Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali


"UKALI" tu usiozingatia misingi ya utu, heshima, busara, hekima na sheria, ni UPUMBAVU na UJINGA na ni dalili za wazi sana za UTAWALA WA UDIKTETA..

Kwani binadamu gani aliyekamilika na asiyekosea? Hayupo!

Hata huyu mtu mwenye cheo cha kidunia cha "URAIS" naye ni binadamu na anakosea...!

Turudi kwa utawala wa Mwl. Julius K. Nyerere

Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa mkali kweli. Lakini ukali wake haukuwa kama wa yule Mwendazake Magufuli.

Hili umethibitisha mwenyewe kuwa alikuwa akiwaita na kukemeana wenyewe kwa wenyewe huko ndani siyo hadharani mbele ya wanaoongozwa ktk namna ya kutweza utu na heshima ya mtu.

Nakupa changamoto moja na kisha tuambie hapa.

Katika utawala wa karibu miaka 25 ya Urais wa J. K. Nyerere, ni wapi aliwahi kumtukana waziri wake hadharani kwenye mkutano wa hadhara? Ni wapi amewahi kufukuza kazi mtumishi wa umma hadharani bila kufuata utaratibu wa kisheria?

All in all hujamwelewa Mama Samia na kauli yake hiyo. Hana maana ya hiyo unayoidhania wewe..!!
 
Waulize watu wazima walinunua mafuta ya kula na sukari shillingi ngapi mwaka 2014 nq 2015 na kisha wakaja kununua shillingi ngapi mwaka 2017 na kuendelea
 
Namuunga mkono Samia hatakiwi kufanya ukiranja kwa kila mtumishi.
Laa sivyo basi nafasi za Uwaziri, Ukatibu Mkuu,Ukurugenzi/Ukamishna viondolewe.
Watumishi wote wawe level moja.
 
Sisi bado ni nchi maskini wewe kilaza, achana na zile propaganda na blah blah za sisi ni dona,.sisi ni matajiri
Jiandaeni kushuka na kuwa nchi maskini tena, muda si mrefu subiri IMF wafanya kikokotoo chao, mtatafuta pa kujificha
 
Jiandaeni kushuka na kuwa nchi maskini tena, muda si mrefu subiri IMF wafanya kikokotoo chao, mtatafuta pa kujificha
Ni lini Tanzania imewahi kuwa nchi tajili? Au na wewe ndio wale mazuzu waliaminishwa na yule mgonjwa wa akili kwamba Tanzania ni Dona kantre?
 
Rais anajuwa kila kinachoendelea katika huo mradi wa umeme hiyo kampuni magu aliyoipa tenda bila ya ushindani haina uwezo wa kutosha mradi uko nyuma ya wakati na magufuli alikuwa halipi kwa wakati hayo ndiyo yaliyochelewesha mradi sasa unataka January afanye nini au rais amfukuze kwa sababu gani .Halafu haitakiwi rais aogopwe inatakiwa aheshimiwe na yeye awaheshimu wasaidizi wake ndio utaratibu mambo ya kufokeana ni ushamba ,samia anaendesha nchi kutokana na ethics za uongozi law sababu yeye mbobezi katika taaluma ya utawala wa umma si mwanajeshi wala mtafiti wa mabibo ya korosho kwa hivyo tumwachie mama afanye kazi chuki zako weka pembeni.
 
Matatizo ya watumishi uliyoyataja hapa yanaweza kumalizwa kwa kurekebisha mfumo wa ajira na ngazi za uwajibikaji sio kwa Rais kuzunguka maofisin na kufokea watumishi wa ngazi za chini na wasimamizi wao.

Bodi za hospitali, bodi za shule, bodi za vyombo kama TRA, polisi,TANROADS, TARURA, Halmashauri, ofisi za DMO, vinapaswa viwe na mamlka ya kufukuza watumishi wasiokidhi vigezo kwa haki na wepesi bila urasimu.
 
Rais wa nchi sio kama mume wako au baba au mama kwenye familia. Nchi ni ya wananchi wote na inaendeshwa kwa mihimili mitatu, taasisi na mifumo kwa kuzingatia sheria na taratibu maalum.
Ndio maana hata familia imekushinda,unataka kila mtu ajiongoze yeye mwenyewe,nn maana ya kuwa kiongozi mkuu?
 
Ndio maana nasema ujinga ni mzigo,kwa hiyo taasisi itakuwepo bira mkuu wa taasisi?, kwani tuna viongozi?, kazi ya kiongozi ni kufanya nini?,kuimba mapambio ni kucheza kwaito?
 
Tabia na hulka za waafrika esp Watanzania kwa namna ya makuzi yetu kuanzia nyumbani hatuna kitu kinaitwa nidhamu ya moyoni tuna nidhamu ya uoga ambayo ndio imetusaidia kufika tulipo leo
Mkuu wa Nchi anaposema anataka nidhamu ya moyoni sio kwa Watanzania Hawa ambao makuzi yao yalitegemea
1. Baba na mama wanataka nini kutoka kwa mtoto Kama ni kusoma basi usome na siyo kucheza na huwezi kutoa maamuzi tofauti na yao
2. Shuleni tunafagia huku tukiwa tumesimamiwa na viranja wakiwa wameshika fimbo Kama walimu
Tumekuzwa makuzi ya kusimamiwa hivyo kuniambia nije kuwa na nidhamu ya moyoni nikiwa na miaka 30 itakuwa ni ngumu Sana kwa iyo nitakapo pata huo mwanya nitafanya kazi as usual tu siku ziende
Afrika ni tofauti na ulaya/America kwenye Mambo mengi Sana na siyo lazima Kila kitu kiende Kama wao ni lazima nasi tuwe na mfumo wetu ili mradi tumekubaliana kufika hata wao miaka hiyo wamepitia ndio maana walitumikisha ndugu zetu
 
Sheria zifuatwe na watu wafanye kazi zao ndio cha msingi na wasipofanya kazi wawajibishwe kwa kufuata sheria zilizopo,hayo mambo ya kuogopwa, ukali au kufokafoka havisaidii chochote na mara nyingi vinajenga nidhamu ya woga tuu na madhara yake ni kushuka kwa utendaji wa kazi na watu wanabaki kufanya kazi kwa kujipendekeza ili waonekane tuu
 
Sasa jaziba mwisho matokeo yake ni nini siyo ukali? we jamaa pimbi kweli

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Marekani na Ulaya, ambapo tunawaiga kwa demokrasia, hawabembelezani.

Trump alikuwa anafukuza watu karibu kila siku.

Hakuna kitu kinachoitwa nidhamu ya moyoni!
Ujinga wako ni kwamba hujui hata Rais wa Marekani ana mamlaka gani US.

Rais wa Marekani ana mamlaka ya moja kwa moja Jeshini, CIA, FBI ,Immigration, Posta, IRS, Mambo ya nje na sehemu nyingine chache sana. Huko ndiko uliona Trump mwenye kichwa kibovu akifukuza na kofokea watu hovyo.

Rais wa Marekani hana mamlaka na hawezi kufanya chochote zaidi ya kushawishi sera juu ya walimu, madaktari, manesi, polisi, maafisa kilimo, afya, pensheni, idara za maji, umeme na sehemu nyingine nyingi. Na hata sera ambazo hazipendwi kwenye hizo sekta zinaweza kupingwa mahakama za majimbo na mahakama kuu.
 
Ni leadership style yake! Hakusema hatawachukulia hatua bali hatafoka. Hana aina ya uongozi wa kufoka. Atawalea watakaoshindwa atawachukulia hatua kali. Kwa hiyo Madam President is right ,Mzee Magufuli was right n Baba wa Taifa Mwalimu was right. Kwani leadership style inategemea pia personal attitude ya kiongozi. Tusome kidogo leadership and governance. # Tusikuze mambo .
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Tengenezeni mifumo imara yakiutendaji itakayosimamia sekta zote.Tusidanganyane kua kuna nchi ambayo rais anasimamia kila kitu.Ukali wa rais hauwezi kua na maana kama nchi haitakua na mifumo thabiti yakumrahisishia rais na wananchi kazi.Tutoke kwenye zama zakumtegemea mtu.
 
Kwahiyo ilo nalo unataka hadi rais aje kuwaambiwa muwajibike.kwa jinsi mnavyofanya unadhani nani mjinga kati ya nyie wafanyakazi na huyo rais anayetaka kila mtu ajitambue nakujisimamia mahali pake pa kazi.inaonekana shule mlizosoma hazikuwasaidia ndo maana mnashindwa kujiongoza nakurekebishana hadi msubiri rais aje awaambie.Waafrika tusipende kua ng'ombe kila mara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…