Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024


CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."


Yani utayari huu unapelekwa JWTZ? Kwanini sio wizara ya mambo ya ndani?
Sasa naelewa kwanini CHADEMA wanataka kuandamana.
 
Na inawezekana they mean biznes kulisema hadharan maana wangeweza kuli communicate internally tu.. sasa kuliweka public inaweza ikawa ni message intended to be delivered kwa wahusika..either humu ndani au huko nje
Soyo siri kuwa Kagame ametumia nguvu kubwa ku infiltrate vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Hii nchi inapaswa kuiga mfano wa Marekani na Canada. Marekani haina mwenyeji wa asili tena zaidi ya Red Indians ambao kimsingi waliuawa wengi ama kupiungua wenyewe baada ya kukosa uhuru na huduma za msingi. Canada pia kila baada ya muda inapokea wahamiaji wa hiari na wanapewa uraia.

Tanzania karibu kila kabila imetoka nchi nyingine. Cha msingi kwa maoni yangu ni kuwa na Katiba nzuri na Sheria nzuri. Then hata mhamiaji anapewa majukumu na atatekeleza kwa mujibu wa Sheria.
 
Huyo hajawahi kuwa mkimbizi yeye wala wazazi wake, wala babu na bibi zake.
 
Hii nchi inapaswa kuiga mfano wa Marekani na Canada. Marekani haina mwenyeji wa asili tena zaidi ya Red Indians ambao kimsingi waliuawa wengi ama kupiungua wenyewe baada ya kukosa uhuru na huduma za msingi. Canada pia kila baada ya muda inapokea wahamiaji wa hiari na wanapewa uraia.

Tanzania karibu kila kabila imetoka nchi nyingine. Cha msingi kwa maoni yangu ni kuwa na Katiba nzuri na Sheria nzuri. Then hata mhamiaji anapewa majukumu na atatekeleza kwa mujibu wa Sheria.
Tulia Mzee,

CDF kasema bado wanatafakari kwanza ili kupata namna bora ya kuwaondosha ama kuwahamisha hapa nchini.
Kwa hiyo wewe, ndugu na jamaa zako mjiandae soon kuwa deported mpaka nyumbani kwenu.
 
Cdf anaongea kuhusu wakimbizi lakini mama anaongealea uchaguzi. Kifupi kila mtu hapo alienda na ajenda yake yaani ni sawa mkaenda sehem kwa nia ya kujadili jambo fulani lakini kila mtu akatanguliza shida zake kwanza.

Swali; lengo la mkutano ilikuwa ni kujadili nini?
Mbaya zaidi public inaona wazi hampo pamoja
 
Yaani,haya ndio maoni ya CDF! Anasema kuna watu wanapata uraia, bila serikali kujua!? Kuna ubaya gani, MTU kutoka Rwanda, Burundi, Congo, kuomba uraia? Au kwa vile ni weusi? Mbona wa Asia, wazungu,wapo kibao tu,? Kama jeshi, na taasisi zake za, intelijensia, hawana, tskwimu, na wala hawajuhi hao watu, basi, huyu jamaa, ni kilaza kweli kweli, yaani na jwtz na wao wanalalamika! Kuhusu, wakimbizi haramu! Ingekuwa jeshi lenye weredi, angesema, wamekamata watu 3000+walioingia kinyemera! Fucking stupid
Unamtukana nani sasa ?
 

..Cdf kusema wakimbizi wanateuliwa nafasi za maamuzi maana yake analaumu vetting system na mamlaka za uteuzi nchini.
 
Chakufanya ni kuendesha nchi kwa utawala wa sheria. Mamraka yote ya rudi kwa wananchi. Hapo hata mgeni akipewa uraisi haita kuwa na shida kwani atafuwata sheria za nchi na kama akikosea wananchi watamuondowa kwa kura. Siku zote maamuzi ya wengi ni maamuzi ya ki Mungu pia ni ya haki.
Kwa Katiba hii ya Kwetu hata Rais akiwa Mkongo anaweza kuteua wakondo wake na akajaza baraza lote la Mawaziri na wakurugenzi wa mashrika na hatuna cha kufanya na ukihoji unapotea au kupigwa kesi ya Ugaidi unafia jela.
 
Huyo hajawahi kuwa mkimbizi yeye wala wazazi wake, wala babu na bibi zake.
Sheria zetu ziko wazi Utaifa wa Kuzaliwa, wa kujiandikisha na wa kuhamia.
Hapa tz as long as wewe ni supporter wa chama kubwa Hakuna anayekuda Cheti cha Kuzaliwa cha Bibi yako wala Babu yako.
 
Back
Top Bottom