Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tumekuwa tukifanya chaguzi tangu enzi za Nyerere hadi sasa lakini jeshi halijawahi kuingilia kati. Inakuaje sasa Samia anataka kuliamuru Jeshi kuingilia uchaguzi? Nadhani anataka kupora uchaguzi kwa nguvu kwa kutumia nguvu ya jeshi. Labda atuambie nchi au magaidi wanaotaka kuvamia uchaguzi hadi aamue kutumia jeshi kwenye mambo ya uchaguzi badala ya polisi.

Kufanya hivi pia ni ishara kuwa jeshi la polisi haliaminiwi tena kwenye masuala ya usimamiaji wa uchaguzi na pia katika mambo ya ulinzi na usalama wa raia pamoja na mali zao. Kwa maana hiyo basi ni bora akalivunje jeshi la polisi na kuimarisha jeshi la ulinzi zaidi. Polisi wanaonekana wapuuzi tu, hawana thamani wala msaada wowote kwenye masuala ya ulinzi. Hili ni tusi kubwa sana ambalo Samia amewatukana polisi kwa vitendo.

Na pia kitendo cha kuamrisha jeshi lisimamie uchaguzi kitasababisha msuguano na uhasama kati ya polisi na wanajeshi. Au anataka kuwapiganisha kwa makusudi? Samia anapaswa achunge sana kauli zake kwani zina hatari ya kuwagawanya wanausalama kwa makusudi na kuwapa mwanya maadui wapenye nchini kwa urahisi. Kwa lugha nyingine ni kwamba kauli zake zinatia rehani maisha, usalama na mali za raia. Kuna shida mahali kwenye uongozi wa huyu mama; sio bure.
 
nenda kwa cdf general john jacob mkunda anazo zote hadi picha na taasisi zao sawa?

Wewe ndio umeanzisha uzi. You were supposed to put evidence , when you tell people to search for evidence , it becomes an accusation

Mamlaka ya Intel inafanya kazi vizuri

Hata huko jeshini wapo na ni kazi ya Tanzania Intel
 
Hiv kwamfano hapo msomali akafanya yake tokea mbali ikawa juu chin chini juu itakuaje?????
Hussein Bashe hana uwezo huo. Yeye atakuwa anatumiwa tu na nchi yake ya Somalia kuipeleleza Tanzania kwa maslahi ya taifa lake.
 
Wewe ndio umeanzisha uzi. You were supposed to put evidence , when you tell people to search for evidence , it becomes an accusation

Mamlaka ya Intel inafanya kazi vizuri

Hata huko jeshini wapo na ni kazi ya Tanzania Intel
acha kunipotezea muda kwani utakuwa umevimbiwa upumbavu sawa?
 
Mipango juu ya mpango
Si wampige repatriation tu arudi kwao Burundi badala ya kuanza kumfanyia visa mzee wa watu? Mzee kwanza tangu aumwe korona hajapona vizuri wanaanza kumchokonoa!
 
Huenda kwa maneno mengine CDF amemtahadharisha Mama kuwa safari hii kwenye chaguzi zinazokuja Uraia uzingatiwe sana! Kuanzia ngazi ya Kitongoji/Mitaa,Kata,Wilaya,Mikoa na Taifa!
 
Tatizo teuzi nyingi zimeacha kuzingatia maoni ya upekuzi wa kiusalama hususani kwenye nafasi za maamuzi. Turudi kwenye utaratibu wetu na idara hii iwezeshwe kikamilifu na iheshimiwe.
 
kwa taarifa za uhakika nilizinazo kuna nchi tatu ambapo mbili ni kubwa na nyingine ndogo ila ina watu makatili mno ndizo zimepandikiza watu wake katika taasisi muhimu na nyeti za tanzania na kama kuna nchi ambayo wala haina mpango wala muda wa kupoteza kuhangaika na tanzania ni ya rwanda

Chuki zetu kwa Rwanda ni laana kwetu kwani tunaisingizia wakati ndiyo taifa pekee ambalo linatufundisha watanzania ( mimi na wewe ) jinsi ya kufikiri na hata mimi mpemba ameir seif wete paje kidagaa ( cognizant ) nikiwa hapa kwangu pemba najifunza kutumia akili kama wanyarwanda ambao wanajua kufikiri kuliko mazuzu na maandamano yao ya kipuuzi yajayo
 
kwa taarifa za uhakika nilizinazo kuna nchi tatu ambapo mbili ni kubwa na nyingine ndogo ila ina watu makatili mno ndizo zimepandikiza watu wake katika taasisi muhimu na nyeti za tanzania
Uingereza, Ufaransa na Uholanzi.

Waingereza wameua sana watu iwa Ukatili. Wachawi wote Uingereza waliuwawa.

Ufaransa walinyonga wale wote waliojifanya ndie wenye Nchi. Waliua mpaka Mfalme-Kikatili

Uholanzi ndio Usiseme. Kama sio Shaka Zulu, leo tusingewasikia kina Mandela. Walikuwa makatili sana.

Tatizo, wamejichimbia(embed) kwa vigezo vya Uwekezaji na Uraia Pacha hapa kwetu. Mpaka CDF hajui anajua.

Hatar
 
Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."
Safari yoyote unapoelekea usipopajua ni mbali kwenda tu sababu muda mwingine utautumia kuulizia uelekeo au kuutafuta uelekeo Ila kurudi sio mbali
 
Na mimi naona hivyo
 
Mtajuana bwana. Sisi hayatuhusu tunawaza Umeme na Mfumuko wa bei.
 
Kingine CDF kuna gepu ameacha wazi angetaja na majina hata mawili matatu km mfano wa hao waliopenyezwa huko kwenye idara nyeti kwamba huyu hapa raia wa Somalia Ila kapachikwa TISS anafanya nini kule na kapewa mafaili yote nyeti yanayotuhusu kwanini?
 
Nadhani masuala ya immigration hayawazii sana anawaza masuala ya uchaguzi tu na mwamvuli wa Jeshi uwe juu yake umlinde ashinde uchaguzi hayo mengine ya uraia na majasusi kujipenyeza idara nyeti yanazungumzika tu Ila uchaguzi kwanza ndio wa muhimu inabidi CCM ashinde kwa Ulinzi na usalama wa Jeshi, ndio nilivyoelewa

Idumu Mizimu!
 
Hawa mnaowakataa kuwa hapa sio kwao ili hali walizaliwa hapa na babu zao wamezikwa hapa, mkiwafukuza mnataka waende wapi? Hawa wakiwa wengi ndio watakwenda misitumi na watawasumbua sana!
 
Tuliona kwa JM Kikwete na akina Lt Gen Shimbo. Nadhani kuna 'copy and paste'.
Hakuna sababu zozote za kuliandaa Jeshi kwa mambo ya ndani 'internal affairs' Nadhani amehisi jambo
Hakuna shaka Polisi haiaminiwi na wenyewe lakini kuna hoja, kwa mtu aliyeeona Polisi amesimama masanduku ya kura feki yanaletwa anasema siyo kazi yake ni ya Tume, hapaswi kuaminiwa tena
Polisi walionyeshwa kura feki nao kama raia wanasema hawana mamlaka ya kufungua mashtaka

Sidhani kamani tusi, nadhani amewaambia ukweli, hawaaminiki na hawana uwezo
Hili ni jambo linalofanywa na Wanasiasa kwa faida za muda mfupi bila kujali madhara ya siku za baadaye.
Jeshi limefunzwa 'kuua' halikufunzwa kushughulika na Wananchi. Kuliingiza katika siasa si jambo la busara

Yes Wanasiasa watafurahi watu wakipata madhara, wasichokumbuka ni kwamba jeshini kuna watu ambao ni Watanzania na ni ndugu zetu na wana ndugu zao Watanzania wenye hisia ziwe za michezo , siasa n.k
Inatosha tuishie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…