hebu taja sifa za kuwa mkuu wa wilaya tuzijue
haina tofaut mana atapokea maagizo toka kwa baba yake na atayatekeleza kwa maslahi yao wao wawili kifamilia.Duh Magufuri angefanya kama Museveni Jf hapa pangechimbika kwa post
Mtoto wa mjomba wa Rais, shemeji wa Rais, mdogo wa Rais, mtoto wa Rais, mke wa Rais, n.k' kuteuliwa na Rais kwenye nafasi za uongozi wa kisiasa upo Afrika tu, ndiyo demokrasia ambayo tumeamua kuifuata. Demokrasia hii ya pekee ya Afrika, inayoshabikiwa na Afrika ndiyo inayolifanya bara la Afrika liwe la pekee lenye maendeleo ya pekee Duniani. Ujijnga mkubwa haupo kwa viongozi wanaoyafanya hayo bali kwa wananchi wa Afrika. Umaskini wetu mkubwa wa kichwani ndiyo chanzo kikuu cha haya yote. Mungu ibariki Afrika ambayo uliipa kila kitu lakini ukaruhusu umaskini wa vichwa vya waafrika.Kwahio kama amemlea na anazo sifa za kuteuliwa basi aachwe?
Ufipa nani kawalogaaaa...
Mara baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya uliofanyika na kutangzwa leo, jamii imeanza kuwachambua na kujuwa historia zao na ushiriki wao katika kumasaidia kazi Mh Rais.
Wananchi wamekuwa na shauku ya kumfahamu na kuelewa historia ya Mkuu wao mpya wa Wilaya Mh. Happy es Senenda William. Kabla ya kuwa DC wa Kisarawe tunaambiwa dada huyu alikuwa Manager wa HR wa TANROADS Mkoa wa Tanga, ni mdada mdogo mwenye elimu ya Masters. Mwaka 2010 aligombea ubunge viti maalumu kupitia mkoa wa Geita lakini hakufanikiwa, mwaka 2015 alipumzika ili kuzunguka na baba kumtafutia kura
Habari zinazidi kupenyeza kuwa Mh.Happyness William ni mtoto wa kulelewa na Rais JPM, amesomeshwa na Rais na amekuwa akiishi na JPM kwa maisha yake mpaka alipopata kazi. Kifupi Mh.Happyness ni "mtoto" wa JPM na kwa sasa ni DC wa Kisarawe
Ama hakika huu ni msimu wa vijana...Vijana mjiibidishe ili muonekane na mpate Wilaya au Mkoa.
Tusishabikie tusichokijua. Hapa suala siyo uwezo wa mteuliwa bali ni kukiuka misingi ya uadilifu. Hii siyo kazi ya uwalimu, udaktari au uhasibu, ni nafasi ya uongozi wa kisiasa. Hapa kuna mgongano wa kimaslahi. Meneji wa kampuni ya umma akimpa tenda kwenye kampuni anayoiongoza mwanae, anakuwa ametenda kosa. Siyo kwa sababu mwanae hana uwezo wa kutekeleza tenda bali tunakuwa hatuna uhakika kama tenda amepewa kwa sababu ya uwezo (ambao anao) au kwa sababu ya mahusiano ya kifamilia.Usigeuze JF kuwa chungu cha majungu! Ongelea uwezo wake, sio uhusiano wake...ungejisikiaje kama ungekuwa wewe unaomba kazi sehemu afu unanyimwa simply because wewe una undugu na rais...tuletee CV na track record ya performance sio mijungu
Mara baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya uliofanyika na kutangzwa leo, jamii imeanza kuwachambua na kujuwa historia zao na ushiriki wao katika kumasaidia kazi Mh Rais.
Wananchi wamekuwa na shauku ya kumfahamu na kuelewa historia ya Mkuu wao mpya wa Wilaya Mh. Happy es Senenda William. Kabla ya kuwa DC wa Kisarawe tunaambiwa dada huyu alikuwa Manager wa HR wa TANROADS Mkoa wa Tanga, ni mdada mdogo mwenye elimu ya Masters. Mwaka 2010 aligombea ubunge viti maalumu kupitia mkoa wa Geita lakini hakufanikiwa, mwaka 2015 alipumzika ili kuzunguka na baba kumtafutia kura
Habari zinazidi kupenyeza kuwa Mh.Happyness William ni mtoto wa kulelewa na Rais JPM, amesomeshwa na Rais na amekuwa akiishi na JPM kwa maisha yake mpaka alipopata kazi. Kifupi Mh.Happyness ni "mtoto" wa JPM na kwa sasa ni DC wa Kisarawe
Ama hakika huu ni msimu wa vijana...Vijana mjiibidishe ili muonekane na mpate Wilaya au Mkoa.
Tusishabikie tusichokijua. Hapa suala siyo uwezo wa mteuliwa bali ni kukiuka misingi ya uadilifu. Hii siyo kazi ya uwalimu, udaktari au uhasibu, ni nafasi ya uongozi wa kisiasa. Hapa kuna mgongano wa kimaslahi. Meneji wa kampuni ya umma akimpa tenda kwenye kampuni anayoiongoza mwanae, anakuwa ametenda kosa. Siyo kwa sababu mwanae hana uwezo wa kutekeleza tenda bali tunakuwa hatuna uhakika kama tenda amepewa kwa sababu ya uwezo (ambao anao) au kwa sababu ya mahusiano ya kifamilia.
Wenye uwezo na masters siyo huyo tu. Kwa nini hao wote hawakupewa? Kwa hiyo hizi teuzi haziangalii uwezo na elimu pekee yake bali ni pamoja na vigezo vingine, huenda vya upendeleo vikawa ni miongoni.
Kama ni kweli yaliyoandikwa, nijuavyo mimi ni kwamba, kiongozi mwadilifu kabisa kabisa, kamwe asingeweza kufanya hivyo. Ndiyo maana Viongozi waliowahi kuwa na uadilifu wa hali ya juu kama Mwalimu hawakuawahi, hata mara moja kuwapa uongozi wanafamilia kwenye nafasi za uteuzi zinazofanywa na Rais, hakuwahi kufanya hata siku moja. Na haya mataifa yenye demokrasia, huwezi kuona kitu kama hicho hata siku moja. Haya yanatokea Afrika, na bahati mbaya sana watu wanatetea vitu vinavyokiuka misingi ya utawala bora.
Wanaanza zengwe na kusahau wasihii..Kwahio kama amemlea na anazo sifa za kuteuliwa basi aachwe?
Ufipa nani kawalogaaaa...
Duh hongera sanaKesho waziri wake nae akiteua ndugu yake ataweza hata kumuhoji kama yeye keshaanza kuonyesha mfano mbaya?
conflict of interest kama unaelewa umepata jibu kama huelew tafuta maana ya neno hiloKwahio kama amemlea na anazo sifa za kuteuliwa basi aachwe?
Ufipa nani kawalogaaaa...
Sifa zilizotajwa hapa ni kuwa na masters,jee hiyo ni sifa ya kuwa mkuu wa wilaya? Pia sifa nyingine ni kugombea ubunge viti maakumu, jee hiyo nayo ni sifa ya kufaa kuwa mkuu wa wilaya? Au hiyo ya kuwa HR Tanroad, tujiukize aneingia Tanroad mwaka gani na kaingiaje maana tunajua Tanroad iko chini ya wizara gani na wizara hiyo ilikuwa chini ya nani.Akiwa mtoto wa JPM kama ana sifa ndiyo asiteuliwe. Mmeambiwa "Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali".