Mliobahatika kuacha unywaji wa pombe mlitumia formular gani?

Mliobahatika kuacha unywaji wa pombe mlitumia formular gani?

Formula yangu nilivyoanza kufuga dread zikawa Zinanicost kuliko kiwango nachotumia kwenye pombe Basi nikaona nichague moja na ofa nazikimbia..mwaka Sasa sijanywa na Sina habari
 
Wakuu
Kiukweli I had a plan kuacha kunywa pombe this year ila nashindwa kabisa.mfano toka Wednesday ya week hii sijagusa kabisa pombe ila leo nimeamka na kiu ya hatari,nikaona nikajiboost kidogo.i feel sorry for me ,na natamani kuachana na hii addiction but nashindwa.
Nyie wenzangu mliobahatika kuachana na unywaji wa pombe mlitumia formular gani kuachana na hii addiction?
Kuacha ni ngumu ila unaweza kupumzika
 
Jibu la kisaikolojia rahisi sana.

Kumbuka pombe sio addiction ni obsession tu

Naweza kusema kuwa kuna sababu moja au kadhaa zinazokufanya uiwaze pombe.

Mimi binafs nikiwaza kitu hata kidogo vp nikiona kinanipa stress nakwwenda kupata pombe. Endapo nikapata faraja ingine kwa mtu au kwa kitu sinywi pombe.

Aniliacha ikabaki sababu nyingine ya pili. Marafiki zangu sina stress wala furaha wakinialika mahala pombe ipo sioni sababu ya kuacha.


So ukiwa na sababu ya kuacha na ukijua nini kinakufanya unywe bas imeisha.

Nianze kwa kukuuliza KWANINI UNATAKA KUACHA NA KWANINI HUWA UNAKUNYWA SABABU IPO.
Mi binafsi nataka kuacha maana naona natumia pesa nyingi kwenye pombe hadi nashindwa kufanya mambo ya maendeleo.Cha kushangza ata nikijaribu kuacha kunywa japo wiki mbili ,mirija yote ya kipato inakata(hakuna cha maana nafanya)[emoji57][emoji57]
 
Si kushauri uache jifunze tu kuimanage usiwe unakunywa kila siku tu
Umeshauri vzuri sana... Me mwenyew nashangaa watu wanaosema mtu aache pombe au anataka kuacha pombe... Pombe inatakiwa uweze kui control kiakili na kimwili...
Mimi nakunywa pombe ijumaa na jumamos pekee, jumapil naweza kunywa kama juma3 ni holiday, yaaan hapo nitakunywa kadri niwezavyo... Katkat ya wiki siwez kunywa pombe kwanza hata chupa 2 naona shida kumaliza...
 
Mimi tangu juzi mpaka Leo nijanywa kitu ambacho before sikuweza, pombe na umalaya vinaleta umasikini na vinamaliza sana sana pesa. Acha pombe utaona tu unavyoanza kung'aa sura ya utoto inarudi. Pombe imenizeesha kiasi ambacho wenzako wa umri mmoja wananisalimia shikamoo. Nina wakati mgumu sana wakuirudisha sura yangu aliyoniachia mama angu Enzi za uhai wake. Nimeshasema sitagusa asilani abadani pombe situmii tena, Malaya situmii tena. Nipo tayari kukaa hata miaka 5 bila sex mpaka hapo nitakapoowa
Rahisi sana kuongea
 
Wakuu
Kiukweli I had a plan kuacha kunywa pombe this year ila nashindwa kabisa.mfano toka Wednesday ya week hii sijagusa kabisa pombe ila leo nimeamka na kiu ya hatari,nikaona nikajiboost kidogo.i feel sorry for me ,na natamani kuachana na hii addiction but nashindwa.
Nyie wenzangu mliobahatika kuachana na unywaji wa pombe mlitumia formular gani kuachana na hii addiction?
Waambie watu wote wanaokuzunguka kuwa unataka kuacha pombe na wafanye kila namna usinywe.

Pressure na msukumo wao vitakufanya uache kabisa

Mfano ukitaka kunywa wao wanakuzuia, mkienda kwenye sherehe wa ahakikishe haugusi pombe hata kidogo, baada ya muda utaweza
 

Attachments

  • FTtjZlUXsAAsJPU.jpeg
    FTtjZlUXsAAsJPU.jpeg
    31.6 KB · Views: 7
Wakuu
Kiukweli I had a plan kuacha kunywa pombe this year ila nashindwa kabisa.mfano toka Wednesday ya week hii sijagusa kabisa pombe ila leo nimeamka na kiu ya hatari,nikaona nikajiboost kidogo.i feel sorry for me ,na natamani kuachana na hii addiction but nashindwa.
Nyie wenzangu mliobahatika kuachana na unywaji wa pombe mlitumia formular gani kuachana na hii addiction?
Mimi nilikunywa wiki nzima bila kula, nikaumwa na kulazwa hospitali. Nilipotoka nikaacha moja kwa moja!
Ebu jaribu hii itakusaidia.
 
Mi binafsi nataka kuacha maana naona natumia pesa nyingi kwenye pombe hadi nashindwa kufanya mambo ya maendeleo.Cha kushangza ata nikijaribu kuacha kunywa japo wiki mbili ,mirija yote ya kipato inakata(hakuna cha maana nafanya)[emoji57][emoji57]
kabla hujafanya matumizi tenga pesa weka benki hata 20k ya malengo yako kama unalenga kufungua kiwanda bas jua hio ndo kazi ya hio pesa inayobaki bas ibajeti na nyingine itunze au oa
 
Cha kwanza kabisa ni kuichukia pombe kwa dhati ya moyo wako huu ndio msingi, epuka kampuni/makundi yako ya awali kuwa siku za kwanza hasa ile miezi miwili ya kwanza. Kunywa maji mengi kila siku kusafisha sumu ya pombe mwilini hadi lita 4.5 kwa siku kwa uzito unaozidi kg 89 kuendelea. Nilikuwa mlevi kupindukia! Nimefanikiwa kuacha kabisa! Mwezi wa 5 huu.
 
Mi siachi pombe labda nipate tatizo la kiafya na wanaonishauri wananijua vizuri majibu nayowapaga hawarudii tena .
 
Pombe sio chakula kwamba usipokunywa unakufa kwa njaa, ukilijua hilo tu unaacha kunywa pombe unabaki unakunywa maji tu
 
Wakuu heshima kwenu,

Nakuja hapa nikiwa na Tatizo moja kubwa sana la unywaji wa Pombe (Beer). Tatizo hili limekuwa kubwa sana kiasi kwamba ni kama nashindwa kuji-control hasa ninapokuwa na pesa mfukoni, Yaani nikiwa na pesa tu basi nitatafuta kiwanja nitapiga mitungi mpaka mida mibaya na kesho yake kuendelea tena hivyo hvyo angalau mpaka pesa ile iishe.

Pombe imeniletea matatizo makubwa hasa kifamilia, Nimegombana na Wife nimegombana na michepuko na nimegombana na ndugu pia. Kwa ufupi ni kama nimetengana na wife kwa namna fulani maana kila mtu anakaa kwake kwa sasa.

Pombe imenisababishia kupata ajali na kupoteza gari yangu nzuri kabisa.

Pombe inaniingiza kwenye hasara nyingi kwenye biashara na kazini, Kwani kuna wakati nakuwa na hela ya offisi ila mm naamua kuipasua pombe na kunywesha watu mpaka inaisha. Imagine naweza kuteketeza laki 8 ndani ya siku mbili au Tatu, Na nisijue imeenda wapi.

Pombe imeniingiza kwenye madeni mengi hasa kwenye Bar mbalimbali wanazoniamini maana wanajua mm ni mnywaji na mlipaji mzuri so huwa wananikopesha mpaka kiwango cha malaki kadhaa na mwisho wa siku najikuta nimeingia kwenye madeni kama hayo.

Pombe pia imeniingiza kwenye madeni na marafiki na ndugu mbalimbali ambao huwa wananikopesha na mimi kushindwa kurejesha maana kuliko nilipe deni ni bora nikakae kwanza ninywe beer mbili tatu nikiwa nafikiria kukulipa hilo deni lako ndugu mdeni.

Pombe inanifanya nashindwa kwenda kanisani Jumapili maana kila jumapili asubuhi nakuwa nipo hoi either kwa pombe za jana yake au kwa pombe nilizoanza kuzipasua jumapili hiyohiyo asubuhi.

Jamani ndugu zangu nafanyaje kuachana na huyu adui pombe, Hapa nilipo nasubiri saa 11 ifike nikapate kitimoto then nianze kushushia vitu.

Pombe inanifanya nasahau kununua nguo nzuri na viatu naona ni bora pesa nipeleke Bar , Yaani kuliko nikafanye shopping ya Laki mbili ni bora hiyo hela nikainywe beer za laki mbili.

Pombe inanifanya sasa nasahau au nashindwa kutuma mahitaji ya watoto kwanzia shule na nyumbani.

Mimi sio mtu wa wanawake sana ila kuna wakati pombe inanifanya pia najiingiza kwenye mambo ya Uzinzi japo ni mara mojamoja ila huwa najuta sana.

Jamani ndugu zangu nafanyaje mimi?

Huwa najaribu kuacha mara kadhaa lakini nikija kurudi ndio inakuwa balaa zaidi yaani inakuwa mara tatu ya ule unywaji kabla ya kuacha.

Kuna muda natamani hii inchi yetu ingekuwa kama zile nchi za waislamu ambazo hawaruhusu pombe , maana ingekuwa hivyo kweli ningeacha. Ila sasa ndio kila nikipita barabarani naona matangazo ya beer, Nikisikiliza redio naona beer yaani ni mtihani kwa kweli

Hapa napoandika huu uzi pia nawaomba kama kuna mtu humu anataka kunishauri basi tukutane tunywe beer mbili tatu tukiendelea kujadili hii pombe naiachaje. Maana imekuwa disaster

Baada ya kusema hayo yote tafadhali naomba ushauri wenu kwa ambao mmefanikiwa kuachana na pombe mlifanyafanyaje , TAFADHAL SANA naomba ushauri wenu

MWISHO WA UZI

IMG_20230125_152433.jpg
 
Back
Top Bottom