Dah! Siku nyingine ukishuka hapo Kisegese, mwambie boda akulete Mofu ili uje ule samaki wa Mto Kilombero. Msimu huu samaki aina Ndipi, njuju na ngogo; ni wengi sana. Ni mwendo tu wa kula na ubwabwa.
Halafu ushukuru siku hizi kuna bajaj, kuna bodaboda, kuna Noah, kuna TATA, nk. Miaka ya 90, usafiri pekee wa huko ulikuwa ni treni ya Tazara, baiskeli, na malori ya mizigo yanayoenda kuchukua mpunga na mchele!
Abiria tulikuwa tunaning'inia juu ya machuma. Gari ikiyumba kidogo tu, unatamani kuirudisha kwa mikono!! Na kumbuka sasa hivi ni kiangazi! Masika ikifika ndiyo balaa zaidi.