Udhibitisho wa kasoro za Katiba tuliyonayo sasa.:
1.Haki inaweza kuporwa wakati wowote.
2.Kura inaweza kuporwa wakati wowote.
3.Uhai unaweza kuporwa wakati wowote.
4.Demokrasia inaweza kuporwa wakati wowote.
5.Mhimili wa Mahakama unaweza kuingiliwa wakati wowote.
Rasimu ya Katiba mpya,ni kiporo ambacho CCM imekatalia kisipashwe.
Tukumbuke fedha ya umma ilitumika kuandaa "Rasimu ya Katiba" mpya,lakini CCM ikaomba isubiri kwanza."Tatizo linaonekana lipo wapi"
Sasa madhara ya kutotekeleza mapendekezo ya Rasimu ya Katiba mpya,Watawala wanatumia mabavu na nguvu kubwa katika kukabiliana na wananchi wenye fikra mbadala.
Kila mtawala anasogeza mbele utekelezaji wa mapendekezo ya katiba mpya,"Baba wa taifa alishasema Katiba iliyopo sasa inamapungufu(Kama kweli tunamheshimu Baba wa Taifa),na inaweza kumfanya kiongozi kuwa dikteta na kujikuta anakuwa juu ya sheria"
Tukumbuke Bunge lilipitisha sheria ya kutoshitakiwa baadhi ya watendaji katika vyombo vya dola,sasa hii madhara yake ndio tunaiona sasa,mwananchi wakati wowote unaweza kuchukuliwa hata usiku bila utaratibu,kuteswa hata kupotezwa.
Badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma kidemokrasia,kiuchumi na kijamii.