Kwanza Break Even haina maana biashara ikutegemee wewe kama ulivyoandika.BEP ni hali ya biashara kutozalisha faida wala hasara.Kwa atakayepitia hapa nafikiri mjinga atamuona ni nani kulingana na comment zetu,sina hofu wala uoga kimaisha naishi maisha ya kawaida kabisa amabayo nasema Mwenyezi Mungu asante (Hivi wakati mwingine mnaposhindwa kukoment kistaarabu mnapungukiwa nini? Hili ni jukwaa tu sio hukukumu wala hatuwezi kumlazimisha aliyeoomba ushauri aamue kama sie tunavyotaka ),safari ya biashara ina kitu inaitwa break even period,ni kipindi ambacho biashara lazima ikutegemee kabla hujaitegemea,ok...sawa nakubaliana na wewe kazi aache kabla hajaanza kuisoma " return" ya biashara atakuwa na mkondo gani wa kuimarisha biashara hiyo?,kumbuka maisha ya kila siku yanahitaji pesa itoke ndani "and at the same time" hujaisoma poa return ya biashara, akikurupuka kuacha kazi atakumbuka.Kaka hata sisi pia ni waajiriwa lakini "at the same time" tunaujasilia mali na maisha yanasonga.
Narudia tena kazi asiaache mpake aweze kusoma return ya biashara imekaaje,kwani kazi ni jela hawezi kuwa muuajiriwa na mwisho awa siku mambo yakisimama wima kazi unaacha ?maisha ya biashara sio 1+1=2.
ABUBAKAR SHEKAU ameshakueleza kwamba ameshaona return ya kilimo biashara unataka aone return ipi ndio aache kazi wakati ameshaeleza kilimo kinalipa.
Hata ukiwa kwenye kazi haina maana kuwa upo salama,kuna matukio mengi ambayo yanaweza kutokea na kuharibu maisha yako yote kuliko hata kilimo biashara unachoofia.Mfano kufukuzwa kazi,kuumwa,kupatwa ajali,au majanga mabaya ya kusingiziwa ukafungwa.Hata mie ni Mfanyakazi wa serikali nimeona matukio mengi watu wanakumbana nayo hata mengine yameshawai kunikuta.
Acha kumtia uoga mwenzako la muhimu hakuna kazi ya kuajiriwa au kujiajiri isiyo na changamoto. ABUBAKAR yupo vizuri muache aache kazi ya kuajiriwa akafanye kazi ya kujiajiri kwa muda mwingi itamlipa.