Mlinzi Suma JKT ajiua kwa kujipiga risasi shingoni

Mshahara mdogo uki compare na kitu gani ?

Mshahara mkubwa ni sh. ngapi ?
Mkuu,mshahara mdg unajulikana bila kulinganisha na kitu chochote.
Mshahara wa laki moja kwa mwez kwa vyovyote vile ni mdogo
 
Mkuu,mshahara mdg unajulikana bila kulinganisha na kitu chochote.
Mshahara wa laki moja kwa mwez kwa vyovyote vile ni mdogo
Amekuuliza pia, mshahara mkubwa unaanza na ngapi??
kuna watu wanalipwa 600k nao wanalalamika kuliko askari wa suma!
 
Mkuu,mshahara mdg unajulikana bila kulinganisha na kitu chochote.
Mshahara wa laki moja kwa mwez kwa vyovyote vile ni mdogo
Ndio maana, nimekuuliza, mshahara mkubwa ni sh. ngapi ?


Kila unacho ongea lazima kiwe na Logic..
 
Mbeya ni mwendo wa risasi sasa, mwanzoni mwa wiki hii mmoja amempiga mwenzake risasi kisa shilingi 7,500
 
Afya ya akili ni tatizo kubwa sana kwa sasa, vijana tunasoma muda mrefu sana na tunatoka vyuoni na expectations nyingi sana ila tukifika mtaani hali ni tofauti sana na tunavyofikiri.

Vyombo vya ulinzi na usalama viangalie namna ya kuwasaidia hawa suma JKT, hasa hawa ambao wamekaa mda mrefu wawasambaze hata huko, imagine mtu na degree yako na GPA kali sana unakaa getini unatumwa soda na dogo mmoja hivi, unafungulia mageti masista duu wamejaa dharau na nyodo, sio mchezo.

Ugawaji wa silaha pia, hivi hakuna utaratibu wa kupima watu akili kwa kipindi fulani hata kwa hawa wanaomiliki silaha labda ndani ya miaka miwili unaenda kupimwa state ikoje? Au kwa askari pia hakuna utaratibu huo?

Ila kiuhalisia hali ni mbaya sana mitaani, vijana wanagraduate kila leo na kazi hakuna, na wa TZ akili ya kujiajiri ipo kwa wachache sana na mazingira bado ni magumu tu vilevile, ngoja tusubiri ripoti ya uchunguzi itasema pengine labda alisinzia ikafyatuka kama alivyosema mdau mmoja hapo juu
 
Tunaomba waajiri wote na taasisi mbalimbali kama za dini wawe wanatoa mafunzo ya afya akili mara kwa mara, vijana tumeelemewa🥴
 
Walinzi wa hii kampuni ni kama wana msongo wa mawazo maana muda mwingi wanapenda shari tu
Mshahara haukidhi mahitaji unategemea nini? hapo kuna mchuchu anamzingua, mwenye nyumba ana dai kodi huku mama kapiga simu 'mwanangu niongezee pesa niwahishe kwenye vikoba' akijua labda mwanae analipwa pesa ndefu kumbe angejua, naomba niishie hapo
 
Poleni wafiwa.
Alikuwa bado kijana mdogo sana, sijui alikuwa na changamoto gani za kimaisha?
 
Tatizo mshahara mdogo,nilikuwa nafanya intern hospital flani nikagundua wanapewa kidogo sana,nilikuwa nashare nao lunch
Kwanini Taasisi iliyo chini ya Serikali ina lipa mishahara midogo sana yano Suma jkt walipa mshahara wa laki na 80 kwa mwezi, kingine wana ajiri lasab C wengi sana

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Depression isee na unaweza kuta ni graduate huyo maana ndio wapo wengi huko suma..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…