Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

Hivi kama angeenda msikitini, Rais akavaa kanzu na walinzi wake pia wakawa sare nae kuna tatizo?
Mie sioni tatizo hapo
 
Hivi kama angeenda msikitini, rais akavaa kanzu na walinzi wake pia wakawa sare nae kuna tatizo?
Mie sioni tatizo hapo
Kama huoni tatizo fatilia tu mjadala labda utaona.

Maana we unafikiri TISS ni kama ulinzi shirikishi tu basi.. hiyo ni nchi ndugu,hicho kitengo ni mahususi. Huyo mlinzi unaemuona hapo alishawahi kupewa Mike msikitini akapiga Dua! Hilo sio tatizo maana misingi ya dini nchi yetu tunaijua ni sehemu ya imani.. Sasa kinchi kwa chombo Kama hicho kuvikwa nguo za chama fulani we huoni jambo lolote hapo.. hujui hao ndo usalama wa taifa?

Vyama vyengine viseme nini kama huo usalama wanavaa nguo za chama chengine, hao hawalindi mtu tu au chama bali wanalinda mtu atakae kuwa na cheo cha urais.. ndio maana nikaandika (cheo).. wanamlinda na makamu wa rais pamoja na waziri mkuu..

Open your eyes and mind..

Hivi we ukienda mahakamani ukakuta hakimu kavalia nguo za chama fulani balaza nalo hivyohivyo unafikiri wasio upande huo watafikiria nini?
Hapo unaweza sema mahakama ipo huru?

Hili jambo ni la kuhoji na wahusika wanahitajika kutoa ufafanuzi wa kina maana linaibua picha nyingi Sana..!
 
Mkiambiwa TISS wengi wamechukuliwa UVCCM mnaona tunachuki na CCM.
Hili swala si lakushangilia tu nakusema hoyeee..

Ikibidi mkuu wa TISS akalishwe mtu kati kabisa ahojiwe this is what..??
 
Nadhani ni namna yao ya kufanya kazi . mwaka 2015 niliona TIss wawili walio vaa mazezi ya kijani kwenye mkutano was Jiwe na nilikua nao pia kwenye mkutano wa Mzee wa mamvi wakiwa wamevalia majezi ya Chadema hadi kofia. Samajani sintoweka picha zao hapa najua hairuhusiwi
 
Hili si jambo geni, Mlinzi wa Raisi amekuwa akivaa nguo za CCM toka wakati wa kampeni 2015 kabla hata mjomba hajawa Raisi, ni chuki tu ulizonazo
 
Hili si jambo geni, Mlinzi wa Raisi amekuwa akivaa nguo za ccm toka wakati wa kampeni 2015 kabla hata mjomba hajawa Raisi, ni chuki tu ulizonazo
Chuki..!!!
Okay ni chuki tuishie hapo.
 
Wenzako wako ki professional, wewe unatema pumba. Hivi Rais angekuwa wa Chadema, na hao walinzi wakavaa jezi ya Chadema ungelalamika?
Unatapika upumbavu,
Walinzi ni wa serikali siyo wa chama
Askari hawatakiwi kuwa na vyama.
Kuwa na akili japo kidogo
 
Mkuu uprofessional kwa ccm ni kwa watumishi wa umma kuvaa sare za vyama vya siasa? Jamani wenzetu huu ujinga mmeusomea wapi? This is unsual
Mkuu ulirudia kusoma mara mbili kabla haujaandika haya maelezo? Humo kuna wakurugenzi, ma-DAS, waalimu, madaktari, wahadhiri, na wengine ambao ni watumishi wa umma lakini wanachama wa vyama vya siasa nao wamevaa sare za chama chao. Pia kuna watumishi wa umma waliokuwa upinzani wakavaa sare za chama chao.

Au umewasahau wahadhiri flani wa chama fulani cha upinzani walivaa sare za chama chao wakiwa hawajastaafu kazi vyuoni.

Hapa ungeuliza uhalali wa kufanya hivyo watumishi wa sekta za ulinzi na usalama tu lakini wengine hawazuiliwi na sheria wakiwa nje ya shughuli za kiserikali.

Mleta mada anayo hoja ya msingi kuhusu afisa wa usalama, lakini inaweza kuwa inaruhusiwa kwao kama njia ya kutojitofautisha na mazingira husika ili adui wasikutambue haraka wakati wa shambulio.
 
Yawezekana kuna ukweli, unaonaje ukitupia picha ya aliyekuwa akimlinda Kikwete, Mkapa, Mwinyi au hata Nyerere akiwa na jezi za.CCM
Picha siwezi kuzipata kwa sasa kuitafuta katika mamia maelfu ya mapicha online si kazi rahisi, ila ilikuwa enzi za JK akiwa katika kampeni ya moja ya mikoa, mmoja wa walinzi wake alikua mwembamba hivi kama mmasai alikuwa amevaa jezi ya kijani
 
Mbona naona mlinzi wa Rais amevaa ngo za Askari (wa kulia)? au hizo ni za chama?

Huyo alievaa za chama atakuwa Mlinzi wa mwenyekiti wa chama.
 
Mi naomba kuuliza
Hivi Hawa walinzi au huyu PSU hapo Alovaa nguo za chama na huyo wa nyuma.

1. Hawanaga bandama maana jamani hawacheki utakuta ukumbi mzima unacheka Ila hao hawachek are they trained to be that way even smiling kwenye kitu kinachosababisha kusmile.

2. Hawana familia?wanakutana nazo sa ngap??au zinakua zinaishi ikulu ??
 
Sidhan kama ni sahihi kwa secret servant kuvaa sare za chama cha siasa maana huyo ana jukumu la kutulinda wote hata tusio na vyama bila ya upendeleo wowote
 
Back
Top Bottom