Habar wanajamvi mimi ni Muajiriwa katika shirika Moja lisilo la kiserikali na kazi ninayo jishuhulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo na pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, wa mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shuhuli zangu za kilimo na ufugaji. Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
Mm nina miez kadhaa tangu nimejing'atua selikalini, mpaka sasa changamoto ninayoipata ni jamii, ndugu na marafiki kuniona kama nimetenda dhambi, ama kama sina akili timamu... jambo ambalo linapelekea kutowamini tena niliokuwa ninawaamini coz wanakuwa kinyume na fıkra zangu, hata ninaowaona kuniunga mkono ninaona Unafiki flani...
So kwa uzoefu wangu mdogo nina haya kwaajiri yako
1.nafikiri ni muhimu kujidhatiti vilivyo kimawazo na msawazo wa akili ili hata ukipitia vipindi vigumu uweze kujikwamua mwenyewe. Yaani kutegemea zaidi nguvu iliyopo ndani yako Mwenyewe.
2.Hadhi yako itabadilika(kimwinekano), japo sijui unafanya nini kwa sasa lkn kwa kuwa utakuwa mjasilia mali ile kuonekana Nadhifu kutapungua na kama ilivyo kwa wengi yamkini ukachukuliwa kama mtu mwenye hadhi ya chini, japo huenda sio. So chukulia poa.
3.kuwa na muda mdogo wa kupumzika.
Hii ınaweza kuwa changamoto au la! Mkiwa kwenye Ajira mnamuda wa kurepot kazini na kuondoka, lkn ukijiajiri hiyokitu haizingatiwi sana(utaendeshwa na Malengo/Shahuku ama hali ya mambo kwa ujumla, mfano unaweza ukawa unafanya kaz ya watu wawili had wanne ili kupunguza gharama za uendeshaji hivyo kuwa na muda mfupi wa kupumzika.... hata ivyo uzur ni kwamba matokeo ya kutumika huko yanakuwa ni yakwako mwenyewe[emoji4] .
4.Changamoto ya mfumo mpya wa maisha.
Ukiamua kujiajiri mwenyewe tena kwa kuacha Ajira flani unakuwa na changamoto ya kuwa na mfumo mpya wa maisha, kama kuwa na marafiki wachache kwakuwa hutokuwa na muda wa kutosha kuwekeza kwa marafiki.. na ukifanikiwa utaonekana unajidai, ama utainekana unadharau na mengine kemkem.... lkn mm nashauri kuwa imara hilo likitokea, usitake sana kuridhisha watu na kuhalalisha kujihujumu kwa kupoteza muda ama pesa! Kataa.
Ninamuda mfupi huku nje kama nilivosema so changamoto zaidi bado, zaidzaid mambo yanaenda vzur japo ni mapema mno kunitumia mimi kama usahihi wa hilo jambo.
Ukihitaji ushauri ama kujadili zaid twende kando.