Mlio karibu na Tundu Lissu mumkanye aache mara moja kuropoka ropoka!

Kuhatamia!
 
Pelekeni ujinga wenu kule enyi chawa na walamba asali mliovimbiwa. Anawapekesha kiasi cha kukosa usingizi, anaropoka nini wakati anasema ukweli? Tulieni watanzania wafumbuliwe macho waone uovu wenu
 

Ulimaanisha huyu huyu

Your browser is not able to display this video.
?

Au ulimaanisha mwingine ndugu?
 
Unapoteza muda wako kushinda mitandaoni unaongelea mtu ambaye sio level yako.
HIyo ya kwake inaitwa Obsessive-compulsive disorder (OCD)
OCD obsessions are repeated, persistent and unwanted thoughts.
OCD compulsions are repetitive behaviors that you feel driven to perform.
Huyu Mkunazi Njiwa asipoangalia atajikuta pabaya sana hivyo awahi matibabu.
 
Hizi kampeni zinasaidia sana viongozi wa siasa kuongea ukweli.Ungemsikiliza Cleopa Msuya Jana kwenye kipindi cha dakika 45,kinachorushwa na ITV hakukosoa hata kidogo movements za vyama vya upinzani.Ungeangalia vizuri aliwaponda vijana wa CCM kwamba hoja zao hazina mashiko kulingana hoja za upinzani.Aliona kama uvccm hawajasukwa kupambana na upinzani.
Na wala hawafanyi tafiti kulinganisha na upinzani.
 
Hana chakupoteza mwache aishi maisha aliyopangiwa na atimize jukumu alikopewa pale litakapo tumia atanyamaza mwenyewe na wala sio kulazimishwa.Maisha yake ni mpango wa Mungu naye anajua mwanzo na mwisho wake na sio binadamu.
 
Huwa siwajibu wapuuzi wa aina yako...

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nawe una DELUSION....

-Fixed and falsefull rigid thoughts kupingapinga tu KIHISIA....

Wahi hospitalini UTIBIWE.....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Dementia and Alzheimer's are really....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
ulitaka akutekenye wewe?
 
Sio ishu ya kushikiwa akili na mtu..

Ni suala la kusikia na pia binafsi kutafuta ukweli ya kile unachokisikia..

Hizi taarifa ziko mitandaoni ktk tovuti ya kampuni husika ikisema waziwazi hicho unachodhani wewe ni sisi "kushikiwa akili"

By the way, siyo ekari milioni 2 tu bali milioni 6.1 ktk maeneo ya hifadhi mbalimbali Tanzania..

Kinachotakiwa ni serikali na wahusika kukanusha au kuukiri ukweli huu na baada ya hapo wajibu maswali yanayofuata..

Soma👇👇

MWIBA HOLDINGS LTD

Uwepo wao Nchini Tanzania

Friedkin Conservation Fund ni shirika linaloshughulika na masuala ya mazingira, uhifadhi na utalii. Shirika hili limesajiliwa Marekani. The Friedkin Conservation Fund of Tanzania ambayo ni sehemu ya umiliki wao limeanzishwa nchini Tanzania kama shirika lisilotengeneza faida.

Katika tovuti yao rasmi, Shirika hilo limeandika;

"Shughuli zetu Tanzania zimesukumwa na dhamira yetu katika uhifadhi wa mazingira na moyo wa hisani. Tumewekeza mabilioni ya shilingi katika jamii ili kuzisaidia kukuza uchumi na kusaidia nchi hii nzuri tunayoipenda sana"

Aidha, Shirika hilo limeonesha makao yake makuu kuwa Jiji la Arusha limetaja mambo 3 ambayo ni dhamira yake kuwepo nchini ambayo ni;
Kusaidia Serikali ya Tanzania na wananchi wa wake kwa juhudi zao za kuhifadhi mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa.
Kuhirikisha jamii za vijijini katika uhifadhi wa urithi wao wa asili na kuwawezesha kupunguza baadhi ya hali zinazochangia umaskini.
Kufuatilia, kutafiti na kuwezesha mipango katika matumizi endelevu ya maliasili.

Uhifadhi wa Ardhi
Kwa mujibu wa tovuti ya Tanzania Invest, Friedkin Conservation Trust inahifadhi takriban ekari milioni 6.1 zilizoko kaskazini mwa Tanzania. Aidha Ekari 300,000 za hifadhi za Friedkin huruhusu wageni kutembelea na kuona wanyama kwenye mbuga ya Serengeti.

Madai haya yanathibitishwa pia na Blog hii inayohusianishwa na Taasisi hiyo. Aidha, Mwaka 2017, Mtumiaji mmoja wa JamiiForums aliwahi kuweka chapisho ambalo pamoja na mambo mengine lilikuwa linaonesha uwepo wa Taasisi hii kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mwaka 2015, Friedkin Conversation Trust iliipa Tanzania Tsh Bilioni 231.55 ili kulinda mazingira na kukuza utalii.

Kazi zao nchini Tanzania zinatajwa kuanza miaka ya 1989 na Thomas Friedkin, Baba mzazi wa Dan Friedkin aliyefariki Machi 14, 2017 akiwa na umri wa miaka 81.

Hata hivyo, ingawa vyanzo kadhaa, ikiwemo makala katika jarida la Forbes inayosema kwamba taasisi inayomilikiwa na familia Freiedkin – yaani Friedkin Conservation Fund (friedkinfund.org) – imekodisha ekari milioni 6 za pori la Tanzania kwa lengo la kuzilinda, wawakilishi wa bilionea huyo walikanusha madai hayo.

"Friedkin Conservation Fund ni shirika la misaada lisilo la faida ambalo wadhamini wake ni Watanzania, na Dan Friedkin akiwa mfadhili ili kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii," alinukuliwa akisema mwakilishi huyo.

Aidha, Septemba 4, 2023, Mwiba Holdings Limited na Thomas Dan Friedkin walitoa taarifa nyingine inayokanusha madai ya kumiliki eneo linalofikia ekari milioni 6 nchini Tanzania.

Sehemu ya taarifa yao iliyotolewa kwa umma ilisema jumla ya eneo lote lililopangishwa kwa kampuni ya Mwiba Holdings Limited wilayani Meatu ni kiasi cha ekari 171,604 - na si ekari milioni 6 kama inavyodaiwa na wale waliowaita kuwa ni wazushi.

Aidha, taarifa hiyo ilibainisha kuwa Kampuni ya Mwiba Holdings haimiliki eneo lolote kwenye maeneo ya hifadhi nchini Tanzania na kuwa haijaingia mkataba wowote (moja kwa moja au kupitia kwa mtu au taasisi nyingine) na Serikali ya Awamu ya
Sita.

Mikataba yote ya UPANGAJI na UWEKEZAJI imekuwepo kwa muda mrefu na iliongezewa muda mwaka 2018 na 2019 wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.
 

Tumaini yetu ipo kwa Lissu na TEC
 
Mlio karibu na Samia mwambieni kuwa aache mara moja kuhamasisha ufisadi kwenye nchi yetu
Your browser is not able to display this video.
 
Nini HIKI!?aibu naona Mimi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…