame ametumia nguvu kubwa ku infiltrate vyombo vya ulinzi na usalama.Na inawezekana they mean biznes kulisema hadharan maana wangeweza kuli communicate internally tu.. sasa kuliweka public inaweza ikawa ni message intended to be delivered kwa wahusika..either humu ndani au huko nje
Hii statement kama haijatolewa kisiasa basi ni statement hatari Sana kwa usalama WA nchi! Je ni akina Nani hao?
Inawezekana...Soyo siri kuwa Kagame ametumia nguvu kubwa ku infiltrate vyombo vya ulinzi na usalama.
Si katajwa juu huko mwanzo mwanzo tu, hakuna sababu ya mimi kurudia.Mtaje please, onyesha uzalendo.
Hussein sio Hussein ni Mtanzania ..
Huyo hajawahi kuwa mkimbizi yeye wala wazazi wake, wala babu na bibi zake.
Hiki kitu kinakera saaanaWewe Mtanzania unahenya kupata passport na hata namba ya NIDA lakini wakimbizi kibao wanazo. Hii nchi yaani basi tu!
..Cdf analenga wakimbizi.
..Mama analenga vyama vya siasa.
Tulia Mzee,Hii nchi inapaswa kuiga mfano wa Marekani na Canada. Marekani haina mwenyeji wa asili tena zaidi ya Red Indians ambao kimsingi waliuawa wengi ama kupiungua wenyewe baada ya kukosa uhuru na huduma za msingi. Canada pia kila baada ya muda inapokea wahamiaji wa hiari na wanapewa uraia.
Tanzania karibu kila kabila imetoka nchi nyingine. Cha msingi kwa maoni yangu ni kuwa na Katiba nzuri na Sheria nzuri. Then hata mhamiaji anapewa majukumu na atatekeleza kwa mujibu wa Sheria.
Mbaya zaidi public inaona wazi hampo pamojaCdf anaongea kuhusu wakimbizi lakini mama anaongealea uchaguzi. Kifupi kila mtu hapo alienda na ajenda yake yaani ni sawa mkaenda sehem kwa nia ya kujadili jambo fulani lakini kila mtu akatanguliza shida zake kwanza.
Swali; lengo la mkutano ilikuwa ni kujadili nini?
Unamtukana nani sasa ?Yaani,haya ndio maoni ya CDF! Anasema kuna watu wanapata uraia, bila serikali kujua!? Kuna ubaya gani, MTU kutoka Rwanda, Burundi, Congo, kuomba uraia? Au kwa vile ni weusi? Mbona wa Asia, wazungu,wapo kibao tu,? Kama jeshi, na taasisi zake za, intelijensia, hawana, tskwimu, na wala hawajuhi hao watu, basi, huyu jamaa, ni kilaza kweli kweli, yaani na jwtz na wao wanalalamika! Kuhusu, wakimbizi haramu! Ingekuwa jeshi lenye weredi, angesema, wamekamata watu 3000+walioingia kinyemera! Fucking stupid
Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania
Kamati kuu ya chama cha mapinduzi imemtosa kijana mahili na chipukizi kwenye siasa Bwana Husein Bashe ambaye aligombea kura za maoni ccm kupitia jimbo la nzega na kumbwaga aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bwana lukas selelii kwa jumla ya kura 14,200 za Bashe,dhidi ya 2700 za selelii,na sababu yao...www.jamiiforums.com
Kwa Katiba hii ya Kwetu hata Rais akiwa Mkongo anaweza kuteua wakondo wake na akajaza baraza lote la Mawaziri na wakurugenzi wa mashrika na hatuna cha kufanya na ukihoji unapotea au kupigwa kesi ya Ugaidi unafia jela.Chakufanya ni kuendesha nchi kwa utawala wa sheria. Mamraka yote ya rudi kwa wananchi. Hapo hata mgeni akipewa uraisi haita kuwa na shida kwani atafuwata sheria za nchi na kama akikosea wananchi watamuondowa kwa kura. Siku zote maamuzi ya wengi ni maamuzi ya ki Mungu pia ni ya haki.
Wao walikuwa wapi? Baraza la Usalama la Taifa wao ndio wanakaa vikao wangeambiana huko huko...Cdf kusema wakimbizi wanateuliwa nafasi za maamuzi maana yake analaumu vetting system na mamlaka za uteuzi nchini.
Wao walikuwa wapi? Baraza la Usalama la Taifa wao ndio wanakaa vikao wangeambiana huko huko.
Sheria zetu ziko wazi Utaifa wa Kuzaliwa, wa kujiandikisha na wa kuhamia.Huyo hajawahi kuwa mkimbizi yeye wala wazazi wake, wala babu na bibi zake.