Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Ni kweli mkuu nashangaa sana nikiona watu wakimsema vibaya.Naam, wewe utakua ni mkazi wa Arusha. Huyu kijana amesaidia wananchi wengi Sana,, bila kujali itikadi zao. Binafsi niliwahi kufika Mara kadhaa ofisini kwake, akifika anawasalimia wananchi kwa nidham huezi amini ni Mkuu wa wilaya. Kuna wanasheria zaidi ya kumi pale ofisini kwake wa kujitolea kwa ajili ya kuwasaidia wananchi yeye ndo naskia anawafadhili. Amekua anafanya semina za ujasiriamali kuwafundisha Wanawake na vijana ujasiriamali.
Nachokiona mh. Mbunge hataki Wala hapendi kuona yule KIJANA anakubalika na kufanya KAZI. Majuzi bila aibu Eti akaitisha kikao Cha bajaji akapanga watu wakumchafua huyu DC. Gambo usipojirekebisha na kufanya hizi siasa zako chafu hatutakuchagua Tena hakika nakuambia.
Jambo lingine lililonifurahisha kwenye ziara zake wakati wa kutatua kero za wananchi, wakati mwananchi anapewa maiki aseme tatizo lake alikuwa akiwakemea wale wanaoanza kusifia ccm ndipo waseme matatizo yao.
Alikuwa akiwaambia, (hapa hatupo kwenye mkutano wa ccm! Sema shida yako tukusaidie).
Kuna ziara tulienda nae kule Kimandolu kwenye soko moja sasa yule mkuu wa soko akamleta kibega mmoja ambaye inasemekana aba tabia ya kupora mizigo ya watu sokoni, huyo kibega akaanza kujitetea kwa mkuu wa wilaya ila mwisho mkuu wa wilaya akamkabidhi kwa mkuu huyohuyo wa soko akamwambia huyu kwa kuwa ameomba msamaha, namuacha kwako uwe mwangalizi wake. Akiiba tena mlete kwangu au nipigie simu nitume gari la polisi.
Kuna migogoro mingi ametatua mbele ya macho yangu mpaka nikafikiria serikali ilikuwa wapi muda wote?
Migogoro mingine mingi ilikuwa ndani ya ofisi aliyopokea kutoka kwa mkuu wa wilaya aliyepita ila yeye aliishughulikia kikawaida kabisa na ana kawaida ya kwenda kwenye eneo lenye mgogoro.
Wakuu wengine wanapambana kutatua matatizo ya wananchi wakiwa kwenye ofisi zao lakini huyu wa Arusha anaenda sehemu husika akiwa na viongozi wote wa ngazi ya chini