Mkuu
Rutashubanyuma
Umeongea ukweli na pia umechambua vizuri kwa kina.
Lissu hataki kukubali kwamba yeye ana kasoro.hafanyi tafakuri kabla ya kutamka jambo.
Lissu ni mfuasi wa sifa bila kujali athari zitakazotokaba na utafutaji sifa wake.
Yuko radhi kuwavunjia heshima wenzake ili mradi yeye asifiwe kwa walioko mbele yake.kwa ujumla Lissu ni mbinafsi na mtu wa Visasi.
Hana staha ya kiuongozi na kweli sio Presidential Material.Ni bahati tu kwamba yuko kwenye chama ambacho
"Code& Conduct" sio kipaumbele chao.
Kuhusu Ngorongoro pia uko sahihi isipokuwa idadi uliyoitaja ya Wamasai ni ndogo kuliko uhalisia.
Na ni kweli wanatishia uoto wa asili na mali kale zilizohifadhiwa hapo Ngorongoro kwa faida za kiuchumi kupitia utalii na kihistoria na ndio maana pale ni mojawapo ta maeneo ambayo yanaangaliwa pia na kuhifadhiwa na taasisi za kimataifa kama UNESCO,AWF na FZS.
Kuendelea kuwaacha wamasai na mifugo yao kuongezeka ndani ya hifadhi ni hasara kubwa kwa taifa kuliko madhara ya kuwahamishia eneo lingine tofauti na hapo.
Pia uko sahihi kuliona suala la kuwapeleka eneo tofauti na Handeni.
Kwa pale Sonjo, Sale na Digodigo tayari palikwisha kuwa na migogoro ya kugombea ardhi baina ya jamii mbili tofauti za Wamasai na Wasomjo.
Na hata kuwahi kupiteza maisha ya mamia ya watu huko nyuma.
Hivyo ni jambo ambalo halingewezekana....
Lakini ninayo imani kwamba kuna maeneo mengine pembezoni mwa Monduli na Longido ambako ingefaa zaidi kuwa mbadala wa Handeni.
Na pia wangeendelea kuishi na kutengamana na jamii zao za kimasai na kuzidi kuimarisha na kuudumisha utamaduni na Mila zao za kiasili kwa pamoja.
Tofauti na Handeni ambako wanakwenda kuwa jamii iliyoxungukwa na tamaduni tofauti za kisambaa,Kibondei na kizigua.
Naomba niishie hapo kwa sasa!