Wakuu heshima kwenu,
Nakuja hapa nikiwa na Tatizo moja kubwa sana la unywaji wa Pombe (Beer). Tatizo hili limekuwa kubwa sana kiasi kwamba ni kama nashindwa kuji-control hasa ninapokuwa na pesa mfukoni, Yaani nikiwa na pesa tu basi nitatafuta kiwanja nitapiga mitungi mpaka mida mibaya na kesho yake kuendelea tena hivyo hvyo angalau mpaka pesa ile iishe.
Pombe imeniletea matatizo makubwa hasa kifamilia, Nimegombana na Wife nimegombana na michepuko na nimegombana na ndugu pia. Kwa ufupi ni kama nimetengana na wife kwa namna fulani maana kila mtu anakaa kwake kwa sasa.
Pombe imenisababishia kupata ajali na kupoteza gari yangu nzuri kabisa.
Pombe inaniingiza kwenye hasara nyingi kwenye biashara na kazini, Kwani kuna wakati nakuwa na hela ya offisi ila mm naamua kuipasua pombe na kunywesha watu mpaka inaisha. Imagine naweza kuteketeza laki 8 ndani ya siku mbili au Tatu, Na nisijue imeenda wapi.
Pombe imeniingiza kwenye madeni mengi hasa kwenye Bar mbalimbali wanazoniamini maana wanajua mm ni mnywaji na mlipaji mzuri so huwa wananikopesha mpaka kiwango cha malaki kadhaa na mwisho wa siku najikuta nimeingia kwenye madeni kama hayo.
Pombe pia imeniingiza kwenye madeni na marafiki na ndugu mbalimbali ambao huwa wananikopesha na mimi kushindwa kurejesha maana kuliko nilipe deni ni bora nikakae kwanza ninywe beer mbili tatu nikiwa nafikiria kukulipa hilo deni lako ndugu mdeni.
Pombe inanifanya nashindwa kwenda kanisani Jumapili maana kila jumapili asubuhi nakuwa nipo hoi either kwa pombe za jana yake au kwa pombe nilizoanza kuzipasua jumapili hiyohiyo asubuhi.
Jamani ndugu zangu nafanyaje kuachana na huyu adui pombe, Hapa nilipo nasubiri saa 11 ifike nikapate kitimoto then nianze kushushia vitu.
Pombe inanifanya nasahau kununua nguo nzuri na viatu naona ni bora pesa nipeleke Bar , Yaani kuliko nikafanye shopping ya Laki mbili ni bora hiyo hela nikainywe beer za laki mbili.
Pombe inanifanya sasa nasahau au nashindwa kutuma mahitaji ya watoto kwanzia shule na nyumbani.
Mimi sio mtu wa wanawake sana ila kuna wakati pombe inanifanya pia najiingiza kwenye mambo ya Uzinzi japo ni mara mojamoja ila huwa najuta sana.
Jamani ndugu zangu nafanyaje mimi?
Huwa najaribu kuacha mara kadhaa lakini nikija kurudi ndio inakuwa balaa zaidi yaani inakuwa mara tatu ya ule unywaji kabla ya kuacha.
Kuna muda natamani hii inchi yetu ingekuwa kama zile nchi za waislamu ambazo hawaruhusu pombe , maana ingekuwa hivyo kweli ningeacha. Ila sasa ndio kila nikipita barabarani naona matangazo ya beer, Nikisikiliza redio naona beer yaani ni mtihani kwa kweli
Hapa napoandika huu uzi pia nawaomba kama kuna mtu humu anataka kunishauri basi tukutane tunywe beer mbili tatu tukiendelea kujadili hii pombe naiachaje. Maana imekuwa disaster
Baada ya kusema hayo yote tafadhali naomba ushauri wenu kwa ambao mmefanikiwa kuachana na pombe mlifanyafanyaje , TAFADHAL SANA naomba ushauri wenu
MWISHO WA UZI
View attachment 2495275