Wanabodi,
Delaration of interest: Mimi Pasco wa JF, Siungi mkono ubaguzi wa aina yoyote ila pia siungi mkono superiority ya baadhi ya makabila kujiona bora kuliko makabila mengine, huu pia ni ubaguzi mbaya kabisa!.
Kuna baadhi ya makabila, wanajisikia sana, na kujiona makabila yao ndio makabila bora na ya maana sana kwa sababu au wamesoma sana, wana pesa sana, wanamaendeleo sana, na kudharau makabila mengine kwa uduni wa makabila hayo au kwa umasikini!, wao kila mahali ndio wanajiona ndio bora kuliko wenyeji! kwa kugombea majimbo ya wengine!, kwa yale maeneo ambayo wenyeji ni kweli hawana uwezo kabisa, it is ok wakiwakilishwa na mtu mwingine yoyote wa kabila jingine lolote mwenye uwezo, lakini kwenye maeneo ambayo wenyeji wenyewe wapo wenye uwezo wa uongozi lakini hawana uwezo wa kifedha kushindana kwenye chaguzi ambazo fedha ndio sifa kuu ya ushindi, natoa wito kwa wenyeji wajengewe uwezo nao wajiwakilishe!.
Kama kuna wenyeji na wana uwezo, kwa nini wawakilishwe na mamluki miaka nenda miaka rudi?!, ifike mahali wenyeji wenyewe wawashukuru hawa mamluki wageni waliowawakilisha kwa kuwaeleza wazi kuwa wanawashukuru sana kwa uwakilishi wao miaka yote iliyopita wakati wao hawana uwezo na kuwashukuru kwa asante kwa kazi nzuri na mema yote, lakini sasa imetosha, ama waende wakagombee makwao, au washindane kwa ushindani wa haki kwa kupanda ulingoni na wenyeji waliojengewa uwezo!.
Kutawaliwa na wageni wahamiaji kwa muda mrefu sana nako kunachosha!, utadhani wenyewe hawapo kumbe wako kama mazuzu tuu!. Kama wenyeji wameacha uzuzu wao, nao sasa wameamka kudai haki yao ya uwakilishi wa watu wao, wapewe haki hiyo!, tena nashauri hata zoezi la kujiandikisha, kila mtu aende akajiandikishe kwao, ili uwingi wa mamluki kwenye baadhi ya maeneo, upungue, na kusipelekee eneo hilo kuendelea kuwakilishwa na mamluki miaka nenda miaka rudi as if hakuna wenyewe!.
Mfano mimi ni Msukuma, nalitamani sana jimbo la Lyatonga kule Moshi Vijijini, niruhusiwe tuu nikagombee popote, lakini kiukweli kule Uchagani wewe kama sio Mchagga, utaanzia wapi kabla ya kuitwa "kyaska" lakini kwa upande wa Wachagga, ambao kwenye maeneo waliolowea hivi 'vyasaka' vyao vimetapakaa majimbo ya wenzao!, yaani kwao ni kwao na kwa wenzao ni kwao!. Hii ni kama 'changu changu', 'chako changu' 'chake changu', 'chao changu', 'chetu changu'.
Yaani eneo lao ni kwao tuu, na wao tuu, lakini maeneo mengine yote kwa wengine pia ni kwao!.
Sorry kwa mtakaoniita mbaguzi, huo ndio ukweli wenyewe, kama wenyewe pia wapo wajengewe uwezo na waruhusiwe kugombea sambamba na wageni, kama wenyeji wapo lakini hawana uwezo, then wajengewe uwezo hata kwa affirmative action, washike wenyewe nafasi za uongozi sambamba na wageni, na sio kila siku kushikiwa tuu na wageni miaka nenda, miaka rudi!.
NB. Kuna makabila yenye kupenda kesherehekea defloration kwa shuka nyeupe kuonyeshwa hadharani ndipo sherehe ya ndoa hufuatia!, ikitokea mhusika ameshindwa kufanya defloration, ili kukinga aibu kwa familia, kaka mtu au hata ikibidi baba mtu, huingia kusaidia kwenye hiyo process ya defloration, na baada ya hapo, huendelea kuservice hadi mhusika apate uwezo na kama anachelewa kupata uwezo, juhudi za dhati za kumjengea uwezo hufanyika!. Sasa hao ambao kila siku huwa wanashikiwa na kuservisiwa na watu baki, wataservisiwa hadi lini?!. Natoa wito wenyeji wajengewe uwezo waji service wenyewe!.
Kama kitendo cha kuomba, wasio na uwezo, wajengewe uwezo kwa affirmative action nako kutatafsiriwa kuwa ni ubaguzi, then najikubali mimi Pasco wa JF ni mbaguzi wa affirmative action!.
Pasco