Mkuu wa Mkoa yuko sahihi kuhusu Mabasi makubwa DSM, ni kero kwenye barabara za jiji.

Mkuu wa Mkoa yuko sahihi kuhusu Mabasi makubwa DSM, ni kero kwenye barabara za jiji.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Sisi abiria tuna tabia ya kutaka kushushiwa popote karibu na nyumbani kwetu. Hivyo basi kubwa litalazimika kusimama na kushusha abiria kwenye vituo vidogo vya madaladala na kusababisha usumbufu kwa daladala na magari madogo mjini. Hivyo, hata kama mmiliki wa mabasi anayo terminal kubwa ya kupaki magari yake huko Mbagala na Chanika lakini kabla ya kufika huko kwenye parking yake amekuwa amesababisha usumbufu mkubwa jijini.

Jambo la msingi wanalofanya wazungu huko ulaya kupunguza magari kwenda katikati ya mji ni tozo kubwa za kutembeza na kupaki magari katikati ya mji badala ya stand.

Serikali ya mkoa yatozeni bei kubwa magari hayo makubwa yanayokwenda katikati ya mji badala ya kuyataka yooote yapaki stand ya Mbezi. Hii itaongeza mapato kwa jiji na yataacha yenyewe kwenda katikati ya jiji ili kukwepa kodi hiyo ya kutembeza na kupaki magari katikati ya jiji.
 
Ni lazima jiji liweke sheria ngumu ili kurudisha nidhamu ya barabarani, otherwise foleni za Dar hazitaisha wala kupungua.
 
Ni lazima jiji liweke sheria ngumu ili kurudisha nidhamu ya barabarani, otherwise foleni za Dar hazitaisha wala kupungua.
Na Miji itakosa mpangilio mzuri kiasi cha kuongeza msongamano
 
Changamoto kubwa ya Dar hi mipango miji mibovu, na Uongozi wa kambale kesho anaweza kuibuka kiongozi mwingine akatengua tamko la Mkuu wa mkoa na watu wakashangilia kama kawaida.
 
Changamoto kubwa ya Dar hi mipango miji mibovu, na Uongozi wa kambale kesho anaweza kuibuka kiongozi mwingine akatengua tamko la Mkuu wa mkoa na watu wakashangilia kama kawaida.
Kutokuwa na sera ya wilaya,Mkoa, Kanda ,Nchi nzima lazima tutayumba tuu maana kila mmoja atakuja na mawazo yake mwishoe tunakuwa kituko sasa, kila mahala Stendi ya kufanya utakacho ukiuliza eti mapato ya mkoa.
 
Tatizo ni location ya mbezi luis.
Mbona airport wanakwenda? Mbona pale boti za Azam zinapopaki kwenda na kutoka Zanzibar wanakwenda hata wanaotoka Kisarawe na Mkuranga?

Kinachotakiwa pale ni connectivity nzuri ya stand ya Magufuli na mabasi ya daladala na mwendokasi kwenda maeneo mengine ya jiji. Kule vilipo vituo vya daladala vya mbezi juu na mbezi chini ni mbali sana kwa abiria wanaoshushwa stendi ya magufuli
 
Back
Top Bottom