Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali

Mkuu wa nchi lazima awe mkali na aogopwe. Asipoogopwa kila kitu kitakwenda mrama. Hata hayati Julius Nyerere aliogopwa na alikuwa mkali

Wewe kinachokusumbua inaonekana uko kwenye kundi la legacy badala ya kuangalia mahitaji ya nchi.Unachoshindwa kurlewa ni kwamba kabla ya huyo magufuli kazi zilikuwepo na watu walifanya na zitaendelea kuwepo hadi mwisho wa dunia.Kwahiyo hakuna mtu special kwenye nchi.Ndo maana tunasema hakuitajiki kua na mtu wakutusukuma bali iwepo mifumo ili ifanye kazi miaka mingi zaidi umri ambao huyo mtu wako wakukufokea hawezi kufika.
Hauelewi ila unajifanya unaelewa.

Hoja hapa ni kuwa hakuna nidhamu ya moyoni kwenye kufanya kazi

Una kichwa kizito sana.
 
Vijana waliopewa kuuwa watu kipindi Cha Simba wa yuda mmeanza kujitokeza!!, Mliwaza kutumia nguvu bila maarifa ndio njia ya kutatua changamoto, mmekatili maisha ya watu huku mkineemeka wachache kwa kivuli Cha kuwatengenezea drama wananchi. Puuzi kubwa hili.
 
Hauelewi ila unajifanya unaelewa.

Hoja hapa ni kuwa hakuna nidhamu ya moyoni kwenye kufanya kazi

Una kichwa kizito sana.
Kwahiyo magufuli alikuwa na nidham ya moyo!!. Mmejaa roho mbaya wapuuz wakubwa
 
Kuongoza maana yake ni kusimamia; hakuna uongozi bila usiamamizi.

Ndiyo maana nilishangaa sana kauli iliyotolewa na rais kwamba watu walikuwa na nidhamu ya woga kwa sababu ya kusimamiwa.

Who cares iwapo nidhamu hiyo ni ya woga au ni ya halali ilimradi shughuli za serikali zinakwenda inavyotakiwa?
Ndugu,ungekuwa wewe au mzazi wako ni mmoja kati ya waliokuwa wananyaswa na kudhalilishwa hadharani, lazima ungejali.
Ungekuwa ni ni mmoja kati ya wanaojali na kuthamini utu na haki za wengine, ungejali.
Yaonekana hukujaliwa Upendo.
 
Samia kulinda heshima yake ang'atuke mara moja.
0_20220404_104346.jpg
 
Kwani huu umeanzisha ww hivyo unatembea na marking scheme, au ni wa mumeo hivyo una haki ya urithi kwenye kila kitu cha mumeo?
Ustaarabu ni kitu cha bure. Jenga hoja acha matusi.
 
Haya ndiyo yanaitwa mawazo mgando. Nchi yenye Katiba Bora lazima iwe na mifumo inayofanya kazi.

Kuwa na Rais anayefoka ni kielelezo cha mapungufu ya mfumo au ya Rais mwenyewe. Kwa nini UFOKE wakati una vyombo vyako vya kufanyia kazi.

Iko siku Nyankurungu2020 utakuja sema kuwa Tanzania inapaswa kuwa na Rais anayetafuna mahindi barabarani, au Rais anayenunua mapapai au Rais anayekaa vijiweni.

Hayo maujinga yote tumeyafukia na Mwendazake mwaka jana mwezi Machi pale Chato
Nani kakuambia rais afoke? Kusimamia madaraka ya urais sio lazima afoke. Kumbuka bianadamu anaishi kwa mazoea .

Kuwa na katiba Bora haimaanishi kuwa mamlaka ya urais yasionekane pale uzembe unapotokea.
 
Nyerere hakuwa na hulka (compulsive) ya kufokea viongozi na watumishi ovyo ovyo tena hadharani. Ilifanyika kwa visa na nyakati maalum. Wala haikuingia mubashara kwenye media (magazetini na kwenye radio).

Mambo yalikuwa yakimalizwa katika mazingira ya kiofisi Ikulu. Wananchi walikuwa wakijionea matokeo tu na kukisia kuwa kuna mtikisiko umepita huko Ikulu, au wizarani au kwenye shirika au kwenye taasisi. Kinachofuatia ni kuvuja kwa udaku.

Hii ya awamu ya tano ni kipropaganda zaidi kama show biz vile. Maagizo ya kazi, maonyo, kejeli, vitisho, adhabu zinatangazwa hadharani hata kwenye taarifa ya habari. Ujinga huo haukuwepo wakati wa Mwalimu na nidhamu ilikuwepo.
Ndugai alikaripiwa hadharani bila ya kukosea.
 
Siyo hospital yetu tu, hali ipo hivyo kote.

Hakuna nidhamu ya moyoni na kwa asili Waafrika hatupendi kazi, tunaona ni utumwa.

That's why tunahitaji kiongozi imara kama Magufuli anayeweza kusimamia vizuri.

Na hiyo ndio nidhamu yetu ya moyoni.
Tunashindwa kutofautisha kati ya UOGA na NIDHAMU. Mara zote sio lazima upende kutoka moyoni kutii Sheria / Kanuni/ SOPs..Inatukumbusha Sayansi Darasa la V. Matendo ya Hiyari na Yasiyo ya Hiyari.

Hiyari Yashinda Utumwa.
 
Bi tozo yeye anasema hana hulka ya kufokafoka kwa sababu ana watu wanaoamua kwa niaba yake.

tofauti na hayati JPM, yeye alijua wazi ukiwaacha baadhi ya watu wafanye wapendavyo nchi ingeenda mlama.

Kama ilivyo hivi sasa, mfumuko wa bei, hakuna anayeudhibiti!

Watu wanafanya wanavyoona inafaa.
Ndiyo maana Nyumba nyingi sana zinaharibiwa na akina Mama Kama Baba hayupo, hadi Masela wanaingia ndani! Lakini Dingi akiwepo hata hao Masela watapita mbali sana na hiyo Nyumba!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tunashindwa kutofautisha kati ya UOGA na NIDHAMU. Mara zote sio lazima upende kutoka moyoni kutii Sheria / Kanuni/ SOPs..Inatukumbusha Sayansi Darasa la V. Matendo ya Hiyari na Yasiyo ya Hiyari.

Hiyari Yashinda Utumwa.
Waafrika tunatafsiri kazi kama utumwa...

As a result wengi wetu hatupendi kazi na ndio maana bila kusimamiwa kazi haiendi.

Hiari yetu ni kutokupenda kazi.
 
Mkuu kwenye hii hospital ninayofanyia kazi siku hizi tunaingia ofisi 07:30 then tunakuwa na vikao vya Morning Report mpaka 09:00 hadi 09:30.

Hapo mtaenda kuhudumia wagonjwa hadi kwenye 10:30 halafu watu wanaenda canteen kunywa chai. Chai inanyweka huku stori zinapigwa hata mpaka 12:00 hivi au zaidi.

Mkirudi mnafanya kazi saa moja au moja na nusu mnarudi canteen kupata lunch ndio mpaka saa 15:30 watu wanarudi ku-sign out. Siku imeisha.

Hiyo ndio nidhamu ya moyoni ya hawa Watanzania hapa nilipo. Enzi za Magufuli tulinyooshwa na kazi zilifanyika kwa weledi knowing ukizingua imekula kwako.

RIP Magufuli.

Enzi za Magufuli si ndio wahanga wa ajali ya moto wa lori la mafuta hapo Morogoro walifia wote hapa Muhimbili wakati wangeweza kupona. Au unadhani ukitunga story ndio utatopoteza maboya? Sasa kama enzi za Magufuli mlikuwa mnafanya kazi hivyo, mbona mlishindwa kumtibu Covid?
 
Waafrika tunatafsiri kazi kama utumwa...

As a result wengi wetu hatupendi kazi na ndio maana bila kusimamiwa kazi haiendi.

Hiari yetu ni kutokupenda kazi.
Hata ulaya na uchina hawakufika kwa pale kwa kuwa legelege..
Na hata sasa kwao mambo ya ufisadi na uhujumu unaadhibiwa kama mnyama
 
Kuongoza maana yake ni kusimamia; hakuna uongozi bila usiamamizi.

Ndiyo maana nilishangaa sana kauli iliyotolewa na rais kwamba watu walikuwa na nidhamu ya woga kwa sababu ya kusimamiwa.

Who cares iwapo nidhamu hiyo ni ya woga au ni ya halali ilimradi shughuli za serikali zinakwenda inavyotakiwa?
Na kwa nini Mfanyakazi uwogope kusimamiwa na mwajiri wako!? Unaficha nini!?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tunashindwa kutofautisha kati ya UOGA na NIDHAMU. Mara zote sio lazima upende kutoka moyoni kutii Sheria / Kanuni/ SOPs..Inatukumbusha Sayansi Darasa la V. Matendo ya Hiyari na Yasiyo ya Hiyari.

Hiyari Yashinda Utumwa.
Na kuna nidhamu ya uoga!
 
Enzi za Magufuli si ndio wahanga wa ajali ya moto wa lori la mafuta hapo Morogoro walifia wote hapa Muhimbili wakati wangeweza kupona. Au unadhani ukitunga story ndio utatopoteza maboya? Sasa kama enzi za Magufuli mlikuwa mnafanya kazi hivyo, mbona mlishindwa kumtibu Covid?
Nani alikuambia mkifanya kazi vifo havitokei?
 
Back
Top Bottom