Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

Mlinzi wa Rais kuvaa sare za chama ni sahihi?

They are justing blending with people and suroundings-camouflaging. Magari anayotumia mh JPM rangi yake kwa sasa umeiona?

Hata wale wa Lissu walikuwa wakifunika nyuso zao na hijabu vyekundu, kama magaidi ya Tamil tigers.
 
Kwa sasa magufuli ni mgombea lakini itifaki zingine kama rais znabaki palepale. Kwahyo kinachofanyika ni kama wale walinzi wanaazimwa na ccm kwani wao kama chama hawana watu wenye uwezo wa kumlinda 'rais' mfano hawawezi kutumia green guard kwan uwezo wao ni mdogo. Hivyo wale wameazimwa na chama kutoka serikalini na chama ndo hupaswa kuwagharamia angalia hata magari anayotumia ni ya chama(kwa muonekano wa rangi zake)
 
Hapo pa magari... Hapana, chuma zile zina wrap ya Chama.. Ni Mali ya JMT, sio Chama. Kuna utumiaji usio sahihi wa rasilimali za Umma kwenye kinyang'anyiro.
 
Wamebadilishwa mbona. Hao ni kwa ajili ya kampeni tu
 
Habarini Wakuu

Kuna jambo linanitatiza sana sana yani. Katika kampeni zilizoanza za Rais John Magufuli, amekuwa akionekana jukwaani na popote akiwa na walinzi waliovalia sare za kijani yaani CCM. Wale jamaa ni wa kitengo kabisa na hawapaswi kuwa na chama chochote kwani TISS ni chombo huru na hakipaswi ku-align kwenye chama chochote cha siasa. Sasa zile uniforms za kijani, nani kaziruhusu?

Najua humu kuna wanasheria na wadau wa ngazi za juu serikalini, naomba tusaidiane. Maana mimi naliona jambo la hatari sana hapa!
View attachment 1557686View attachment 1557690
Kwanza ungejiuliza why nguo ya jeshi ina mabaka mabaka na inafanana na msitu? Ukisha pata majibu basi ujuwe hata hivyo unawaona wanakuwa kiusalama zaidi wakiamua kumficha Rais hapo ningumu kumpata why they have same colour.
 
Katiba inakataza watumishi wa umma kujihusisha na shughuli za vyama vya siasa, hasa majeshi kwa namna yoyote ile. Kuvaa sare ya chama cha siasa ni dhahiri kuwa una mahaba na chama husika.

Liko wazi kuwa katiba yetu ina mapungufu juu ya Urais mara bunge linapovunjwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu, kwani Rais anaendelea mpaka mwingine atakapoapishwa.

Kama kifungu ndio kinafuatwa, kwa nini hao walinzi wa Rais wavae ki-CCM wakati wana sare zao rasmi? Hivi na walinzi wa wagombea wengine nao wanavaa sare za vyama vile? Nimeuliza hivi kwani hawa wa Rais sura zao na maumbile yao ya muonekano wa mwili kwa nje yanafahamika.

1600407600939.png

1600407854842.png

Je, hapa chini kwa Lissu kuna TISS?
1600407964760.png

1600408035985.png
 
Tanzania ni moja kati ya The Poorest Countries in the World inashika nafasi ya 8 kutoka chini. ( Focus economy 2019- 23)

CCM imetufikisha hapa.
 
Magufuli ana walinzi wa Serikali, kama Rais aliyeko madarakani, pia ana walinzi wa chama kiongozi mkuu. Nawe umeonyesha Lissu ana walinzi.

Mleta mada tafuta hoja nyingine ya kumwondoa Magufuli kwenye kampeni baada ya pingamizi la Lissu kutupiliwa mbali.
 
Jamaa wamejikita kwenye siasa kuhakikisha ccm inabaki madarakani.

Dunia imebadilika sana hiki chombo kwa dunia ya kwanza ndio Engine ya uchumi.
 
Usalama wa taifa anaweza jiweke vyovyote anavyoona inafaa ili aweze kutekeleza jukumu lake kwa ufanisi utumishi wa usalama wa Taifa ni utumishi tofauti kabisa na wowote unaoujua unatawaliwa na usiri uliotukuka kwa hiyo anaweza kujiweka vyovyote ili kile alichokikusudia akitimize kwa hiyo sioni ajabu kuvaa sare za ccm
 
Utumishi wa TISS Ni tofauti na wewe Mwalimu, elewa Hilo ndiyo maana hujawahi kuwaona kwenye mei mosi wameshika mabango!
 
Kwa sasa sio uvunjifu kabisa kwa sababu TISS ni Kitengo cha CCM, na kwahiyo wapo sawa tu kuvaa uniform za CCM!!

The so-called constitution ceased to work for almost 5 years now, and that being saidi, huwezi kuvunja kitu ambacho kilishavunjwa vunjwa miaka kadhaa iliyopita!

Una lingine Ndugu Mwananchi?
 
Katiba inakataza watumishi wa umma kujihusisha na shughuli za vyama vya siasa, hasa majeshi kwa namna yoyote ile. Kuvaa sare ya chama cha siasa ni dhahiri kuwa una mahaba na chama husika.

Liko wazi kuwa katiba yetu ina mapungufu juu ya Urais mara bunge linapovunjwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu, kwani Rais anaendelea mpaka mwingine atakapoapishwa.

Kama kifungu ndio kinafuatwa, kwa nini hao walinzi wa Rais wavae ki-CCM wakati wana sare zao rasmi? Hivi na walinzi wa wagombea wengine nao wanavaa sare za vyama vile? Nimeuliza hivi kwani hawa wa Rais sura zao na maumbile yao ya muonekano wa mwili kwa nje yanafahamika.

Huo sio usalama wa taifa ni usalama wa CCM.
 
Back
Top Bottom