Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga: RUWASA Hakikisheni Wananchi Wanapata Maji Safi na Salama Muda Wote

Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga: RUWASA Hakikisheni Wananchi Wanapata Maji Safi na Salama Muda Wote

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mkuu wa Mkoa Manyara, Mhe. Queen Sendiga amewataka Wakala wa Maji na USAFI wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha wananchi Mkoani humo wanapata huduma Bora ya maji safi na Salama muda wote.

Ameyasema hayo katika kikao cha watumishi wa RUWASA Mkoani humo kolicholenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika Kutoa huduma Bora za maji Kwa wananchi wa vijijini.

Meneja Wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Manyara Walter Kirita alitangaza dhamira hiyo katika kikao kazi cha watumishi wa RUWASA mkoa wa Manyara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya White Rose Wilayani Babati.

Kirita ameisema Taasisi ya RUWASA wakati inaanzishwa upatikanaji wa maji ulikuwa ni asilimia 55.5 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 70.5 Disemba 2023 ambapo kufuatia miradi ya maji inayoendelea kiwango hicho wanaimani kuwa kitaongezeka.

Azma hiyo imekuja wakati Dunia ikisheherekea siku ya familia duniani tarehe 15 Mei ya kila mwaka yenye lengo la kukumbusha wajibu wa kulea familia sambamba na umuhimu wa upatikanaji wa maji kwa familia.

Naye, Meneja raslimali watu kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mkuu RUWASA, Philemena Luambano alisema kuwa Taasisi hiyo itaendelea kufanyakazi kwa kuzingatia ilani ya CCM inayotamka kumtua ndoo mama kichwani.

WhatsApp Image 2024-05-16 at 23.20.07.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-16 at 23.20.08.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-16 at 23.20.08(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-05-16 at 23.20.10.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-16 at 23.20.09.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-16 at 23.20.10(1).jpeg
 
Back
Top Bottom