Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Nyamwasa walikuwa pamoja na Kagame muda wote kuanzia miaka ya 1990's mpaka 2010 ilipoonekana Kagame anataka kumuondoa kabisa serikalini akakimbilia Africa Kusini ndipo akaanza kutoa hizi tuhuma zake.
Alikimbilia huko kuokoa maisha yake.
 
Aliyewahi kuwa mkuu wa ujasusi Rwanda na Balozi wa Rwanda nchini India, Lt. Gen Kayumba anasema matatizo yote yanayotokea mashariki ya Congo yanasababishwa na kagame.

Anasema Congo hamna tena tatizo la Banyamulenge ,lilishakwisha zamani na wana haki sawa na wanahudumu hata sasa katika serikali ya Congo.
Anasema kagame amekuwa Congo zaidi ya miaka 30 akiwaua wahutu wa Fdrl baada ya Genocide mpaka leo, na kwamba hana kisingizio tena kuhusu Fdrl nchini Congo.

Anasema M23 wameiburiwa upya na Rwanda 2021 baada ya Tshikedi kuingia makubaliano na Burundi na Uganda, ndipo Kagame alichukia na kusema kama hajakaribishwa atajikaribisha mwenyewe.

Amekiri Rwanda inaiba madini Congo na kupeleka Rwanda kwa ajili ya kuyauza nje na anasema kila eneo wanaloshika M23 lenye madini, madini uanza kusafirishwa haraka kwenda Rwanda.

Anakiri RDF inatoa sapoti ya 100% kwa M23.

Anasema Rwanda akiikamata Kivu yote, ataivamia Burundi na huo ndio mpango.

Anakiri ndani ya Rwanda wahutu wamefungwa minyororo na kufuri hawana pakuongelea na hawana mtetezi.

Anakiri Rwanda ina wakimbizi wengi wahutu na watusi ambao hawakubalina na sera na utawala wa kagame, na kwamba kagame asipowasikiliza kuna hatarii ya kutokea Genocide nyingine Rwanda.

Kumbuka huyu Mtusi kama ilivyo kwa kagame.

Hapa chini nimeweka interview yake yote ya leo wakati akihojiwa akiwa uhamishoni nchini Afrika Kusini.

View: https://x.com/Sentletse/status/1885998079419003033?t=XrJ7G6I2xDOUSU6Sr__OXg&s=19

Oooh ,...! Ndo maana Kagame ana Hasira na South Africa.
 
Hata Sudan Kusini haikupaswa kupewa uanachama wa EAC kwa sasa.
Yeah nimemsahau na S.Sudan Jumuiya haina standards imara inaokoteza tu takataka yoyote.

Mgogoro huo umeripuka tena jumuiya kimya wala haielewi nini cha kufanya member muathirika wa mgogoro anasusia kikao kama sio uwehu huu nini ?

Kwake yeye anaiamini zaidi SADC kuliko EAC huyu kama sio chizi ni nani ?
 
Mkuu unamsemea Leutenant General, former Chief of Staff wa jeshi, jasusi, Balozi. Haya unayoandika hapa sio ya wewe kumfundisha yeye, ni ya yeye kutufundisha sisi.

Uliyoandika almost yote kayafanya kama maagizo au mikakati yake kwa ngazi za kati mpaka ngazi ya juu jeshini. Mpaka anafikia kutuhumiwa kumpa challenge Kagame unahisi alikuwa level za kuwa boya mwoga; kutoroka mamlaka, mpaka anasalimika kuuwawa. Unahisi ni kiazi kama unavyomuandika hapa?

Nasema hivi, zipo level ambazo mtu akifikia plus matendo aliyofanya kumtishia kifo ni kujisumbua tu. Anakijua kifo kukuzidi, ameshuhudia vifo, ameshiriki kuua, ameagiza kuua. Sasa kuanza kumuelekeza Rwanda wanaua hivi na vile wakati ndio kazi zake hapo unanishangaza.
Hawa watoto wakishaangalia movie za hollywood wanahisi wanajua kila kitu kuhusu ujasusi.
 
Congo has always been unstable kusingizia Rwanda matatizo yote ya Congo ni ufinyu wa akili.

Burundi imechoka kuliko Ileje kuna ubaya gani kakiwa kamkoa ka Rwanda au TZ? Hata fees zao za uanachama EAC wanashindwa kulipa bora iwe mkoa tu.
 
Aliyewahi kuwa mkuu wa ujasusi Rwanda na Balozi wa Rwanda nchini India, Lt. Gen Kayumba anasema matatizo yote yanayotokea mashariki ya Congo yanasababishwa na kagame.

Anasema Congo hamna tena tatizo la Banyamulenge ,lilishakwisha zamani na wana haki sawa na wanahudumu hata sasa katika serikali ya Congo.
Anasema kagame amekuwa Congo zaidi ya miaka 30 akiwaua wahutu wa Fdrl baada ya Genocide mpaka leo, na kwamba hana kisingizio tena kuhusu Fdrl nchini Congo.

Anasema M23 wameiburiwa upya na Rwanda 2021 baada ya Tshikedi kuingia makubaliano na Burundi na Uganda, ndipo Kagame alichukia na kusema kama hajakaribishwa atajikaribisha mwenyewe.

Amekiri Rwanda inaiba madini Congo na kupeleka Rwanda kwa ajili ya kuyauza nje na anasema kila eneo wanaloshika M23 lenye madini, madini uanza kusafirishwa haraka kwenda Rwanda.

Anakiri RDF inatoa sapoti ya 100% kwa M23.

Anasema Rwanda akiikamata Kivu yote, ataivamia Burundi na huo ndio mpango.

Anakiri ndani ya Rwanda wahutu wamefungwa minyororo na kufuri hawana pakuongelea na hawana mtetezi.

Anakiri Rwanda ina wakimbizi wengi wahutu na watusi ambao hawakubalina na sera na utawala wa kagame, na kwamba kagame asipowasikiliza kuna hatarii ya kutokea Genocide nyingine Rwanda.

Kumbuka huyu Mtusi kama ilivyo kwa kagame.

Hapa chini nimeweka interview yake yote ya leo wakati akihojiwa akiwa uhamishoni nchini Afrika Kusini.

View: https://x.com/Sentletse/status/1885998079419003033?t=XrJ7G6I2xDOUSU6Sr__OXg&s=19

Huo U General na Uluteni aliupata kwa kuua watu. Sasa anaanza kutumiwa na mabeberu wakati yeye mwenyew ni part of problem
 
Congo has always been unstable kusingizia Rwanda matatizo yote ya Congo ni ufinyu wa akili.

Burundi imechoka kuliko Ileje kuna ubaya gani kakiwa kamkoa ka Rwanda au TZ? Hata fees zao za uanachama EAC wanashindwa kulipa bora iwe mkoa tu.
Ufisadi, umalaya na ubinafsi vinamaliza Afrika
 
Hili nimelisoma kwenye makala nyingi sana..... kiufupi Kagame anatamani mno kuwa na Ushawishi huko Drc kuizidi Uganda na Burundi mahasimu wake wa kikanda.

zitto junior JokaKuu
Kagame anataka kujipenyeza ndani kabisa ya DRC, anataka kusimamisha uongozi ambao utakuwa loyal kwake, anataka kuweka mamluki wake ili aifaidi DRC vizuri, na amegundua jeshi la DRC ni dhaifu, ana intel ya kutosha kuhusu jeshi la DRC, hii vita ni ngumu kwa DRC kwa sababu tayari PAKA ameshaweka mashushu kila mahali, analifahamu jeshi la DRC kuliko hata jeshi linavyojifahamu.

Kwa namna yeyote intel ya DRC imefeli, na intel ikifeli hamna tena ujanja,.

Lakini pia Kagame anagomba na kutishia nchi baadhi za SADC kuingilia windo lake, hao waasi wamesema watakwenda hadi Kinshasa.

Pasipo msaada wa SADC, Congo inapigwa na Rwanda hadi Kinshasa.
 
Back
Top Bottom