Kama kazi sio ya maana haina security yoyote wala maslahi naomba iache haraka. nenda kajiajiri.Habar wanajamvi mimi ni Muajiriwa katika shirika Moja lisilo la kiserikali na kazi ninayo jishuhulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo na pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, wa mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shuhuli zangu za kilimo na ufugaji. Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
Mm nina miez kadhaa tangu nimejing'atua selikalini, mpaka sasa changamoto ninayoipata ni jamii, ndugu na marafiki kuniona kama nimetenda dhambi, ama kama sina akili timamu... jambo ambalo linapelekea kutowamini tena niliokuwa ninawaamini coz wanakuwa kinyume na fıkra zangu, hata ninaowaona kuniunga mkono ninaona Unafiki flani...Habar wanajamvi mimi ni Muajiriwa katika shirika Moja lisilo la kiserikali na kazi ninayo jishuhulisha nayo nje ya ajira yangu ni kilimo na pia nina malengo ya kufuga kuku wa aina zote yaani chotara, wa mayai na wanyama na malengo yangu ni kuacha kazi na kusimamia shuhuli zangu za kilimo na ufugaji. Sasa wadau ambao mliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri wenyewe mlipitia changamoto gani pindi Mlipoacha kazi.
Thanks MkuuMm nina miez kadhaa tangu nimejing'atua selikalini, mpaka sasa changamoto ninayoipata ni jamii, ndugu na marafiki kuniona kama nimetenda dhambi, ama kama sina akili timamu... jambo ambalo linapelekea kutowamini tena niliokuwa ninawaamini coz wanakuwa kinyume na fıkra zangu, hata ninaowaona kuniunga mkono ninaona Unafiki flani...
So kwa uzoefu wangu mdogo nina haya kwaajiri yako
1.nafikiri ni muhimu kujidhatiti vilivyo kimawazo na msawazo wa akili ili hata ukipitia vipindi vigumu uweze kujikwamua mwenyewe. Yaani kutegemea zaidi nguvu iliyopo ndani yako Mwenyewe.
2.Hadhi yako itabadilika(kimwinekano), japo sijui unafanya nini kwa sasa lkn kwa kuwa utakuwa mjasilia mali ile kuonekana Nadhifu kutapungua na kama ilivyo kwa wengi yamkini ukachukuliwa kama mtu mwenye hadhi ya chini, japo huenda sio. So chukulia poa.
3.kuwa na muda mdogo wa kupumzika.
Hii ınaweza kuwa changamoto au la! Mkiwa kwenye Ajira mnamuda wa kurepot kazini na kuondoka, lkn ukijiajiri hiyokitu haizingatiwi sana(utaendeshwa na Malengo/Shahuku ama hali ya mambo kwa ujumla, mfano unaweza ukawa unafanya kaz ya watu wawili had wanne ili kupunguza gharama za uendeshaji hivyo kuwa na muda mfupi wa kupumzika.... hata ivyo uzur ni kwamba matokeo ya kutumika huko yanakuwa ni yakwako mwenyewe[emoji4] .
4.Changamoto ya mfumo mpya wa maisha.
Ukiamua kujiajiri mwenyewe tena kwa kuacha Ajira flani unakuwa na changamoto ya kuwa na mfumo mpya wa maisha, kama kuwa na marafiki wachache kwakuwa hutokuwa na muda wa kutosha kuwekeza kwa marafiki.. na ukifanikiwa utaonekana unajidai, ama utainekana unadharau na mengine kemkem.... lkn mm nashauri kuwa imara hilo likitokea, usitake sana kuridhisha watu na kuhalalisha kujihujumu kwa kupoteza muda ama pesa! Kataa.
Ninamuda mfupi huku nje kama nilivosema so changamoto zaidi bado, zaidzaid mambo yanaenda vzur japo ni mapema mno kunitumia mimi kama usahihi wa hilo jambo.
Ukihitaji ushauri ama kujadili zaid twende kando.
Pamoja ndugu, tunaweza wasiliana pia kama ukihiyari, weka namba ya simu yako kama unatumia watsapThanks Mkuu
Kwa hiyo unataka kusema wenye familia wote wameajiriwa, au kuna mda ukipita huwezi kujiajii, basi wastaafu wanahari mbaya kama ndo ivoUna umri gani? Je una familia? Hayo ni maswali mazuri ya kuzingatia!
Kama umri wako ni chini ya miaka 30 na hujaoa acha kazi fasta na ujiajiri hata kama mtaji ni kidogo, utakua Nao!
Lakini kama una umri zaidi ya 35! Au kama tayari una familia usithubutu kuacha ajira Bali ajiri mtu asimamie miradi yako!
Safi saana nafikiri ungefata ushauri huu ni mzuri fanya kazi kwa juhud kuajiriwa hakuna ishuKaribu sana mdau labda nikutie Moyo tu kwa uamuzi wako na nikupe mfano wa kosa linalofanywa na wengi walio ajiriwa. Kuna watu kama wewe huanzisha miradi hii na kuajiri watu waisimamie, unakuta anayesimamia haifanyi kazi ipsavyo ila atakuibia kidogo kidogo na akiondoka anaanzisha biashara kama hiyo bila wewe kufahamu alikuwa anakuibia kiasi cha kupata mtaji. Tunaona vijana wengi wanavyo ajiriwa kwenye maduka hasa ya rejareja na kuacha kazi baadae na kufungua maduka binafsi wakati mshahara wake ulikuwa elfu hamsini au laki. Sasa aliyemuajiri angeacha hiyo kazi anayofanya na akasimamia mradi mwenyewe si mradi ungemtoa?
Kikubwa kuwa jasiri na ujue kujifariji maana kuna nyakati mambo yanaweza kuwa hovyo ukawaza kurudi kuajiriwa. Self motivation is key to succeed in this. Kila la heri.
Nimecheka sana eti Hongo Ila ndio ukweli unaweza kupewa Mshahara mkubwa ili uwezo wako wakufikiri uishie hapo!Mshahara ni Hongo ya kukufanya uachane na Drean zako, na u implement dream za watu wengine hasa walio kuajiri
Ndugu lengo Langu ni kuacha kazi ndugu ili nisimamie mambo yangu mwenyewe
usiache wewe tafuta mfanya kazi akusaidiage tuu
We jamaa jasiri sana! Kiukweli umeeleza ule ukweli wenyewe! Unavoacha kazi hata mkeo atachukia sana na anaweza hata kukununia. Ndugu wa karibu ndio watakuwa wakosoaji wako wakuu huku wakisubiri kushuhudia anguko lako! Maneno yao ni "Wewe unajidai unaacha kazi, tutaona". Msemo huo maana yake wanasubiri kushuhudia anguko lako. Ukiwa na moyo rahisi utarudi kazini.kama kazi sio ya maana haina security yoyote wala maslahi naomba iache haraka. nenda kajiajiri
Hii ndio experience halisi, unapaswa kuwa motivational speaker mkuu. Umeniongezea confidence siku nikiamua kuacha kibarua changu mkuu.Ajira humfanya mtu kuwa muoga na kutojiamini hakuna tajir mwajiriwa hata wakat mwingine mwajiriwa akipewa ridandas huzimia wengine hufa na akati anaelimu yake mfano mimi binafsi nilikuwa mwajiriwa tena serikalini nikapata shamba karibu na kisima kikubwa cha maji nikalima ekari mbili za kitunguu nikaajiri vijana Mimi nikaendelea kuwajibika huko kazini nikawapa na pump ya maji matokeo wakawa hawamwagilii, mbolea wakauza wanalewa na mashine ikaibiwa nikaishia kupata gunia 30 ambazo zilirudisha gharama baadae nikalima tena ekar mbili zao hilo nikaweka mbolea mwenyewe nilikuwa likizo nikanunua machine nyingine akati vinakaribia kukomaa bosi akaanza kunibania ruhusa ikabidi nifoji ugonjwa nikahamia shamba nikavuna magunia 147 nikapata 12 milion mwaka uliofuata nikashindwa kulima kutokana na ubize wa kibarua mwaka uliofuata nikalima ekar 3 vitunguu na ekar 4 mahindi ya kumwagilia ya kuchoma nilipoona mazao yanakuja vizuri nikajiripua kuacha kazi nikabahatisha kupata jumla ya 19 milion hapo mazao hayakuja vizur nikaacha kazi mazima nimefanya kazi miaka 11 cjapandishwa daraja na akati naacha kazi nilikuwa nalipwa laki 6 lakini kwa sasa kipato cha shambani ni sawa na kipato cha 3.7 million kwa mwezi ninachokushaur fanya utafiti wewe mwenyewe na ujiridhishe kuchukuwa uamuz wakati mwingine huna haja ya kuuliza watu utapandikizwa uoga wa ajabu na ndoto zako zikafa kumbuka humu ndani kuna watu wanalipwa laki 2 kwa mwez lakini nyumbani kwao kuna maeneo makubwa ya uwekezaji lakini kang'ang'ania kibarua huyu akijapigwa ridanda anafia ofisini
Unfortunately, sijasoma comments zote, ila kutokana na uzoefu wangu, ukiwa mwajiriwa na unaendelea na biashara, hakuna point itafika useme mambo ya biashara yamesimama vizuri, so ni wakati muafaka wa kuacha kazi. Mara nyingi watu wa namna hiyo huwa wanaacha kazi pindi wanapostaafu. Ambapo kibiashara nafikiri at that age, inakua a little too late for them.Kwa atakayepitia hapa nafikiri mjinga atamuona ni nani kulingana na comment zetu,sina hofu wala uoga kimaisha naishi maisha ya kawaida kabisa amabayo nasema Mwenyezi Mungu asante (Hivi wakati mwingine mnaposhindwa kukoment kistaarabu mnapungukiwa nini? Hili ni jukwaa tu sio hukukumu wala hatuwezi kumlazimisha aliyeoomba ushauri aamue kama sie tunavyotaka ),safari ya biashara ina kitu inaitwa break even period,ni kipindi ambacho biashara lazima ikutegemee kabla hujaitegemea,ok...sawa nakubaliana na wewe kazi aache kabla hajaanza kuisoma " return" ya biashara atakuwa na mkondo gani wa kuimarisha biashara hiyo?,kumbuka maisha ya kila siku yanahitaji pesa itoke ndani "and at the same time" hujaisoma poa return ya biashara, akikurupuka kuacha kazi atakumbuka.Kaka hata sisi pia ni waajiriwa lakini "at the same time" tunaujasilia mali na maisha yanasonga.
Narudia tena kazi asiaache mpake aweze kusoma return ya biashara imekaaje,kwani kazi ni jela hawezi kuwa muuajiriwa na mwisho awa siku mambo yakisimama wima kazi unaacha ?maisha ya biashara sio 1+1=2.