Mkuu wa majeshi wa Uganda, Gen. Muhoozi Kainerugaba, anapanda mbegu gani kisiasa na anatoa ujumbe gani kwa demokrasia ya Afrika Mashariki?

Hakuna demokrasia hapa mkuu,,, ni uhuni wa watu wachache,,,,, tofauti yetu na Uganda ni kwamba Museveni anatumia jeshi moja kwa moja kukaaa madarakani,,,, ila nyie mnatumia indirect….kwa kuiba na kutisha watu.
 
ukiona mambo kama hayo yanatokea na raia wapo kimya ujue hakuna mbada wake kungekuwa na mbadala wake raia wangeshafanya maamuzi magumu
hofu yangu ni kwamba majigambo yake yanaweza kuwaudhi maafisa vijana wenzake na hata wazee wazoefu na wenye nguvu humo humo UPDF ambao pia wanaweza kupanga mapinduzi na ikasababisha hali mbaya zaidi uganda 🐒

ikitokea hivyo raia wote wa UGANDA wataunga mkono mapinduzi hayo coz wameichoka sana familia ya m7.
 
Hakuna demokrasia hapa mkuu,,, ni uhuni wa watu wachache,,,,, tofauti yetu na Uganda ni kwamba Museveni anatumia jeshi moja kwa moja kukaaa madarakani,,,, ila nyie mnatumia indirect….kwa kuiba na kutisha watu.
Nyinyi kina nani tena gentleman?

eleza kwa kina kifupi kidogo kwa faida ya wadau 🐒
 
Yuko sahihi bora waafrica tuongozwe kwanza na wanajeshi hadi wanasiasa wapate akili ,waache kuahirisha kufikiri kizalendo, kama burkina faso ndiyo mfano mzuri kwasasa
 
Jitahidi unavo andika maada mtandaoni
Ambatanisha
1.Picha
2.chanzo cha habari
3.Ushahidi au nukuu

Usiandike tu kama kijana wa mparange aliyeokota simu
 
Kama siyo kifo cjui hata sisi leo tungekuwa wapi
 
Yuko sahihi bora waafrica tuongozwe kwanza na wanajeshi hadi wanasiasa wapate akili ,waache kuahirisha kufikiri kizalendo
sawa umewabeza wanasiasa ni uhuru na haki yako ya kutoa maoni,

vipi kuhusu vijana na wazee wenye nguvu na vyeo humo ndani ya hilo jeshi la UPDF, waliochoshwa na utawala wa kijeshi wa familia ya Mseveni, na wenye nia na dhamira thabiti ya kuona uganda inafaa kuongozwa kiraia, wanajiskiaje kwa kauli hizi za Gen Muhozi?🐒

huoni hatari ya mapinduzi zaidi hapo?
 
Kwani hapo kuna tofauti ipi na CCM ya TZ? Si huwa mnabadirisha magarasha tu; wote Sawa tu, Africa ni laana
 
Sawa...kuna hotuba yake moja alisema ilikumtoa na wao waingie
Msituni 😄 mpaka akawa anajiita quarter pin

Ova
 
Jitahidi unavo andika maada mtandaoni
Ambatanisha
1.Picha
2.chanzo cha habari
3.Ushahidi au nukuu

Usiandike tu kama kijana wa mparange aliyeokota simu
Huyu Generali yuko vizuri kichwani amesomea mambo mengi wewe Google tu kuhusu yeye, alipelekwa kusoma shule nzuri
 
Huyu Generali yuko vizuri kichwani amesomea mambo mengi wewe Google tu kuhusu yeye, alipelekwa kusoma shule nzuri
Basi shule itakua imemuharibu sana, amejaa akili mingi mno, mpaka sasa upeo, Ufahamu na uelewa wake umekua wa kupindukia, na inaonekana upeo huo unamrejesha utotoni kifikra kwasababu maoni yake yaliyojaa, majivuno, kiburi na jeuri yanaamsha hasira za raia na vijana kwa wazee wenye nia nadhamira ya dhati ya kuona Uganda yenye utawala wa kiraia unasonga mbele kwa mipango madhubuti ya maendeleo na sio majivuno na majigambo mtu fulani 🐒
 
Hana busara kabisa na staha ya mdomo wake. Si unakumbuka dharau zake kwa Nchi na jeshi la Kenya mpaka ikabidi baba yake aombe msamaha kwa wakenya.
Yes,
nakumbuka vizuri sana ile,
For sure the gentleman ni tishio kwa demokrasia ya uganda,

Lakini pia kwa uhai na ustawi wa jumuiya ya Africa Mashariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…