Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Pre GE2025 Mkuu wa Majeshi: Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024

CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."

Kama kijana kakulia Tanzania kuanzia akiwa mdogo kumuondoa kwenye madara kwasababu ya wazazi kuwa wakimbizi ni ubaguzi na haina manufaa yeyote. Tuwape uraia watu na tuondokane na ubaguzi
 
Ni kweli ila ni mali yako lazima udai
Cha kufanya tuachane na utaratibu wa vyeti bali Kila kitu kiwe compurized pale mtoto anapozaliwa tu basi taarifa zake ziingizwe chapu kwenye mfumo, na mifumo isomane mtu akisema amezaliwa sehemu flani basi chapu unaingia website Kila kitu unakikuta vyeti vinaoza,vinaliwa na panya,mende,vinasombwa na mafuriko,vinaungua na moto n.k
 
Cdf anaongea kuhusu wakimbizi lakini mama anaongealea uchaguzi. Kifupi kila mtu hapo alienda na ajenda yake yaani ni sawa mkaenda sehem kwa nia ya kujadili jambo fulani lakini kila mtu akatanguliza shida zake kwanza.

Swali; lengo la mkutano ilikuwa ni kujadili nini?
Hizo taarifa za cdf rais huzipata zikiwa za moto,hapo mlikula mnapewa wengine taarifa
 
Kama kijana kakulia Tanzania kuanzia akiwa mdogo kumuondoa kwenye madara kwasababu ya wazazi kuwa wakimbizi ni ubaguzi na haina manufaa yeyote. Tuwape uraia watu na tuondokane na ubaguzi
Mijitu isiyokuwa na exposure ni ya hovyo kwelikweli, hao Uingereza wenyewe PM wao sasa hivi ni Muhindi.

Huyo CDF ukute nchi alizotembea ni Cuba, China na Urusi tu hana exposure.
 
Umesahau aliomba uraia kipindi cha Chikwete ?.
Wakati baba wa Bashe,sheikh mkuu wa nzega, Muhammad Ibrahim Bashe akiingia tz,Bashe alikua kishazaliwa,wazazi wake waliukana usomali lakini Bashe hakufanya hivyo,ndiyo matatizo Yale ya 2010,Ila wadogo zake Bashe yaani marehem Ismail,mushtar,kauthar na Ibrahim,walizaliwa tz wazazi wao wakiwa washaukana usomali na kuwa watz
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Januari, 2024

CDF: VIJANA WETU WA MIAKA 15 HADI 35 WANALENGWA NA WANA MTANDAO WA UGAIDI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema hali ya ulinzi na usalama ni shwari licha ya uwepo wa matukio ya kigaidi na itikadi kali na kuwa kuna vijana wanaochukuliwa na kwenda kujiunga kwenye makundi ya Kigaidi Nchini DR Congo, Msumbiji na Somalia.

Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anashiriki kwenye Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

CDF: BAADHI YA WAKIMBIZI WAMEPEWA TEUZI SERIKALINI KATIKA NAFASI ZENYE MAAMUZI
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Jacob John Mkunda amesema kuanzia Januari Mosi, 2023 hadi Desemba 31, 2023 jumla ya Waomba Hifadhi 138,149 walipokelewa Nchini Tanzania.

Ameongeza kuwa imebainika baadhi ya Waomba Hifadhi au Wakimbizi au familia zao wameteuliwa Serikalini katika nafasi zenye maamuzi.

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa CDF na Makamanda unaofanyika 302 KV Brigade Mess, Mwenge Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

RAIS SAMIA: JESHI LIWE TAYARI KUKABILIANA NA CHOCHOTE KITAKACHOJITOKEZA
Rais Samia Suluhu amesema "Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba Mwaka huu (2024) na Mwakani (2025) tunatarajia kuwa na chaguzi na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii.”

Amesema hayo katika Mkutano wa Saba wa Mkuu wa Majeshi-CDF na Makamanda wa Mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2024.

Ameongeza “Ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza."

Enzi ya baba wa taifa mapinduzi karibu yafanyike kwa kuratibiwa na wenye asili ya rwanda. Hao watutsi walikua wanafanya mikutano yao dsm na ngara wakipanga na wanajeshi jamaa zao namna ya kumuangusha mwalimu na wao kutwaa madaraka. Kwa hiyo ushauri uchukuliwe kwa uzito unaostahili. Kuna kabila wakikaa mahali wanataka lazima wao wawe watawala.
 
Kwa kweli usalama wa nchi yetu upo kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu kwa sababu kama hali ipo hivyo na CDF anajua lakini hachukui hatua hilo ni tatizo.
Natoa rai kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuchukua hatua haraka lakini nawaza je ikiwa huko nako wapo itakuwaje? Watanzania tuombe na kusali hatupo salama kabisa tusijidanganye ipo siku tunaweza kujikuta tunatangaziwa kuwa sasa tupo chini ya utawala wa nchi fulani jirani maana wakati huo tunaweza kuwa tupo chini ya viongozi wakuu wote ni kutoka nchi hiyo.
Kazi ni kuonea watu tu hata wakati ule wa mapambano na "Magaidi" kule kibiti sikuwahi kuamini kama kulikuwa na magaidi.
 
Aise! Wao waliteuliwaje katika teuzi hizo na waliajiriwaje katika nafasi mbali mbali?
 
Sasa CDF analalamika au anapongeza wakimbizi kupenya serikalini?

Au anaripoti, anakemea au ni nini shida?
Mnataarifiwa watanzania. Ni taarifa ambayo CDF ameamua kuichomoa toka kwenye hadhi ya SIRI na kuileta kwa jamii. Mchango wako juu ya hili ni muhimu kwake.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Baada ya kusoma comment mbali mbali za wadau nimegundua watz wengi hakuna wanachokijua,kwanza kabisa tutambue tangu mwaka 1972 yaliyokua makazi ya wakimbizi ya ulyankulu,katumba,mishamo na kigoma huko watu tangu mwaka huo kutoka ktk makazi hayo wanasoma na kuhitimu shule mbali mbali zilizoko nchini haya tujiulize,Kila mwaka wanahitimu je wanaenda wapi Kama sio kwenye mfumo wa ajira.Kwa hiyo hao watu wametapakaa kwenye Kila idala na hapa CDF kachelewa kulijua na Wala tatizo sio wao bali watz wenyewe tu.Hata hao anaofanya nao kazi CDF Kuna wengine ni wenyewe ni ngumu kumtambua mtu ukizingatia nchi zetu za Africa hazikua na utaratibu wa kuwatambua watoto mapema mahali waliko zaliwa kutokana na ufinyu wa miundombinu na usikute mpaka saivi Kuna watu Bado wanajifungulia nyumbani.
Kama wamezaliwa Tanzania hao sio wageni. Kitu mhimi ni kuimalisha mifumo ya sheria na elimu ili wote wanao zariwa Tanzania wawe watanzania kiakiri na kitabia. Nchi kama marekani mtoto yoyote aliye zariwa kwenye ardhi Yao hata kama wazazi wake ni wahamiaji halam, mtoto anakuwa ni marekani kama wa marekani wengine. Kwa nchi zenye utawala wa sheria haijarishi umepata je uraia kinacho matters ni unachagiaje kwenye uchumi.
 
CDF yupo sahihi, kazi ya Jeshi ni kulinda mipaka ya nchi na katika hilo wameona tatizo.

Kazi ya kutathmini ilipaswa kuwa ya Uhamiaji na TISS, kwa bahati mbaya wapo 'busy' na mambo yasiwahusu.
Kwa mfano Uhamiaji imetumika kuadhibu watu kisiasa, TISS wapo mguu sawa na Wapinzani

Afadhali CDF amesema maana wahusika hawana habari na hili ni jambo la hatari.
Lakini pia vetting katika ajiri na Teuzi ni tatizo ambalo TISS walipaswa kuliona

Pili, Tanzania ina Wakimbizi katika Vijiji bila kuwatawanya. Ipo siku Watakuwa M23 n.k. kwasababu wana maeneo.
DRC wanalipa gharama ya uzembe, '' Raia '' waliokuwa wakimbizi kutoka Rwanda sasa wanashirikiana na Rwanda

Wakimbizi walipaswa kutawanywa ili wachanganyike na Raia wengine si kuwapa ' nchi' ndani ya Nchi

Tatu, kikao hiki kimefanywa kwa 'mkakati' wakati CDM wakiandaa maandamano na fagio la RC kudoda.

RC alilitumbukiza Jeshi katika uzoaji taka, sasa Rais analiingiza Jeshi katika siasa kwa njia ya usalama wa uchaguzi.
Hapa anawaamuru kwamba wakipata maagizo waingilie kati. Ipo siku utasikia '' tumebaini' viashiaria vya hali XX

Bado tatizo la kuliingiza Jeshi katika siasa lipo pale pale ingawa leo limefanywa 'kiufundi' .
Hatari ni kwamba Jeshini kuna Watu wenye itikadi tofauti za kila eneo iwe siasa au dini.

JokaKuu Tindo Pascal Mayalla
 
Na leo ni Wamarekani na wana haki zote
Wewe unapigania nini sasa hapa wala sikuelewi
Tujikite kwenye hoja ya mkuu wa majeshi
Mnawabagua wasomali kwa muonekano lakini kuna wenye asili ya kibantu kibao hata kabla ya mkoloni
Hata wewe babu yako anaweza kuwa alitokea Malawi ila hamtaki kusema kwa woga tu
Ila you have to be proud aisee kwa asili yako
Hata kama ni nani haijalishi mbona Mkapa walikuwa wanasema wqlitokea jirani na alikuwa mzalendo haswa na kuiongoza nchi?

Kama kuna wahaini au magaidi kamateni lakini Dunia hii hakuna anaeweza kukataza movements za watu
Nikitaka kupita border napita bila hata passport mradi uwe na hela tu kwa nchi masikini
Mambo ya ugaidi yametoka wapi tena kinachoongelewa ni watu kufuata utaratibu ndo maana ya kuwepo uhamiaji hata marekani watu kibao wanakua deported sababu tu hawajafuata utaratibu
 
Back
Top Bottom