Ngoja nikusaidie kitu, ukisoma sheria ya usalama wa Taifa ya Mwaka 1996 imeweka wazi kuwa watumishi wa Idara hiyo hawabanwi na sheria ya utumishi wa umma.
Hivyo unapaswa kuelewa kwamba kutokana na nature ya majukumu yao (kama ulivyoambiwa hapo juu, watu hao wapo kila sehemu, ikiwemo kwenye hivyo vyama vyenu), isingewezekana wao kufanya kazi katika mazingira yanayofanana na watumishi wengine wa umma.
Ni akili ya kawaida tu inahitajika kuweza kuelewa haya mambo. Soma zaidi ili ujenge uwezo wa kujenga hoja kwenye majukwaa kama haya.