Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

Sishangai kwani uyo mwamba si ndo alikuwa anamlinda Jiwe kwenye kampeni za 2015, Wakati hajachaguliwa kuwa Rais? Infact Mwana alikuwa amemis kuvaa gamba la CCM.
 
watu ni wasahaulifu sana! tulie na katiba ila kiukweli hii nchi ni ya chama kimoja japo tunaamnishwa ni ya vyama vingi! je mnajua urais mtu anaupata mara tuu anapoteuliwa na ccm na kuanza kulindwa na usalama? so kwa hili la leo mie sishangai. nawakumbusha kidogo 2015 mlizi wa rais wa sasa huyu nyuma yake ndiye alikua mlinz kwenye kampeni. sasa jiulizeni uvccm anaweza kuwa mlinzi wa rais? means usalama hutoa ulinz kwa mgombea wa ccm mara tuu anapoteuliwa na vikao!
 
Hizo mbinu akina Kikwete walikuwa hawazijui?
Unaelewa unachokiongea? Hawavai nguo sababu ya ushabiki, ni mbinu ya kublend in na crowd. Wewe umemuona huyo mmoja tu, wape wengi sana hapo ambao mtu wa kawaida atawagundua tu wachache wanaonekana karibu na mkuu. Fuatilia baadhi ya event za nyuma za JK, kuna walinzi walikuwa wanavaa hayo mashati.
 
Hao ni walinzi wa kisiasa wanaitwa Green guard,hata chadema wanao hao walinzi,so ni kawaida tu
 
Wanajukwaa naomba kuuliza hili la walinzi wa Rais Magufuli kuvaa sare za CCM limekaaje?

Siyo kawaida, hiyo ni kasoro kubwa sana ya kiufundi.

Huyo usalama wa taifa ni mtumishi wa 'vyombo vya ulinzi na usalama'.

Hivyo kikatiba na kisheria, watumishi wa kada ya 'ulinzi' hawana uanachama, kushabikia wala kuvaa sare ya chama chochote kile, kwao ni mwiko mkubwa unaofahamika na kila member.

Mapenzi na ushabiki unatakiwa uhifadhiwe moyoni mwa mtu binafsi na kisha ukafanyiwe ndani ya sanduku la kura pekee na si hadharani kuonesha askari huyo anashabikia nini ama upande gani, never.
 
Wenzako wako ki professional, wewe unatema pumba. Hivi Rais angekuwa wa Chadema, na hao walinzi wakavaa jezi ya Chadema ungelalamika?
Yani ccm nasikiaga hamna akili sasa nakubali!!! Hapo hata ingekua ACT ni sawa?? Ndio maana hata shule mnafeli mnabaki kufoji vyeti!! Kama DAB
 
Kwani nguo zake Za kazi Huyo mlinzi ni zipi? Anauniform Zake za kazi ambazo hakuvaa siku Hiyo? Au huwa anavaa kadiri ya mazingira ya siku Hiyo?
 
Mlinzi ana kadi ya CCM?
 
Zipo wapi zile trilion 1.5 zilizomtoa CAG kafara? Zipo wapi trilion 12 za Ndungai?
 
Presidential detail ana camouflage wakati identity yake iko compromised kitambo? Hiyo sura ya jamaa kila mtu anaijua so hahitaji kuwa undercover. Kma walinzi wa kisiri kibao tu wamejichanganya kwenye kadamnasi.

Rais ni post ya kisiasa ila TISS ni watumishi ambao kisheria hawapaswi kuwa na chama kabisa ssa nashangaa watu mmatetea humu wakati ni ukiukwaji sheria.
 
CCM wamevunja Sheria lakini kwa kuwa ni wababe sisi tutaishia kuwambia ukweli wajue watanzania siyo wajinga wanajua wamevunja katiba ya Nchi kuwavalisha vyombo vya dola nguo zao za CCM
 
Yawezekana kuna ukweli, unaonaje ukitupia picha ya aliyekuwa akimlinda Kikwete, Mkapa, Mwinyi au hata Nyerere akiwa na jezi za.CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…