Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Ahahahaa!! We jamaa Califonia akachungulie nini? Ugeni wangu uliochanganyika na uenyeji kuna siku nimekaa Califonia napiga maji ya Devi. Kama unavyojua kibofu kikaanza fujo.

Nimeenda washroom nilichokutana nacho ni balaa 🤣 acha niishie hapa.
Hapa nahitaji maelezo mkuu 😂😂
 
Dah! Siku nyingine ukishuka hapo Kisegese, mwambie boda akulete Mofu ili uje ule samaki wa Mto Kilombero. Msimu huu samaki aina Ndipi, njuju na ngogo; ni wengi sana. Ni mwendo tu wa kula na ubwabwa.

Halafu ushukuru siku hizi kuna bajaj, kuna bodaboda, kuna Noah, kuna TATA, nk. Miaka ya 90, usafiri pekee wa huko ulikuwa ni treni ya Tazara, baiskeli, na malori ya mizigo yanayoenda kuchukua mpunga na mchele!

Abiria tulikuwa tunaning'inia juu ya machuma. Gari ikiyumba kidogo tu, unatamani kuirudisha kwa mikono!! Na kumbuka sasa hivi ni kiangazi! Masika ikifika ndiyo balaa zaidi.
Nadhani kuna ulazima wa lami fasta kuwekwa maana kuna wanakijiji wengi sana
 
Ndio maana watu wa Morogoro bado wanalia sana na barabara,

Barabara zote zipo Morogoro mjini tu ndanindani hamna kitu

Halafu mkoa nao mi mkubwa sana, masaa manne mtu unasafiri ndani ya mkoa mmoja tu. Huu mkoa unatakiwa ugawanywe, watu wa ifakara na Mlimba wako mbali mno na Morogoro mjini, wako karibu na Njombe kuliko Morogoro mjini
Kwa hiyo ikigawanywa umbali kutoka eneo moja kwenda lingine unapungua?
 
Ukikuta sehem kuna noah usipele tata useme unarahisha itakula kwako,
Noah inaingia watu 10-15 tata inaingia abilia 40 kwaaana ww mwenye tata utakuwa hauja,I kwenye noa wakifika abilia 12 noah inatembea, mwenye tata uktega ukiwa na abilia 15 ikija noah wanashuka na kupanda noah
 
Kuna basi moja la saa 7 kama sikosei inaitwa SARDINI / SADINI hilo likienda leo linarud kesho alfajiri..

Ndani kuna chawa, viroboto kama wote, na siti zake ni 2 by 3 mlango mmoja.. ndani kunapakiwa kila aina ya mzigo.

Sasa usiombe ukae siti za nyuma nyuma alafu unataka kushuka😂 utachagua ushukie dirishani au utambae juu ya siti kama buibui.
Dah, aisee kuna maisha hapa bongo mtu wa town akisimuliwa haamini 😂
 
Dah! Siku nyingine ukishuka hapo Kisegese, mwambie boda akulete Mofu ili uje ule samaki wa Mto Kilombero. Msimu huu samaki aina Ndipi, njuju na ngogo; ni wengi sana. Ni mwendo tu wa kula na ubwabwa.

Halafu ushukuru siku hizi kuna bajaj, kuna bodaboda, kuna Noah, kuna TATA, nk. Miaka ya 90, usafiri pekee wa huko ulikuwa ni treni ya Tazara, baiskeli, na malori ya mizigo yanayoenda kuchukua mpunga na mchele!

Abiria tulikuwa tunaning'inia juu ya machuma. Gari ikiyumba kidogo tu, unatamani kuirudisha kwa mikono!! Na kumbuka sasa hivi ni kiangazi! Masika ikifika ndiyo balaa zaidi.
Dah mkuu umenikumbusha mbali miaka ya 2004 niliwahi kutoka ifakara kwenda malinyi ndan kidg kama kilosampepo usafiri ni trekta tu
 
Dah! Hiyo Califonia ndiyo Kahumba ya Ifakara hiyo!! Halafu zamani hata haikuwepo. Binafsi huwa nikija Ifakara, mara nyingi napenda kuweka kambi yale maeneo ya Posta. Kuna kuku wengi sana wa kuchoma nyakati za usiku.
Maeneo ya posta kidg kuna usalama pia lakini kwa sasa maeneo yaliochangamka ni mashimoni kwani kuna bar nying nzuri na za kisasa na hata ukicheki califonia nayo ipi line ya mashimoni
 
Dah mkuu umenikumbusha mbali miaka ya 2004 niliwahi kutoka ifakara kwenda malinyi ndan kidg kama kilosampepo usafiri ni trekta tu
Hahahaa raia kule wana maisha yao
 
Kusema kweli ukibaki Dar utahisi na wa mikoani kwingine kero zao ni foreni kama wewe. Kumbe uko ata magari tu hamna.
Na yaliopo Sasa!nakumbuka Kuna wakati Geita zile hiace fupiii kioo Cha pembeni kilinimwagikia chote na gari inaendelea TU driver na konda wanaongea kisukuma na abiria wanasikitika kisukuma huku wananiangalia na mi Niko na vioo vyangu hadi tunafika stend
 
Haha vile vidude navijua vifupi sana
 
Back
Top Bottom