Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

OLE,
Unajua ukiunganisha topic zikipandiana zinakuwa zinaboa sana, nakushauri iache hapa hapa, topic ikiwa mpya "fresh" ina raha yake kuliko ikichakaa !! naomba kutoa hoja !!
 
Ndugu Ditto hajatolewa huru kama baadhi wanavyodai, shitaka lake lilibadilishwa na kuwa ni KUUA BILA KUKUSUDIA kulingana na ushahidi aliotoa na nature ya shitaka hilo ni kuwa anaweza kupata dhamana.

Ameshakaa ndani kwa miezi minne sasa na leo ameachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000 na mahakama ilikataa ombi kuwa aachiwe eti kwa vile ni mtu maarufu, waliamua kwamba hiyo sio bond enough. Amesalimisha pasi yake ya kusafiria na kesi inaendelea.

Hizi speculations za nini?!!

Kama nilivyowahi kueleza hapo jana kuwa sheria kuchukua mkondo wake sio lazima underdog washinde ingawa najua huwa kuna sensation sana iwapo mtu wa hivyo akishinda.

Sasa bado kesi inaendelea leo BBC wamevurunda in my view wametoa text ya mtu akisema ''najua wewe Ditto ni mtu mzuri na utatoka tu'' kuna hatari ya contempt of court hapa....

Kesi inaendelea YETU MACHO!!

Hongera Kulikoni ndio Tanzania yetu ina sheria kwa kina Dito na Kina Mwamwindi sheria tofauti.
 
OLE,
Unajua ukiunganisha topic zikipandiana zinakuwa zinaboa sana, nakushauri iache hapa hapa, topic ikiwa mpya "fresh" ina raha yake kuliko ikichakaa !! naomba kutoa hoja !!
Ndugu zangu
Topic zimekuwa nyingi kwanini zile ambazo ni muendelezo wa tukio hilohilo zisiendelee.
 
Kakalende,
Naona Kulikoni bado anabisha. Hata baada ya Radio Tanzania kutangaza kwenye habari zake za saa mbili usiku.
 
http://www.mwananchi.co.tz/mwananchisite/Mwananchi/Habari/Habari0.asp

Mahakama yamwachia Ditopile nduguze wazusha vurugu

Na Tausi Ally

WAKATI Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ameachiwa kwa dhamana, ndugu zake wamefanya fujo na kuwapiga waandishi wa habari katika Mahakama Kuu Dar es Salaam jana.

Dhamana hiyo ilitolewa saa 7:45 mchana na Jaji wa Mahakama Kuu, Augustino Mwarija, baada ya upande wa utetezi kuwasilisha ombi la dhamana mahakamani.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Mwarija, alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, ameona hakuna kipingamizi cha kutoa dhamana hiyo kwa kuwa kosa aliloshitakiwa nalo mtuhumiwa la kuua bila kukusudia, linastahili dhamana.

Awali, mawakili wanaomtetea Ditopile wakiongozwa na Profesa Jwani Mwakyusa, waliiomba mahakama imuachie huru kwa dhamana mteja wao kwa maelezo kuwa hawezi kuruka dhamana na kwamba anaweza kujidhamini mwenyewe na akiwa huru atapata muda wa kutosha wa kujiandaa kwa utetezi.

Upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Vicent Tango, ulieleza kuwa hauna pingamizi la dhamana kwa kuwa kosa hilo linadhaminika.

Jaji Mwarija alikataa hoja ya mawakili wa utetezi kuwa mtuhumiwa anaweza kujidhamini mwenyewe na badala yake akautaka upande huo kuandaa wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Sh20 milioni kila mmoja, akiwamo Ditopile mwenyewe ambaye naye alitakiwa kusaini bondi ya kiasi hicho cha fedha.

Mbali na masharti hayo, Jaji Mwarija pia alimtaka Ditopile kuwasilisha hati za kusafiria kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na asitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam bila kibali cha Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Ditopile alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 2.54 asubuhi akiwa amevalia suruali nyeusi na shati la mistari ya kijivu na mieusi na kofia yake aina ya pama yenye rangi nyeusi iliyofunika uso wake pamoja na miwani.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida, mara baada ya kufika mahakamani hapo, kundi la skari polisi zaidi ya 10 waliokuwa wakimlinda, walimuongoza kuingia ndani ya mahakama kupitia mlango unaotumiwa na majaji, kitendo ambacho si cha kawaida kwa watuhumiwa.

Hali hiyo iliwashangaza watu wengi akiwemo Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Prophir Lyimo, aliyehoji kitendo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lyimo alisema kitendo hicho cha kumpitisha mtuhumiwa katika mlango wa majaji kimeikera mahakama na hawakufarahishwa nacho.

"Kitendo hiki si cha kawaida na hakijawahi kutokea, askari hao hawajaruhusiwa kumpitisha mtuhumiwa huyo huko na wala hawajawahi kuruhusiwa kufanya hivyo," alisema Lyimo kwa masikitiko.

Alisema kutokana na kitendo hicho, amewasiliana na Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Alfred Tibaigana, ili afuatilie suala hilo na kwamba ameahidi kufanya uchunguzi.

Hata mlinzi aliyekuwepo katika mlango wa majaji, alisikika akilalamika kwamba alipigwa kikumbo na askari hao waliokuwa wakimpitisha Ditopile, hivyo ilimbidi akae pembeni, na kwamba anahofia kupoteza kazi kutokana na kitendo kwani tayari alikuwa ametakiwa kuandika barua ya kujieleza.

Kama hiyo haitoshi, wakati mtuhumiwa huyo akiingizwa katika mahakama ya wazi namba moja, askari kwa kushirikiana na ndugu wa mtuhumiwa walianza kupambana na waandishi wa habari hasa wapiga picha, wakitaka kuwanyang'anya kamera ili wasiweze kumpiga mpicha Ditopile.

Ndani ya mahakama hiyo ya wazi, kulikuwa kumefurika watuambao kati yao walikuwamo familia ya Ditopile, makarani wa mahakama ambao waliacha shughuli zao, waandishi wa habari na wananchi wa kawaida waliotaka kujua hatma ya ombi la dhamana la mtuhumiwa huyo.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Jaji Mwarija kutoa dhamana kwani wakati mtuhumiwa akitoka mahakamani kurudi nyumbani kwake majira ya saa 8.01 mchana, ndugu zake walianza vituko vya kuwafanyia vurugu waandishi wa habari ili wasiweze kuona namna mtuhumiwa huyo anavyoondoka katika eneo la mahakama.

Watu hao walianza kushika kamera ili picha zisipigwe, kuwarushia ngumi, mateke na kutoa lugha chafu kwa waandishi wa habari, huku wengine wakiwa wamemzunguka mtuhumiwa na kumfunika kwa kanga kiasi cha kufanya asionekane kabisa kabla ya kuingia kwenye gari ndogo aina ya Toyota balloon namba T 723 AFD na kuondoka naye.

Katika sakata hilo lililodumu kwa zaidi ya dakika 10, mwandishi mmoja alijeruhiwa kwa kuchanika mdomoni huku wengine wakiumizwa sehemu mbalimbali za mwili.

Katika hali ya kushangaza, pamoja na kuwapo kwa askari wengi katika eneo hilo, hakuna askari hata mmoja aliyechukuwa hatua ya kuzuia vitendo hivyo vya ndugu zake Ditopile na badala yake walisimama pembeni na kuangalia kama sinema.

Hii ni mara ya pili kwa watu hao kufanya vurugu mahakamani, kwani hivi karibuni wakati kesi hiyo ikiwa bado katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu, walifanya vurugu kubwa ambayo ililaaniwa na waendesha mashitaka.

Mara ya mwisho kesi hiyo ilipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, upande wa mashitaka ulitoa maelezo ya mashahidi 23 wa upande huo.

Katika maelezo ya mashahidi hao ambao watasimama dhidi ya Ditopile wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, walieleza namna tukio zima la mauaji ya dereva wa daladala, Hassan Mbonde lilivyotokea.

Kwa upande wake, Ditopile kupitia maelezo yake yalivyoandikwa na ASP Sabasi na kusomwa mahakani hapo na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Germanus Mhume mbele ya Hakimu Michael Luguru, naye alieleza mazingira ya tukio hilo lilivyotokea kabla ya kujisalimisha polisi.

Ditopile alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Novemba 6 mwaka jana akikabiliwa na tuhuma za kumuua dereva wa daladala Hassan Mbonde.

Anadaiwa kuwa Novemba 4, mwaka jana, majira ya saa 1.00 usiku, katika eneo la njia panda ya Bagamoyo na Kawe wilayani Kinondoni Ditopile alimuua bila ya kukusudia dereva huyo wa daladala.
 
Mambo tuliyoyasema hapo awali yanaonekana wazi sasa.Kila kitu kinapindwa,na naahidi hapa kuwa huyu Mh.Muuaji atapewa kifungo ambacho kitafuatiwa na msamaha wa Rais atakaoutoa 2010 atakapomaliza muda wake wa Urais.Haya yanayotokea sasa yalikwishajulikana,kile kitendo cha kumbadilishia mashitaka kutoka KUUA na kuwa KUUA BILA YA KUKUSUDIA,kilichofanywa na Bw.Kaduma (angalia jina hilo) ndio kimemfanya Bw.Ukiwaona Mwinshehe akalale nyumbani.Eeeh Mungu Mrehemu Mbonde!
 
Kama mambo ni hivi, Ditopile Aachiwe!!!

Na. M. M. Mwanakijiji
Hivi majuzi nilikuwa namtambia rafiki yangu wa Kiganda kuwa Tanzania ukilinganisha na nchi nyingi za kiafrika na hata sehemu nyingine duniani ina mahakama huru zaidi na zinazoheshimika. Niliendelea kutamba kuwa kitendo kama kilichotokea huko Uganda ambapo askari waliingia kwenye maeneo ya mahakama na kuwakamata watu walioachiwa huru hakiwezi kutokea Tanzania. Kumbe nisichokijua kilikuwa ni kama 'usiku wa kiza'. Waswahili walisema "usimtukane mamba kabla hujavuka mto" na ndio hao hao waliosema "usitukane wakunga na uzazi ungalipo". Hata kabla ya wiki kwisha nikajikuta nimeumbuliwa na nchi yangu, kwani kile ambacho sikuwaza kinaweza kutokea Tanzania kimetokea na kuniacha nimepigwa na butwaa huku nimeyauma meno yangu kwa hasira. Jeshi la Polisi limeingia mahakamani kwa nguvu.

Mazingaombwe na wale wafanyao mazingaombwe! Siku ya Alhamisi kimefanyika kitendo kwenye Mahakama Kuu ambacho kama hakitakemewa na waliohusika kuchukuliwa hatua kali kinaashiria kubomoka kwa utawala wa sheria na utafutwaji wa haki katika mahakama za Tanzania. Na kitendo hicho kinatishia uhuru wa Mahakama, uhuru wa vyombo vya habari, na usawa wa raia wote mbele ya sheria.

Wakati polisi wanamfikisha mtuhumiwa wa kesi ya mauaji Bw. Ditopile Mzuzuri kwenye mahakama kuu jijini Dar-es-Salaam, bila sababu ya msingi waliamua kumpitisha mtuhumiwa huyo kuingia kwenye mahakama hiyo kwa kupitia mlango unaotumiwa na majaji. Kwa wale ambao hawajui taratibu za mahakama nyingi (siyo Tanzania peke yake hata sehemu nyingine duniani), majaji wanapokuja kazini au kwa shughuli mbalimbali mahakamani hapo kuna mlango ambao wao pekee wanapitia na mlango huo mara nyingi hautumiwi na watu wengine wakiwamo wafanyakazi wengine wa chombo hicho. Hata mawikili hawaruhusiwi kupita huko. Siyo tu kwa ajili ya heshima ya cheo chao bali pia kwa ajili ya usalama wao na uhuru wa chombo hicho

Lakini kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania ambayo naweza kuikumbuka kwa haraka maaskari wa jeshi la Polisi walitumia ubavu (pamoja na kumpiga kikumbo mlinzi wa Mahakama hiyo) na kulazimisha mtuhumiwa huyo kuingizwa mahakamani hapo kwa kupitia mlango huo wa majaji. Kitendo hicho kama kilivyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kiliwashangaza watu wengi wakiwamo wafanyakazi wa Mahakama hiyo. Licha ya polisi kuingia kwa nguvu mahakamani hapo waandishi wa habari nao walishambuliwa na maafisa hao na baadhi yao vyombo vyao vya kazi kuharibiwa na polisi hao na wanafamilia ya Dito na hivyo wandishi kunyimwa nafasi ya kufanya kazi zao kama kawaida. Vitendo hivyo siyo tu vinatishia uhuru wa mahakama bali pia uhuru wa vyombo vya habari wa kutafuta, kupata na kutoa habari.

Mshangao wa kitendo hicho ulioneshwa wazi na Msajili wa Mahakama hiyo bw. Prophi Lyimo ambaye alinukuliwa akisema kuwa "Kwa kweli tumekasirika sana, sijuwi walipewa nini, maana katika hali ya kawaida hawawezi kufanya hivyo. Haijawahi kutokea hapa, nimemwambia Tibaigana awabane polisi wake na wamueleze kwa nini wamefanya hivyo". Katika vyombo vya habari haijawekwa wazi kama askari waliompitisha Ditopile kupitia mlango huo walikuwa na silaha ama la. Kama walikuwa na silaha kitendo hicho kinakuwa na uzito ambao maneno ya karatasi hayatoshi kuelezea. Bila ya shaka kuna sababu iliyowafanya askari hao kufanya kitendo hicho na hapa nitashuku tu sababu hizo hadi zitakaposemwa hadharani.

Inawezekana kabisa kuwa maafisa wa ngazi za chini wa polisi walifanya kitendo hicho baada ya kupewa amri na "mkubwa wao" kumpitisha Mtuhumiwa huyo wa mauaji kupitia mlango huo wa majaji. Kama ni kweli, "mkubwa" huyo ni lazima ajulikane na hatua za kinidhamu (ikiwemo kufukuzwa kazi, kushushwa cheo n.k) zichukuliwe dhidi yake. Afisa yeyote wa jeshi la polisi ambaye hajui uzito wa kuingia kwenye chumba cha majaji kwa nguvu na kupitisha watuhumiwa huko wakati kuna milango iliyopo kwa ajili ya kazi hizo hastahili kuvaa nembo ya jeshi letu! Askari wa chini waliotekeleza amri hiyo ambayo si halali ni lazima nao wachukuliwe hatua kali. Maaskari hawa hawawezi kujitetea kuwa "walikuwa wanafuata amri tu". Kutii amri ambayo siyo halali ni kosa!! Rais kwa mfano, hawezi akatoka nje pale Ikulu na kumuamuru askari ampigie mtu risasi kwa vile Rais amejisikia hivyo na askari huyo akafanya hivyo!! Siyo kila amri inayotolewa na mkubwa ni halali! Maafisa wetu ni lazima (kupitia tukio hili) wafundishwe wazi kuwa "mkubwa" akikuamuru kufanya jambo ambalo unajua au unahisi ni kinyume na sheria unayo haki ya kukataa kulitekeleza hata kama itatishia ajira yako au kumuudhi mkubwa huyo. Hadi pale utakapohakikishiwa usheria wa amri hiyo. Endapo maaskari hawawezi kukataa kutekeleza amri isiyo halali basi Watanzania tuna matatizo kwani viongozi wanaweza kuwaamuru mamluki hao kufanya lolote lile bila kujali matokeo yake, kwani "bosi" kasema.!! Hili katika Tanzania ya leo halikubaliki, tunalipinga, na tunalilaani kwa uzito wote unaostahili.

Inawezekana pia kuwa maafisa wa polisi walifanya kitendo hicho ili kuonesha "ni nani" anayeletwa mahakamani hapo na ni jinsi gani mtu huyo ni tofauti na washtakiwa wengine. Ni wazi kuwa kesi ya Ditopile ni mojawapo ya kesi chache zenye makosa makubwa ambayo kiongozi wa serikali anaweza kuhusishwa nacho, lakini kesi shitaka analokabiliwa nalo siyo ngeni kwenye mahakama zetu. Huko nyuma kuna viongozi walioshtakiwa kwa kuhujuma uchumi, ubadhirifu, wizi n.k lakini hili la kiongozi kutuhumiwa kumuua mtu ni jipya na hasa jinsi mauaji hayo yanavyodaiwa kufanyika. Mara zote ambapo Bw. Dito amekuwa akiletwa mahakamani kuanzia kule Kisutu hadi Mahakamani vimbwanga hufuatana naye. Hiki cha sasa kimepita hayo yote! Polisi hawana sababu yoyote ya kuionesha mahakamani "uzito" wa mtuhumiwa kwani Ditopile anajulikana na jina lake limetangaa. Lakini, waliofanya kitendo hicho inawezekana kabisa walitaka kutuma ujumbe kuwa "Tutampeleka tunakotaka sisi, kwa wakati tunaotaka sisi, na hakuna anayeweza kutuzuia" Kama hilo ndilo lilikuwa mawazoni mwa maafisa hawa basi nalo ni sababu ya kumwajibisha afisa aliyesimamia zoezi hilo, na kama mkuu wa polisi wa Kanda alikuwa anaujuzi wa kitendo hicho na akashindwa kukizuia na yeye hana budi kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kuandika barua ya kujiuzulu. Kitendo hiki inawezekana kimechukua mistari michache kwenye vyombo vya habari lakini uzito wake unaweza kujaza maktaba!

Sababu nyingine ambayo naombea isiwe ya kweli inatokana na hiyo ya hapo juu. Maafisa wa polisi kutokana na amri waliyopewa au maelekezo waliyopewa waliamua kuitishia mahakama na hususan jaji au majaji ambayo wanaweza kujikuta wakisikiliza kesi hii. Hivi karibuni huko Uganda jambo kama hili limesababisha mgomo wa Majaji na wafanyakazi wa mahakama baada ya polisi kuingia mahakamani kwa mabavu na kuwakamata watu walioachiwa huru na mahakama hiyo ya Uganda. Hapo Tanzania , endapo jambo kama litavumiliwa au kujaribu kupuuzwa litajenga jaribio la chombo cha dola kuitisha mahakama ili isifanye kazi zake za kugawa haki kwa uhuru bila upendeleo. Katika mahakama zetu kuna watu wengi ambao wamewahi kushitakiwa kwa tuhuma nzito zaidi ya hiyo ya Ditopile, na hakuna siku ambapo washtakiwa waliingizwa kupitia mlango wa majaji, siyo wakati wa kesi ile ya uhaini au wa kesi ya Kiula na wenzake. Jaribio hili la kuitisha mahakama natumaini limeshindwa na halitatokea tena.

Hata kama mojawapo ya sababu hizo hapo juu ni ya kweli (ama zote) serikali ni lazima itamke mara moja kukikana kitendo hicho na kuahidi kuchukua hatua za kinidhamu siyo kuunda tume ya uchunguzi! Ingawa Msajili wa Mahakama ametamka kutofurahishwa kwake na kitendo hicho, Jaji Mkuu Bw. Barnabas Samatta ni lazima atamke na kukikemea kitendo hicho na aiambie serikali kuwa endapo jambo kama hilo au hata linalokaribiana na hilo kwa mbali litafanyika, waliohusika watatiwa mbaroni kwa kudharau mahakama na Mahakama yake haiwezi kukubali kuingiliwa na chombo kingine cha serikali hata kama kesi inamhusu mtu mashuhuri kiasi gani.

Zaidi ya yote, kwa vile kesi inaonekana kuwa na mvuto wa hisia nyingi hususan upande wa wanafamilia ya Ditopile ambao wamejaa jijini Dar-es-Salaam, Jaji Mkuu anaweza kuamuru kesi hiyo kuhamishiwa katika mahakama ya Kanda na kupelekwa mkoa mwingine kwenye matawi ya Mahakama hiyo ambapo inaweza kusikilizwa kwa uhuru bila kuvutia watu wenye hisia kali kwani siyo tu inatishia usalama wa maafisa wa mahakama bali pia raia wanaokuja mahakamani kwa kesi nyingine na watu wengine ambao kwa sababu moja ama nyingine wanaweza kujikuta wapo hapo mahakamani.

Vile vile, Jaji Mkuu ni lazima ahakikishe kuwa kama wale walioapishwa kulinda Katiba (maafisa wa Polisi) wameshindwa kazi hiyo, aamuru kuanzia sasa maafisa wa Magereza kumleta Mshitakiwa mahakama na kumuingiza mahakamani na kutoa ulinzi mahakamani hapo badala ya Polisi na ikibidi aombe Rais aidhinishe kikosi cha Polisi wa Jeshi kulinda mahakama hiyo kutoka kwa polisi wasiojua wajibu wao. Lililotekea mahakamani hapo jana si jambo dogo kwa kipimo chochote kile.

Ni matumaini ya wapenda demokrasia wote na wale wanaoelewa mtengano wa madaraka kuwa kitendo hicho (au kifananacho na hicho) hakitarudiwa tena, na endapo kitendo kama hicho kitarudiwa, basi Mahakama iamue kumuachia Ditopile huru kuliko kuvunja vunja na kusagasaga kama kwenye kinu uhuru wa mahakama zetu na hivyo kuharibu mchakato mzima wa utafutaji wa haki!
 
kama kitendo hicho kimewaudhi majaji kikweli....there could be backfiring! otherwise ni mazingaombwe na ujuha mtupu.

BTW: JK awaombe wazungu watuletee askari wanaoweza kazi yao vizuri.
 
Kuna tetesi kwamba huyu Ditto siku zote amekuwa akiishi nyumbani kwake na mazingaombwe kuchukua nafasi siku ya kuja mahakamani.Kuna kila sababu ya kuamini haya maana hata gari lake limekuwa lake tu kuja na kurudi Keko. Hivi kwa vurugu zote hizi tusiamini kwamba CCM na JK wanatuchezea watanzania ?
 
Ditopile finally out on bail
FAUSTINE KAPAMA
Daily News; Friday,March 09, 2007 @00:07

resize_image1.php

FORMER Tabora Regional Commissioner Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (see arrow) hides his face after being released on bail by the High Court in Dar es Salaam yesterday. Others in the picture are relatives and police officers.

THE High Court in Dar es Salaam yesterday released on a 20m/- bail former Tabora Regional Commissioner (RC) Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (58), who is charged with the manslaughter of commuter bus driver Hassan Mbonde (33) some four months ago.

Ditopile's release was greeted by a breakdown in order after some people, who are believed to be his relatives, attempted to block press photographers from doing their work.

Some journalists and press photographers traded blows as policemen who were at the court simply watched without taking any action.

Justice Augustine Mwarija grated bail to Ditopile on several conditions that included signing a bond of 20m/- with two sureties of the like sum. The sureties required approval by the District Registrar of the High Court, Dar es Salaam Zone.

The judge also ordered the then RC to surrender his passport and other travel documents to the Zonal Crime Officer and instructed him not to leave the city without reporting to the court's registrar.

Immediately after approval of the sureties, police officials and other relatives surrounded him as he was going out of the court's building to block press photographers from doing their work.

The District Registrar, Mr Prophir Lyimo, told reporters later that they have reported the matter to the relevant authorities. Mr Lyimo said another complaint was that Ditopile was given VIP treatment by police who allowed him to enter the court's building through the door reserved for judges.

"We have not been satisfied by the conduct of these police officers," the registrar said. Ditople was brought to the court under tight security at around 8.50am in a police salon car.

The police who were escorting the accused allegedly pushed away a court security guard, identified as Kulwa Mkoka, when she attempted to block them from entering the building through the door reserved for High Court judges.

Prof Jwani Mwaikusa, assisted by Dr Ringo Tenga and Mr Cuthbert Tenga, presented their submissions to convince the court to release the accused on bail. State Attorney Vincent Tango raised no objection to the bail application but cautioned the court not to bail the accused simply because he was a big shot.
 
Mk, nimekuwa nasoma habari hapa siku zote na kwa kweli nakupongeza kwa juhudi zako kudai haki na kuleta maendeleo Tanzania.

kwenye hili suala ndugu yangu punguza jazba, wenye mpini hii ni issue yao kubwa sana. Utaisaidia nchi yako kwenye mambo mengi lakini ningekuwa wewe hili suala ningeliacha kama lilivyo.

naomba nisijibiwe kuhusu haki nk. Naelewa yote lakini swahiba wake huyo mtu ndio karuhusu dito kuwa mtaani na kesi yote kutoendelea popote.

Mungu ibariki Tanzania
 
Ditopile apewa dhamana, ngumi zafumuka Kortini

Basil Msongo

HabariLeo; Friday,March 09, 2007 @00:07

resize_image1.php

Ndugu, jamaa na wapambe wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile-Mzuzuri wakimkinga asipigwe picha nje ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam, baada ya kupewa dhamana jana. Baadaye waliwashambulia waandishi wa habari. (Picha na Mroki Mroki).

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, jana iligeuka uwanja wa mapigano baada ya ndugu na jamaa wa Ukiwaona Ditopile Mzuzuri kuwashambulia waandishi wa habari kwa ngumi na mateke wakiwazuia wasimpige picha kabla ya kupanda kizimbani na baada ya kudhaminiwa.

Mapigano yalikuwa makali zaidi saa 8.56 mchana ndani ya jengo la Mahakama hiyo, wakati Ditopile akitoka nje kwenda kupanda gari huku wapambe wake wakiwa wamemfunika ili asipigwe picha.

Kabla ya tukio hilo, saa 4.52 asubuhi ndugu na jamaa hao walizua tafrani jirani na chumba namba moja cha Mahakama hiyo walipowazuia waandishi wa habari kupiga picha wakati Ditopile akienda kupanda kizimbani.

Baada ya mapigano ya mchana, Ditopile alipanda gari dogo aina ya Toyota, maarufu kwa jina la ‘baloon’, namba T 723 AFD na kuondoka akiwa anasindikizwa na gari la Polisi namba T 212 AMV.

Mtuhumiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya watu wawili na yeye kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh milioni 20 kila mmoja, lakini alitakiwa kupeleka hati yake ya kusafiria na hatakiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kutoa taarifa Mahakama Kuu.

Jaji Augustino Mwarija alikubali maombi ya dhamana kwa maelezo kwamba hakuona sababu ya kumkatalia ombi hilo kwa kuwa mtuhumiwa wa kosa la kuua bila kukusudia ana haki ya kupata dhamana. HabariLeo lilikuwa gazeti la kwanza nchini kuandika habari kwamba Ditopile angeshitakiwa kwa kuua bila kukusudia badala ya mashitaka ya mauaji na angelipewa dhamana.

Awali, mmoja wa mawakili wa Ditopile, Prof. Juan Mwaikusa alitumia takriban dakika 50 kuomba dhamana hiyo kwa kutoa hoja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusema kuwa mtuhumiwa alionyesha uaminifu tangu siku lilipotokea tukio la mauaji, Novemba 4 mwaka jana kwa kuwa siku hiyo hiyo usiku alijisalimisha Polisi na akawa rumande mpaka jana.

Prof. Mwaikusa aliiambia Mahakama kuwa, mtuhumiwa anahitaji dhamana ili akajiandae kujibu tuhuma ikiwa ni pamoja na kupata ushauri muafaka wa kisheria kuhusiana na tuhuma zinazomkabili tangu Februari 15 kwa kuwa awali Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi Kisutu ilimsomea mashitaka ya mauaji.

Wakimuingiza mahakamani hapo asubuhi, Polisi walitumia nguvu kumpitisha Ditopile katika lango la kuingilia majaji wa Mahakama Kuu badala ya lango la kawaida kama watuhumiwa wengine. Msajili wa Mahakama Kuu, Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Prophir Lyimo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Lyimo alisema alimpigia simu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana kumfahamisha achunguze na kuwachukulia hatua wahusika kwa kuwa watuhumiwa hawaruhusiwi kupita kwenye lango hilo.

Akizungumzia suala hilo Tibaigana alikiri kupokea simu kutoka kwa Msajili wa Mahakama Mkuu kanda ya Dar es Salaam ikimueleza kuwa watu wengi wamefurika mahakamani hapo kwa hiyo wanahofia inaweza kutokea vurugu kama iliyotokea Kisutu kipindi cha nyuma.

“Polisi wangu hawajafanya fujo ila walimpitisha mtuhumiwa katika mlango wa dharura kutokana na umati wa watu mahakamani hapo... “Mimi nilipokea taarifa ya kuwapo kwa watu wengi eneo hilo tu na nilimtuma msaidizi wangu na katika taarifa aliyoniletea hakuna mahali paliposema Polisi hao wamepiga waandishi wala kufanya vurugu yoyote zaidi ya kutumia mlango wa dharura kitu ambacho ni kizuri kwa usalama,” alisisitiza Tibaigana.
 
Kama kumbukumbu yangu iko sawasawa, siku ya krismas mwaka 1971, mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Wilbert Kreluu alimfuata jamaa mmoja aliyekuwa anaitwa Mwamwindi na kumuuliza kwa nini alikuwa hataki kuhamia kwenye kijiji cha Ujamaa. Mwamwindi akamwambia kuwa hawezi kuhama pale kwake kwa sababu za kihistoria kuwa kulikuwa na makaburi ya wazazi na mababu zake na
asingeweza kuyaacha bila uangalizi. Dr. Kreluu akamjibu kitu kama vile "....yaani hayo makaburi ya watu waliokwisha kufa ndiyo yanayokufanya uwe na mawazo ya kibepari." Mwamwindi kusikia vile aka-swear kwa kihehe akisema "Swea" kwa hasira na kusema "yaani unadharau wazazi wangu kwa eti kwa vile wameshakufa!!." Bila simile akavuta gobore lake na kumfyatuliwa Mwamwindi nadhani risasi ya kifuani vile na kumwua papo hapo. Baada ya tukio lile akachukua maiti ya Dr. Kreluu na kuipeleka polisi kwa gari la Mkuu wa Mkoa lililokuwa na namba "RC IR." Kisheria, kesi ile ingeweza kabisa kuwa ya kuua bila kukusidia kwa sababu ya provocation hasa ukizingatia kuwa Dr. Kreluu alimfuata Mwamwindi nyumbani kwake tena siku ya sikukuu bila kuwa na dereva wala mlinzi. Lakini Mwamwindi alikaa ndani kwa karibu miaka mitatu na baadaye kunyongwa kichinichini; ni kati ya watu wachache sana walionyongwa wakati wa utawala Nyerere.

Kila nikijaribu kulinganisha kosa alilolifanya raia wa kawaida (Mwamwindi) kumwua Mkuu wa Mkoa (Kreluu) aliyemchokoza kwa makusudi na kosa la Mkuu wa Mkoa (Dito) kumwua raia wa kawaida (Mbonde) kwa kumgongea gari na jinsi serikali inavyochukulia matukio hayo kwa uzito tofauti nashindwa kabisa kuelewa maane yake.

Mungu Ibariki Tanzania,
Wabariki Viongozi Wake,....
 
Nakuunga mkono 101% kwa hii comment. Tatizo lipo wapi? Mahakama?
 
Kichuguu chukua 7
 
Utawala wa sheria na haki za binadamu hapa hakuna. Hivi hapa Tanzania nani hasa yuko juu ya sheria na nani anabaki kuw chini yake? Ndugu wa Dito wanawapiga waandishi wa habaeri bila polisi kuingilia kati?

Wanasheria mliobobea, hao mawakili wanaomtetea Dito wanasimama vipi ktk taaluma yenu? Ni mabingwa, maamuma au wanafiki? (Mkono na kampuni yake wana mengi ya uozo migongoni mwao - ya IPTL).

Mtuhumiwa anapitishwa mlango wa majaji!

Heko Kichuguu, posting yako inamguso wa kizalendfo mno - keep it up!!
 
Mk, nimekuwa nasoma habari hapa siku zote na kwa kweli nakupongeza kwa juhudi zako kudai haki na kuleta maendeleo Tanzania.

kwenye hili suala ndugu yangu punguza jazba, wenye mpini hii ni issue yao kubwa sana. Utaisaidia nchi yako kwenye mambo mengi lakini ningekuwa wewe hili suala ningeliacha kama lilivyo.

naomba nisijibiwe kuhusu haki nk. Naelewa yote lakini swahiba wake huyo mtu ndio karuhusu dito kuwa mtaani na kesi yote kutoendelea popote.

Mungu ibariki Tanzania
Dar-es-salaam umeingia na unajaribu kutisha wanaforum? kwa taarifa yako slogan ya hapa ni "WHERE WE DARE TALK OPENLY".

Hapa ni mawe tu, ataendelea kuandikwa hata kama yuko nje kwa dhamana.
 
maybe we could get expert lawyers from norway kama raisi alivyoomba expert lawyers wa kuandika mikataba ya madini
 
Kama mambo ni hivi, Ditopile Aachiwe!!!

Na. M. M. Mwanakijiji
Hivi majuzi nilikuwa namtambia rafiki yangu wa Kiganda kuwa Tanzania ukilinganisha na nchi nyingi za kiafrika na hata sehemu nyingine duniani ina mahakama huru zaidi na zinazoheshimika. Niliendelea kutamba kuwa kitendo kama kilichotokea huko Uganda ambapo askari waliingia kwenye maeneo ya mahakama na kuwakamata watu walioachiwa huru hakiwezi kutokea Tanzania. Kumbe nisichokijua kilikuwa ni kama 'usiku wa kiza'. Waswahili walisema "usimtukane mamba kabla hujavuka mto" na ndio hao hao waliosema "usitukane wakunga na uzazi ungalipo". Hata kabla ya wiki kwisha nikajikuta nimeumbuliwa na nchi yangu, kwani kile ambacho sikuwaza kinaweza kutokea Tanzania kimetokea na kuniacha nimepigwa na butwaa huku nimeyauma meno yangu kwa hasira. Jeshi la Polisi limeingia mahakamani kwa nguvu.

Mazingaombwe na wale wafanyao mazingaombwe! Siku ya Alhamisi kimefanyika kitendo kwenye Mahakama Kuu ambacho kama hakitakemewa na waliohusika kuchukuliwa hatua kali kinaashiria kubomoka kwa utawala wa sheria na utafutwaji wa haki katika mahakama za Tanzania. Na kitendo hicho kinatishia uhuru wa Mahakama, uhuru wa vyombo vya habari, na usawa wa raia wote mbele ya sheria.

Wakati polisi wanamfikisha mtuhumiwa wa kesi ya mauaji Bw. Ditopile Mzuzuri kwenye mahakama kuu jijini Dar-es-Salaam, bila sababu ya msingi waliamua kumpitisha mtuhumiwa huyo kuingia kwenye mahakama hiyo kwa kupitia mlango unaotumiwa na majaji. Kwa wale ambao hawajui taratibu za mahakama nyingi (siyo Tanzania peke yake hata sehemu nyingine duniani), majaji wanapokuja kazini au kwa shughuli mbalimbali mahakamani hapo kuna mlango ambao wao pekee wanapitia na mlango huo mara nyingi hautumiwi na watu wengine wakiwamo wafanyakazi wengine wa chombo hicho. Hata mawikili hawaruhusiwi kupita huko. Siyo tu kwa ajili ya heshima ya cheo chao bali pia kwa ajili ya usalama wao na uhuru wa chombo hicho

Lakini kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania ambayo naweza kuikumbuka kwa haraka maaskari wa jeshi la Polisi walitumia ubavu (pamoja na kumpiga kikumbo mlinzi wa Mahakama hiyo) na kulazimisha mtuhumiwa huyo kuingizwa mahakamani hapo kwa kupitia mlango huo wa majaji. Kitendo hicho kama kilivyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kiliwashangaza watu wengi wakiwamo wafanyakazi wa Mahakama hiyo. Licha ya polisi kuingia kwa nguvu mahakamani hapo waandishi wa habari nao walishambuliwa na maafisa hao na baadhi yao vyombo vyao vya kazi kuharibiwa na polisi hao na wanafamilia ya Dito na hivyo wandishi kunyimwa nafasi ya kufanya kazi zao kama kawaida. Vitendo hivyo siyo tu vinatishia uhuru wa mahakama bali pia uhuru wa vyombo vya habari wa kutafuta, kupata na kutoa habari.

Mshangao wa kitendo hicho ulioneshwa wazi na Msajili wa Mahakama hiyo bw. Prophi Lyimo ambaye alinukuliwa akisema kuwa “Kwa kweli tumekasirika sana, sijuwi walipewa nini, maana katika hali ya kawaida hawawezi kufanya hivyo. Haijawahi kutokea hapa, nimemwambia Tibaigana awabane polisi wake na wamueleze kwa nini wamefanya hivyo”. Katika vyombo vya habari haijawekwa wazi kama askari waliompitisha Ditopile kupitia mlango huo walikuwa na silaha ama la. Kama walikuwa na silaha kitendo hicho kinakuwa na uzito ambao maneno ya karatasi hayatoshi kuelezea. Bila ya shaka kuna sababu iliyowafanya askari hao kufanya kitendo hicho na hapa nitashuku tu sababu hizo hadi zitakaposemwa hadharani.

Inawezekana kabisa kuwa maafisa wa ngazi za chini wa polisi walifanya kitendo hicho baada ya kupewa amri na “mkubwa wao” kumpitisha Mtuhumiwa huyo wa mauaji kupitia mlango huo wa majaji. Kama ni kweli, “mkubwa” huyo ni lazima ajulikane na hatua za kinidhamu (ikiwemo kufukuzwa kazi, kushushwa cheo n.k) zichukuliwe dhidi yake. Afisa yeyote wa jeshi la polisi ambaye hajui uzito wa kuingia kwenye chumba cha majaji kwa nguvu na kupitisha watuhumiwa huko wakati kuna milango iliyopo kwa ajili ya kazi hizo hastahili kuvaa nembo ya jeshi letu! Askari wa chini waliotekeleza amri hiyo ambayo si halali ni lazima nao wachukuliwe hatua kali. Maaskari hawa hawawezi kujitetea kuwa “walikuwa wanafuata amri tu”. Kutii amri ambayo siyo halali ni kosa!! Rais kwa mfano, hawezi akatoka nje pale Ikulu na kumuamuru askari ampigie mtu risasi kwa vile Rais amejisikia hivyo na askari huyo akafanya hivyo!! Siyo kila amri inayotolewa na mkubwa ni halali! Maafisa wetu ni lazima (kupitia tukio hili) wafundishwe wazi kuwa “mkubwa” akikuamuru kufanya jambo ambalo unajua au unahisi ni kinyume na sheria unayo haki ya kukataa kulitekeleza hata kama itatishia ajira yako au kumuudhi mkubwa huyo. Hadi pale utakapohakikishiwa usheria wa amri hiyo. Endapo maaskari hawawezi kukataa kutekeleza amri isiyo halali basi Watanzania tuna matatizo kwani viongozi wanaweza kuwaamuru mamluki hao kufanya lolote lile bila kujali matokeo yake, kwani “bosi” kasema.!! Hili katika Tanzania ya leo halikubaliki, tunalipinga, na tunalilaani kwa uzito wote unaostahili.

Inawezekana pia kuwa maafisa wa polisi walifanya kitendo hicho ili kuonesha “ni nani” anayeletwa mahakamani hapo na ni jinsi gani mtu huyo ni tofauti na washtakiwa wengine. Ni wazi kuwa kesi ya Ditopile ni mojawapo ya kesi chache zenye makosa makubwa ambayo kiongozi wa serikali anaweza kuhusishwa nacho, lakini kesi shitaka analokabiliwa nalo siyo ngeni kwenye mahakama zetu. Huko nyuma kuna viongozi walioshtakiwa kwa kuhujuma uchumi, ubadhirifu, wizi n.k lakini hili la kiongozi kutuhumiwa kumuua mtu ni jipya na hasa jinsi mauaji hayo yanavyodaiwa kufanyika. Mara zote ambapo Bw. Dito amekuwa akiletwa mahakamani kuanzia kule Kisutu hadi Mahakamani vimbwanga hufuatana naye. Hiki cha sasa kimepita hayo yote! Polisi hawana sababu yoyote ya kuionesha mahakamani “uzito” wa mtuhumiwa kwani Ditopile anajulikana na jina lake limetangaa. Lakini, waliofanya kitendo hicho inawezekana kabisa walitaka kutuma ujumbe kuwa “Tutampeleka tunakotaka sisi, kwa wakati tunaotaka sisi, na hakuna anayeweza kutuzuia” Kama hilo ndilo lilikuwa mawazoni mwa maafisa hawa basi nalo ni sababu ya kumwajibisha afisa aliyesimamia zoezi hilo, na kama mkuu wa polisi wa Kanda alikuwa anaujuzi wa kitendo hicho na akashindwa kukizuia na yeye hana budi kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kuandika barua ya kujiuzulu. Kitendo hiki inawezekana kimechukua mistari michache kwenye vyombo vya habari lakini uzito wake unaweza kujaza maktaba!

Sababu nyingine ambayo naombea isiwe ya kweli inatokana na hiyo ya hapo juu. Maafisa wa polisi kutokana na amri waliyopewa au maelekezo waliyopewa waliamua kuitishia mahakama na hususan jaji au majaji ambayo wanaweza kujikuta wakisikiliza kesi hii. Hivi karibuni huko Uganda jambo kama hili limesababisha mgomo wa Majaji na wafanyakazi wa mahakama baada ya polisi kuingia mahakamani kwa mabavu na kuwakamata watu walioachiwa huru na mahakama hiyo ya Uganda. Hapo Tanzania , endapo jambo kama litavumiliwa au kujaribu kupuuzwa litajenga jaribio la chombo cha dola kuitisha mahakama ili isifanye kazi zake za kugawa haki kwa uhuru bila upendeleo. Katika mahakama zetu kuna watu wengi ambao wamewahi kushitakiwa kwa tuhuma nzito zaidi ya hiyo ya Ditopile, na hakuna siku ambapo washtakiwa waliingizwa kupitia mlango wa majaji, siyo wakati wa kesi ile ya uhaini au wa kesi ya Kiula na wenzake. Jaribio hili la kuitisha mahakama natumaini limeshindwa na halitatokea tena.

Hata kama mojawapo ya sababu hizo hapo juu ni ya kweli (ama zote) serikali ni lazima itamke mara moja kukikana kitendo hicho na kuahidi kuchukua hatua za kinidhamu siyo kuunda tume ya uchunguzi! Ingawa Msajili wa Mahakama ametamka kutofurahishwa kwake na kitendo hicho, Jaji Mkuu Bw. Barnabas Samatta ni lazima atamke na kukikemea kitendo hicho na aiambie serikali kuwa endapo jambo kama hilo au hata linalokaribiana na hilo kwa mbali litafanyika, waliohusika watatiwa mbaroni kwa kudharau mahakama na Mahakama yake haiwezi kukubali kuingiliwa na chombo kingine cha serikali hata kama kesi inamhusu mtu mashuhuri kiasi gani.

Zaidi ya yote, kwa vile kesi inaonekana kuwa na mvuto wa hisia nyingi hususan upande wa wanafamilia ya Ditopile ambao wamejaa jijini Dar-es-Salaam, Jaji Mkuu anaweza kuamuru kesi hiyo kuhamishiwa katika mahakama ya Kanda na kupelekwa mkoa mwingine kwenye matawi ya Mahakama hiyo ambapo inaweza kusikilizwa kwa uhuru bila kuvutia watu wenye hisia kali kwani siyo tu inatishia usalama wa maafisa wa mahakama bali pia raia wanaokuja mahakamani kwa kesi nyingine na watu wengine ambao kwa sababu moja ama nyingine wanaweza kujikuta wapo hapo mahakamani.

Vile vile, Jaji Mkuu ni lazima ahakikishe kuwa kama wale walioapishwa kulinda Katiba (maafisa wa Polisi) wameshindwa kazi hiyo, aamuru kuanzia sasa maafisa wa Magereza kumleta Mshitakiwa mahakama na kumuingiza mahakamani na kutoa ulinzi mahakamani hapo badala ya Polisi na ikibidi aombe Rais aidhinishe kikosi cha Polisi wa Jeshi kulinda mahakama hiyo kutoka kwa polisi wasiojua wajibu wao. Lililotekea mahakamani hapo jana si jambo dogo kwa kipimo chochote kile.

Ni matumaini ya wapenda demokrasia wote na wale wanaoelewa mtengano wa madaraka kuwa kitendo hicho (au kifananacho na hicho) hakitarudiwa tena, na endapo kitendo kama hicho kitarudiwa, basi Mahakama iamue kumuachia Ditopile huru kuliko kuvunja vunja na kusagasaga kama kwenye kinu uhuru wa mahakama zetu na hivyo kuharibu mchakato mzima wa utafutaji wa haki!
MKJJ!
"HUYU NI MWENZETU TENA NI MWEZANGU WA KARIBU SANA"
Umesema mengi Lakini hakuna hata moja litakalofanyika kuhakikisha huyu mtuhumiwa anawekwa katika kundi la watuhumiwa wengine wa aina yake.Kuhusu uwezekano wa yeye kuhamishwa na kesi ikasikilizwe sehemu nyingine kwa yale yaliyojiri sasa,Hili nalo si suluhisho.Suluhisho Kamili ni kila mtu mwenye jukumu lake kikazi anatakiwa kulitekeleza bila ya kujali huyu alikuwa ni nani ?Kuanzia Law enforecement organ and judiciary system, Lakini hilo ni ndoto kwasababu "HUYU NI MWENZETU TENA NI MWEZANGU WA KARIBU" Guess what do I meant by HUYU NI MWENZETU TENA MWEZANGU WA KARIBU?
 
Back
Top Bottom