Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Habari zinazoingia KLH News Studios.. zinasema kuwa Jaji Mkuu Bw. Barnabas Samatta amesikitishwa na yale yaliyotokea siku ya Alhamisi... habari zaidi kufuata..!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
2007-03-12 15:52:42
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Siku chache tu baada ya kuachiwa kwa dhamana na Korti Kuu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Kapteni Mstaafu Ditopile Mzuzuri, yuko shakani kufunguliwa kesi nyingine mpya inayohusiana na ile inayomkabili sasa ya kumuua dereva wa daladala bila ya kukusudia.
Hofu juu ya kufunguliwa upya kwa kesi hiyo ambayo sasa ingali ikiendelea Kortri Kuu inatokana na tishio linalotolewa sasa na kiongozi wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, anayedai kuwa mkuu huyo wa zamani mkoani Tabora anastahili kushitakiwa kwa `Kesi ya Mauaji` na wala siyo ile inayoendelea sasa ya \'kuua bila ya kukusudia`.
Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, Mchungaji Mtikila amesema lazima afungue kesi hiyo mapema iwezekanavyo ili kuona haki ikitendeka, huku akidai kuwa ile ya sasa siyo hasa anayostahili kukabiliwa nayo Dito.
Akasema Mtikila kuwa leo atawasiliana na jopo la mawakili wake ili ikiwezekana, kama si mchana wa leo hii, kesho asubuhi aweze kuifikisha kesi hiyo mpya haraka iwezekanavyo. `Mimi na wanaharakati wenzangu tumeamua kufungua kesi hii chini ya utaratibu wa mashtaka binafsi kwa sababu ya kutoridhishwa kwetu na namna kesi ya sasa ya Bw. Ditopile inavyoendeshwa,` akasema Mchungaji Mtikila.
Amesema hata kama mawakili wake watashindwa kutekeleza azma yake hiyo, yeye binafsi yuko tayari kutinga Mahakama Kuu, akidai kuwa anayo haki ya kikatiba kuweza kufanya hivyo.
`Mimi mwenyewe ni mwanasheria, na tena ni Mtanzania mwenye haki zote za kikatiba� ninayo haki ya kwenda mahakamani hata kama sitakuwa na wakili,` akasema, huku akiitaja Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndiyo inayompa `jeuri` hiyo.
Amesema wakati akichukua uamuzi wa kwenda mahakamani kufungua kesi upya dhidi ya Dito, amemwandikia barua Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Alfred Tibaigana, akimtaka awalinde mashahidi muhimu waliokuwepo wakati wa tukio hilo.
Katika kesi ya sasa, Ditopilie ambaye aliachiwa kwa dhamana na Korti Kuu, anadaiwa kuwa mnamo Novemba 4 mwaka jana, mishale ya saa 1:00 usiku, katika barabara ya Bagamoyo na Kawe, jijini Dar es Salaam, alimuua bila ya dereva wa daladala Hassan Mbonde kwa kumpiga risasi.
Wakati huohuo, kitimtim cha aina yake kimeibuka leo katika Mahakama ya Kisutu Jijini baada ya mahabusu kugoma wakitaka nao kesi zao ziendeshwe haraka kama ilivyo kesi ya Ditopile. Kazi zote za mahakama hiyo zimesimama kuanzia saa 2 :00 asubuhi baada ya kuwasili kwa makarandinga yaliyobeba mahabusu, ambapo mahabusu hao waligoma kutelemka kwenye malori hayo.
Mahabusu hao wamegoma kutelemka kwenye malori mawili yenye namba za usajili STH 3058 na STJ 903 yaliyowaleta mahakamani hapo wakihoji kuwa inakuwaje upelelezi wa kesi inayomkabili Ditopile umewahi kukamilika na kuziacha kesi za walalahoi ambao wanaendelea kusota rumande kwa miaka kadhaa sasa.
Kufuatia mgomo huo, eneo zima la Mahakama ya Kisutu lilijaa askari kanzu, askari wa kawaida na wale wa kikosi cha kutuliza ghasia, FFU, ambao walimwagwa kwa wingi. Hali hiyo imemlazimu Hakimu Mkuu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Bw. Sivangilwa Mwangesi kutoka nje ya mahakama kujaribu kuwashawishi mahabusu hao watelemke kwenye gari ili mahakama iendelee na shughuli zake.
Hata hivyo hakuna mahabusu aliyemsikiliza na badala yake, mahabusu hao waliendelea kushusha nyimbo za mapambio ya kilokole, wakitaka nao wahakikishiwe kuwa kesi zao zitasikilizwa haraka kama Dito.
Mpaka Gazeti hili linakwenda mitamboni, mambo yalikuwa bado mabichi kwenye viwanja vya mahakama ya Kisutu na askari wakaamua kuwarejesha mahabusu hao gerezani.
Daily News; Tuesday,March 13, 2007 @00:07
IT was a bit of a drama at the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam yesterday when over 300 inmates refused to disembark from their van from the Keko and Segerea remand prisons, demanding they talk to the police Zonal Crime Officer (ZCO).
The men were protesting delayed investigation of their cases and what they termed as favouritism in the treatment of suspects under custody. They threatened not to go back until former Tabora regional commissioner Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (58) was also taken back to custody. Ditopile was bailed out by the High Court five days ago after spending over three months in custody on a charge of manslaughter.
"We want equal justice to all. Some of us here have been languishing in remand for almost 15 years, but investigations into murder cases we are facing have not been completed to date. Why are cases involving big shots being investigated faster than those of the downtrodden?" one of the accused queried. They would not even listen to the in-charge, Senior Resident Magistrate Sivangilwa Mwangesi, who promised to forward their grievances to higher authorities.
Mr Mwangesi later said the court session could not proceed. "We have no option. Their cases will be adjourned to other dates," he said. The ZCO, Assistant Commissioner of Police Erick Ndanshao, arrived at the court a few minutes later with some 50 armed officers and riot police but the men too stuck to their ‘guns.'
Mr Ndanshao had no option but to order the men returned to custody. Mr Mwangesi somehow sympathised with the men but was not happy with the manner they presented their message. "I do not think they all have similar complaints," he said. Observers noted that the complaints by the prisoners involved two ministries - Public Safety and Security under Mr Bakari Mwapachu and Justice and Constitutional Affairs led by Dr Mary Nagu. Mr Mwapachu said he had no comment while Dr Nagu could not be reached.
NA WAANDISHI WETU
MAHABUSU mkoani Arusha wamegoma kuunga mkono wenzao wa Dar es Salaam waliogoma juzi na kuendelea na msimamo huo jana, pia wamemtaka Waziri wa Sheria na Katiba Dk. Mary Nagu kueleza ni muda gani unahitajika kukamilisha upelelezi kwa makosa ya mauaji.
Wakati hayo yakitendeka, mmoja wa mawakili wanaomtetea aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ditopile Mzuzuri amesema mahabusu wanaolalamikia kesi zao kucheleweshwa wana hoja, lakini wanakosea wanapolihusisha suala hilo na mteja wao. Jana karibu mahakama zote za Dar es Salaam hazikufanya kazi, kutokana na mahabusu zaidi ya 300 kuendelea na mgomo huku wakimtaka Waziri Dk. Mary na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutoa tamko la pamoja.
Tunamuomba waziri (Dk. Mary) atoe tamko kuhusu muda wa kufanyika upelelezi kwa kesi za mauaji, kama hatafanya hivyo, wembe ni ule ule, magari tutapanda lakini hatutashuka mpaka pale litakapotolewa tamko, walisikika wakisema mahabusu hao waliokuwa kwenye karandinga.
Mahabusu wa Dar es Salaam walianza mgomo juzi, siku chache baada ya Ditopile (58) anayekabiliwa na kosa la kuua bila ya kukusudia kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. Walikuwa wakihoji ni kwa nini upelelezi wa kesi zao unacheleweshwa.
Mahabusu hao jana pia waligoma kushuka kutoka kwenye makarandinga. Taarifa kutoka Mahakama ya Wilaya Temeke, zilisema mahabusu kutoka gereza la Keko ndio waliohudhuria mahakamani kwa siku ya jana.
Chanzo cha habari kilisema mahabusu wa gereza la Segerea waligoma kushuka walipofikishwa Temeke. Mahabusu wengine waliogoma kushuka ni wale wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ambapo waliokubali kushuka ni wale waliokuwa na kesi zilizokuwa zikienda kutolewa hukumu.
Katika mahakama za Kinondoni na Ilala, nako msimamo wa mahabusu hao ulikuwa ule ule wa kutoshuka kutoka kwenye makarandinga.
Mahabusu wakiwa kwenye makarandinga walisema wamechoka kuonewa, wakidai haiwezekani kesi ya bangi ikakaa miaka 10 bila ya upelelezi kukamilika.
Karandinga kutoka gereza la Segerea lenye namba za usajili STJ 903 lililokuwa likiongozwa na magari mawili ya polisi likiwemo la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), lilifika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu saa 4:38 asubuhi, ambapo baada ya mahabusu hao kugoma waliwarudisha gerezani.
Wakati likiingia mahakamani hapo, mahabusu hao walikuwa wakipiga kelele, baadhi wakiimba nyimbo za dini, kugonga bodi la gari na wengine wakitoa kauli tunamtaka Nagu aje ili atoe tamko. Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Eric Ndashau alisema hawezi kuzungumzia suala hilo, kwani atakayeweza kutoa tamko ni Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ambaye hakuweza kupatikana.
Kutoka Arusha mwandishi wetu Grace Msovela anaripoti kuwa, mahabusu jana waligoma kushuka katika karandinga mara baada ya kufikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Baada ya karandinga kufika mahakamani saa 4:00 asubuhi na askari kufungua mlango ili washuke, walikataa na kuanza kuimba Dito katoa nini, tuambiwe na sisi hicho alichokitoa, tuambiwe tuachiwe.
Mahabusu hao ambao idadi yao haikujulikana mara moja walikuwa
kwenye karandinga lenye namba za usajili STJ 5499 kutoka gereza la Kisongo, nje kidogo ya mji wa Arusha. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Basilio Matei alisema mgomo huo umekuja kufuatia uliofanyika juzi Dar es Salaam.
Alisema mahabusu hao walirudishwa mahabusu na mahakama haikufanyakazi kwa siku ya jana.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwanasheria wa Ditopile ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa siyo msemaji wa jopo hilo, alisema kimsingi mahabusu wana haki ya kulalamikia ucheleweshaji wa kesi zao.
Hata hivyo, alisema matukio yanayofanywa na mahabusu hao yakiwemo ya kugoma kuingia mahakamani, wakimuhusisha mteja wao hayamtendei haki.
Tunachosema wana haki ya kulalamika lakini siyo kumlalamikia Ditopile kwa sababu wengi wamewahi kupewa dhamana katika mashitaka kama haya, alisema mwanasheria huyo.
Huo ndiyo uwanaharakati wenyewe nilichokuwa nikimaanisha ni kwamba waliitumia Jumapili ya kutembelewa vizuri na kuweka mikakati ,ndiyo maana unaona magari yalikuwa mawili tofauti na mahabusu walitoka magereza mawili tofauti Lakini wote walisimama kidete kwamba HASHUKI MTU,Dua hiki ni kitu kilipangwa na hakikutokea tu pale mahakamani.(Lazima kulikuwa na mtandao).Hawa ni mahabusu ambao wanapelekewa chakula na ndugu zao ambao huongea nao hivyo habari ya Dito inaongelewa kwenye sehemu zote sidhani kama kuna upupu. Bali kitu kitakachotokea ni kwamba kuna watu watakosa kazi i.e. scapegoat. TUSUBIRI TUONE
Naam kweli mahabusu wameamua kuonyesha msimamo.
Tatizo la tanzania yetu bado tuna watalaam wachache kusikiliza kesi lukuki zilizojaa, kisha kuna vitu nadhani we are not getting them right kama vile kupima uzito wa kesi.
Wakati umefika sasa kwa wadau wa idara ya mahakama JUDICIARY to get to grips with reality ili mambo yakae sawa.
Mfungwa anaweza kuwa kaiba kuku kisha kakaa jela miaka mitano, gharama ya kumhifadhi jela ni kubwa kuliko kosa lake!
This has nothing to do with the system ila ni kuwa jela zetu zinahitaji kuwa ni social rehabilitation centre manake kwa hali hii itafikia wakati tunapeleka watu kujifunza uhalifu mkubwa zaidi.
I support JK katika efforts zake kwenye kurekebisha hili ameweza kujionea hali halisi kwenye majela na hatua zake zimeanza kuzaa matunda, more judges have been appointed, more budget funds allocated to the judiciary naamini matatizo yatapungua.