Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Habari zinazoingia KLH News Studios.. zinasema kuwa Jaji Mkuu Bw. Barnabas Samatta amesikitishwa na yale yaliyotokea siku ya Alhamisi... habari zaidi kufuata..!
 
Mungu ni mwema . Kuachiwa Ditto kutaamsha mambo mapya . Wameanza wenyewe wacha tuone watakapo ishia .
 
Dito shakani:Kufunguliwa kesi upya, mahabusu leo wagoma

2007-03-12 15:52:42
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Siku chache tu baada ya kuachiwa kwa dhamana na Korti Kuu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Kapteni Mstaafu Ditopile Mzuzuri, yuko shakani kufunguliwa kesi nyingine mpya inayohusiana na ile inayomkabili sasa ya kumuua dereva wa daladala bila ya kukusudia.

Hofu juu ya kufunguliwa upya kwa kesi hiyo ambayo sasa ingali ikiendelea Kortri Kuu inatokana na tishio linalotolewa sasa na kiongozi wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, anayedai kuwa mkuu huyo wa zamani mkoani Tabora anastahili kushitakiwa kwa `Kesi ya Mauaji` na wala siyo ile inayoendelea sasa ya \'kuua bila ya kukusudia`.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, Mchungaji Mtikila amesema lazima afungue kesi hiyo mapema iwezekanavyo ili kuona haki ikitendeka, huku akidai kuwa ile ya sasa siyo hasa anayostahili kukabiliwa nayo Dito.

Akasema Mtikila kuwa leo atawasiliana na jopo la mawakili wake ili ikiwezekana, kama si mchana wa leo hii, kesho asubuhi aweze kuifikisha kesi hiyo mpya haraka iwezekanavyo.

`Mimi na wanaharakati wenzangu tumeamua kufungua kesi hii chini ya utaratibu wa mashtaka binafsi kwa sababu ya kutoridhishwa kwetu na namna kesi ya sasa ya Bw. Ditopile inavyoendeshwa,` akasema Mchungaji Mtikila.

Amesema hata kama mawakili wake watashindwa kutekeleza azma yake hiyo, yeye binafsi yuko tayari kutinga Mahakama Kuu, akidai kuwa anayo haki ya kikatiba kuweza kufanya hivyo.

`Mimi mwenyewe ni mwanasheria, na tena ni Mtanzania mwenye haki zote za kikatiba� ninayo haki ya kwenda mahakamani hata kama sitakuwa na wakili,` akasema, huku akiitaja Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndiyo inayompa `jeuri` hiyo.

Amesema wakati akichukua uamuzi wa kwenda mahakamani kufungua kesi upya dhidi ya Dito, amemwandikia barua Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Alfred Tibaigana, akimtaka awalinde mashahidi muhimu waliokuwepo wakati wa tukio hilo.

Katika kesi ya sasa, Ditopilie ambaye aliachiwa kwa dhamana na Korti Kuu, anadaiwa kuwa mnamo Novemba 4 mwaka jana, mishale ya saa 1:00 usiku, katika barabara ya Bagamoyo na Kawe, jijini Dar es Salaam, alimuua bila ya dereva wa daladala Hassan Mbonde kwa kumpiga risasi.

Wakati huohuo, kitimtim cha aina yake kimeibuka leo katika Mahakama ya Kisutu Jijini baada ya mahabusu kugoma wakitaka nao kesi zao ziendeshwe haraka kama ilivyo kesi ya Ditopile.

Kazi zote za mahakama hiyo zimesimama kuanzia saa 2 :00 asubuhi baada ya kuwasili kwa makarandinga yaliyobeba mahabusu, ambapo mahabusu hao waligoma kutelemka kwenye malori hayo.

Mahabusu hao wamegoma kutelemka kwenye malori mawili yenye namba za usajili STH 3058 na STJ 903 yaliyowaleta mahakamani hapo wakihoji kuwa inakuwaje upelelezi wa kesi inayomkabili Ditopile umewahi kukamilika na kuziacha kesi za walalahoi ambao wanaendelea kusota rumande kwa miaka kadhaa sasa.

Kufuatia mgomo huo, eneo zima la Mahakama ya Kisutu lilijaa askari kanzu, askari wa kawaida na wale wa kikosi cha kutuliza ghasia, FFU, ambao walimwagwa kwa wingi.

Hali hiyo imemlazimu Hakimu Mkuu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Bw. Sivangilwa Mwangesi kutoka nje ya mahakama kujaribu kuwashawishi mahabusu hao watelemke kwenye gari ili mahakama iendelee na shughuli zake.

Hata hivyo hakuna mahabusu aliyemsikiliza na badala yake, mahabusu hao waliendelea kushusha nyimbo za mapambio ya kilokole, wakitaka nao wahakikishiwe kuwa kesi zao zitasikilizwa haraka kama Dito.

Mpaka Gazeti hili linakwenda mitamboni, mambo yalikuwa bado mabichi kwenye viwanja vya mahakama ya Kisutu na askari wakaamua kuwarejesha mahabusu hao gerezani.

SOURCE: Alasiri
 
12-03-2007
 
Rage ajiandae kufungwa tena 2009 na kuachiwa 2011. Like I told you guys na mwanakijiji alivyosema, tunahesabu siku tu. Watu watachoka na huu upuuzi.
 
habari zaidi leo ni kuwa pamekuwepo MGOMO WA MAHABUSU walikataa kushuka kwenye makarandinga na wakabakia kuimba na kutoa laana kwa kitendo cha mwenzao ditto kesi yake ya mauaji kuendeshwa haraka ndani ya miezi miwili upelelezi umekamilika wakati wengi wao wapo mahabusu hadi miaka kumi wanasubiri upelelezi huo huo...

pamoja na askari wa FFU ,askari kanzu na mahakimu kuwaomba walishikilia msimamo kitendo kilichofanya kesi ziahirishwe leo na mahabusu kurudishwa keko na segerea...

hii ni mwanzo tu lakini kuachiwa kwa ditto na vitendo vya kesi yake ni kati ya udhalilishaji wa hali ya juu kwa idara ya mahakama tangu uhuru.....tutegemee migomo zaidi na migomo hata ya kula...........
 
TRUCKS with inmates who refused to disembark at the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar e Salaam yesterday. (Photo by Mroki Mroki)

Inmates flex muscle in Dar FAUSTINE KAPAMA
 
Naona wanachi sasa wanaanza kuelewa! Safi sana. Ombi lao ni " the same speed that was applied to Mh Dittos case nayo pia iwe applied kwao" . Common sense! Is that to much to ask.....?? wameshasota sana .....
Sijui watajibiwa nini...as usual unajua tulivyomafundi wa maneno. Come what may....what they did (mahabusu) it is commendable. Hope it has rang a bell to our leaders...
 
President J.Kikwete has to follow the example of President Pervez Musharraf of Pakistan and suspend the Attorney General Johnson Mwanyika. Dittopile has only been in police custody for just 4 months while other prisoners having similar case have been in prison now for 15 years without being sentenced or bailed.
Is this justice? This is discrimination!

” Chief Justice Iftikhar Mohammed Chaudhry has been suspended by President Pervez Musharraf. ”

Remandees protest against Ditopile`s case

2007-03-13 09:22:40
By Rosemary Mirondo
Remand prisoners from Keko and Segerea in Dar es Salaam yesterday refused to alight from a truck that usually ferries them to different courts.

They were protesting against the way the case of former Tabora regional commissioner Ukiwaona Ditopile Mzuzuri was being handled by both the Judiciary and the State authorities.

Ditopile, who is facing manslaughter charges, was released on bail last week by the High Court.

The remandees, who seemed irked by the High Court`s decision, yesterday refused to alight from the prisoners` truck - commonly known as `karandinga` - at the Kisutu Resident Magistrate?s Court.

They shouted that the Judiciary and State authorities should explain why Ditopile?s case has been given special treatment.

Some of the remand prisoners said they are facing murder charges and have been in custody for more than 15 years, waiting for investigations to be completed.

They said more than 170 remand prisoners were normally being hauled into a single `karandinga` with a carrying capacity of only 30 people, calling that a gross violation of human rights.

Complained that they usually left the prison premises at around 6.00am for the court grounds and returned around 5.00pm without eating anything or even drinking a glass of water, they called on the government to treat all remandees equally.

Normally remand prisoners from the two prisons are collected by one `karandinga` and dispatched to various court houses in the city.

Yesterday, the first stop was the Kisutu court, where the ?karandinga? arrived at 9.00 am. It was supposed to drop accused persons with pending cases there and proceed to other courts.

However, upon arrival, those supposed to drop at Kisutu refused to disembark.

They remained in the truck until 11.00am, when Kisutu Resident Magistrate in-charge Sivangiliwa Mwagesi ordered that the prison warders take them back to prison lest they fall sick because of the scorching heat.

Criminal sessions in some courts were therefore adjourned and, as they waited, the prisoners shouted:`Tunaonewa, tunaonewa,`(meaning: we are being given a raw deal).

They then asked to have an audience with Magistrate Mwagesi to know why they were not treated as fairly as Ditopile, investigations into whose case were fast-tracked.

Ditopile was arrested on November 4, last year for allegedly killing commuter bus driver Hassan Mbonde at a road junction near Lugalo in Dar es Salaam.

He was initially charged with murder, but the charge was later commuted to manslaughter.

The former RC was released on bail last Thursday amid chaos after people believed to be his relatives beat up journalists covering the event.

Efforts to get Attorney General Johnson Mwanyika to comment on the remand prisoners? ordeal failed yesterday, as his phone kept ringing without any response.
· SOURCE: GUARDIAN
 
Safi sana,kwa kweli Hii ni hatua kubwa kuelekea kupata kilicho chetu HAKI
 
Baada ya Kisutu, wazikumba pia Arusha na Mahakama Kuu

Wataka Waziri, DPP watoe tamko

http://www.uhuru.info/kitaifa.htm

Wameyaanza wenyewe sasa watayaona
 
Hakuna wanaharakati waliomwaga upupu wa tujikomboe ndani ya hayo magereza................................wakati ni huu........................saa ya kudai haki!
 
Hawa ni mahabusu ambao wanapelekewa chakula na ndugu zao ambao huongea nao hivyo habari ya Dito inaongelewa kwenye sehemu zote sidhani kama kuna upupu. Bali kitu kitakachotokea ni kwamba kuna watu watakosa kazi i.e. scapegoat. TUSUBIRI TUONE
 
Huo ndiyo uwanaharakati wenyewe nilichokuwa nikimaanisha ni kwamba waliitumia Jumapili ya kutembelewa vizuri na kuweka mikakati ,ndiyo maana unaona magari yalikuwa mawili tofauti na mahabusu walitoka magereza mawili tofauti Lakini wote walisimama kidete kwamba HASHUKI MTU,Dua hiki ni kitu kilipangwa na hakikutokea tu pale mahakamani.(Lazima kulikuwa na mtandao).
 
Naam kweli mahabusu wameamua kuonyesha msimamo.

Tatizo la tanzania yetu bado tuna watalaam wachache kusikiliza kesi lukuki zilizojaa, kisha kuna vitu nadhani we are not getting them right kama vile kupima uzito wa kesi.

Wakati umefika sasa kwa wadau wa idara ya mahakama JUDICIARY to get to grips with reality ili mambo yakae sawa.

Mfungwa anaweza kuwa kaiba kuku kisha kakaa jela miaka mitano, gharama ya kumhifadhi jela ni kubwa kuliko kosa lake!

This has nothing to do with the system ila ni kuwa jela zetu zinahitaji kuwa ni social rehabilitation centre manake kwa hali hii itafikia wakati tunapeleka watu kujifunza uhalifu mkubwa zaidi.

I support JK katika efforts zake kwenye kurekebisha hili ameweza kujionea hali halisi kwenye majela na hatua zake zimeanza kuzaa matunda, more judges have been appointed, more budget funds allocated to the judiciary naamini matatizo yatapungua.
 
Kulikoni,
I admire your optimism. You see the cup half full when the rest of us see it half empty.
 
Nimeona kwenye thread nyingine ukimkosoa Mnyika eti hajui separation of powers na ukapiga blah blah nyingi eti CHADEMA kupewa nchi n.k. wakati wewe mwenyewe unaonyesha hapa huijui hiyo separation of powers.
Hapa wewe unataka mahakama ifanyeje ikiwa kila siku visingizio ni upelelezi haujakamilika? Hatufuati sheria za ufaransa kwamba mahakama ndio inafanya upelelezi, kwetu State (polisi na ofisi ya DPP) ndio wanaofanya upelelezi sasa kunukuu maneno yako "Wakati umefika sasa kwa wadau wa idara ya mahakama JUDICIARY to get to grips with reality ili mambo yakae sawa." inawezekana vipi?
Haya maneno yako yanafaa kama ungekuwa unawaaambia Wadanganyika wa huko Lushamba. Kuteua majaji lukuki waka idara ya polisi inasuasua vilevile kutaidia nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…