Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maisha yangu yote nilijua kuwa kosa la mauaji yawe ya kukusudia au la halina dhamana...sasa wale ndugu zetu ambao wanasota kwa miaka 12 au zaidi kabla ya kuachiwa kwa kukosa ushahidi inakuwaje?
Kwenu mlioko Bongo hebu tupasheni hii habari nasikia Ditopile kaachiwa kwa dhamana na anatinga nje ya Keko hivi sasa.
Ditto ameachiwa leo kwa dhamana; tayari iko hewani kwenye news
Ditto ameachiwa leo kwa dhamana; tayari iko hewani kwenye news
Toka tupate uhuru hadi leo nipe mfano wa mtuhumiwa yeyote wa kesi ya mauaji amabaye kesi yake na jarida lake limewahi kupelekwa kwa mkurugenzi wa mashitaka kwa kipindi kifupi kama cha ditto?ni mtuhumiwa gani wa kosa kama la Ditto ambaye alishawahi kuomba dhamana na akapewa hata kwa masharti kama ya Ditto na akashindwa mwenyewe?Ndugu Ditto hajatolewa huru kama baadhi wanavyodai, shitaka lake lilibadilishwa na kuwa ni KUUA BILA KUKUSUDIA kulingana na ushahidi aliotoa na nature ya shitaka hilo ni kuwa anaweza kupata dhamana.
Ameshakaa ndani kwa miezi minne sasa na leo ameachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000 na mahakama ilikataa ombi kuwa aachiwe eti kwa vile ni mtu maarufu, waliamua kwamba hiyo sio bond enough. Amesalimisha pasi yake ya kusafiria na kesi inaendelea.
Hizi speculations za nini?!!
Kama nilivyowahi kueleza hapo jana kuwa sheria kuchukua mkondo wake sio lazima underdog washinde ingawa najua huwa kuna sensation sana iwapo mtu wa hivyo akishinda.
Sasa bado kesi inaendelea leo BBC wamevurunda in my view wametoa text ya mtu akisema ''najua wewe Ditto ni mtu mzuri na utatoka tu'' kuna hatari ya contempt of court hapa....
Kesi inaendelea YETU MACHO!!